Tanzania kuanza kununua umeme kutoka Ethiopia

Tanzania kuanza kununua umeme kutoka Ethiopia

Si tulikubaliana sisi ndio tutakaowauzia majirani baada ya mwlm Nyerere dam kukamilika ?
Vipi Tena gear inabadilika angani mbona
 
Tanzania inalenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme nchini kufuatia mpango wa kuanza kununua nishati hiyo kutoka Ethiopia.

Tayari mamlaka za nishati kutoka nchi hizo mbili zipo kwenue meza ya majadiliano kukubaliana kuhusu vifungu, vigezo na masharti ya makubaliana hayo ya miaka 20.

Katika makubaliano hayo, shirika la umeme la Ethiopia litakuwa linaiuzia Tanzania nishati ya umeme, kupitia shirika la TANESCO.

Kwa kuanzia, Tanzania inalenga kununua Megawati 100 za umeme kutoka Ethiopia, baada ya kukamiliaka kwa majadiliano ya awali.

" Lengo la mpango huu ni kuunganisha mradi wa umeme wa Afrika Mashariki na ule wa Kusini mwa Afrika, ambapo Tanzania itakuwa katikati ya miradi hiyo miwili. Kukamilika kwa huu mpango kutafanikisha kuuziana umeme kati ya nchi za Afrika Mashariki na zile za Kusini mwa Afrika." anaeleza Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa Umeme wa Nishati Jadilifu, kutoka wizara ya nishati nchini Tanzania.

"Mambo yote hayo yapo kwenye hatua za majadiliano ambayo hujulikana kitapları kama "Wheeling Charges Agreement." amesisitiza Luoga.

Kulingana na kamishna huyo, mkubaliano yakikamilika, Ethiopia itaanza kuiuzia umeme Tanzania.

Kupitia mradi huo pia Tanzania itakuwa imejitosheleza katika nishati ya umeme na hivyo kuwa na uwezo wa kuiuzia tena Ethiopia au nchi yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Chanzo TRT Afrika
Hii ni Serikali sugu sana na sijui lini itaamka katika usingizi mzito .Ukitaka maendeleo katika nchi yako jambo la mwanzo ni ENERGY ENERGY ENERGY pamoja na Maji hawzi kuja INVESTOR kuja kuwekeza ikiwa vitu hivo viwili hakuna .
Raisi Samia Suluhu Jenga kinu cha NUCLEAR ndio solution ya umeme Tanzania na mwengine utwauzia Kenya Uganda na Burundi na wote huo ndio muarubaini.Tatizo viongozi wetu hawana VISION.
 
Huyu ndio CHURA ninae mjua mm. Yy kukesha kwenye kigodoro siku 3. Ndio anacho weza zaidi.
All the best
 
Wakati wa gesi tulisema tutauza umeme stigula ilipokuwa inataka kujegwa tukaambiwa pia tutauza umeme sasa hayo mambo ya kununua umeme sijui yanatokea wapi Kwa kweli hii nchi inakatisha tamaa kabisa.
 
Maji wanayotumia Ethiopia kuzalisha umeme ni ya mto nile ambayo chanzo chake ni ziwa Victoria lililopo Tanzania, tunaenda kununua umeme kwao
 
Si walisema sisi ndio tuna umeme rahisi kuliko nchi yoyote Afrika hii. Sasa tunakwenda kununua tuliyo ghari?
 
Umeitika vyema, maana hii ni sawa na hadithi za Sungura na Fisi.

Ccm wameshajihakikishia kwamba watanzania ni wakupeleka wapendavyo..maana hawahoji chocolate.
 
Maelezo hayajanyooka. Ikumbukwe na sisi bwawa la Nyerere likikamilika tutakuwa na umeme mwingi kuliko matumizi

Ukiona mna umeme mwingi kuliko matumizi, kimbia upesi. Hiyo nchi itakuwa ya watu wanaobeti tu. Hawana wanachozalisha
 
Mnatuchanganya hasa wimbo unaoimbwa wa bwana la mwalimu Nyerere. Umeme wa nini tena?
 
Back
Top Bottom