Tanzania kuanza kununua umeme kutoka Ethiopia

Tanzania kuanza kununua umeme kutoka Ethiopia

Ukiwauliza TANESCO watakuambia haiwezekani tununue umeme kwa bei iliyopo sasa. Lengo wanataka tuminywe mpaka basi.
Inakuwaje wanasema wamezima mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gas, kwa kuwa umeme umekuwa mwingi matumizi machache, na leo hii wanunue umeme kutoka nje?
Nakumbuka kuna jamaa alisema umeme wa bwawa la Nyerere sio wetu ni biashara watafaidi mataifa jirani, nimeanza kuamini.
 
But why, si tuna Mwl Nyerere dam project? Na tulisema umeme wake utakuwa mwingi sana hadi kuuza nje..? Tukumbushane
 
But why, si tuna Mwl Nyerere dam project? Na tulisema umeme wake utakuwa mwingi sana hadi kuuza nje..? Tukumbushane
 
Habari haijaeleweka kulinganisha na ukweli wa habari yenyewe. Aliyeleta kakurupuka
Bahati mbaya kabisa wanaojadili nao wanajadili kwa kukurupuka hakuna anayejisumbua kujua hiyo taarifa ipo vipi

So sad

Home of GT😂
 
Hapa kulia bwawa la Mwl Nyerere, huku kushoto Tren ya SGR, katikati kasimama Mhabesh na Token ya umeme 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Hii nchi imekaa kimikakati ya upigaji kila eneo, yaani kuna mambo hua nikiyasikia naona kabisa nchi yangu nikama kichwa cha mwendawazimu tu bladi hell....☹️
Sio ni kama,,Ni kichwa cha Mwendawazimu
 
Tanzania inalenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme nchini kufuatia mpango wa kuanza kununua nishati hiyo kutoka Ethiopia.

Tayari mamlaka za nishati kutoka nchi hizo mbili zipo kwenye meza ya majadiliano kukubaliana kuhusu vifungu, vigezo na masharti ya makubaliana hayo ya miaka 20.

Katika makubaliano hayo, shirika la umeme la Ethiopia litakuwa linaiuzia Tanzania nishati ya umeme, kupitia shirika la TANESCO.

Soma:
Kwa kuanzia, Tanzania inalenga kununua Megawati 100 za umeme kutoka Ethiopia, baada ya kukamiliaka kwa majadiliano ya awali.

"Lengo la mpango huu ni kuunganisha mradi wa umeme wa Afrika Mashariki na ule wa Kusini mwa Afrika, ambapo Tanzania itakuwa katikati ya miradi hiyo miwili. Kukamilika kwa huu mpango kutafanikisha kuuziana umeme kati ya nchi za Afrika Mashariki na zile za Kusini mwa Afrika." anaeleza Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa Umeme wa Nishati Jadilifu, kutoka wizara ya nishati nchini Tanzania.

"Mambo yote hayo yapo kwenye hatua za majadiliano ambayo hujulikana kama "Wheeling Charges Agreement." amesisitiza Luoga.

Kulingana na kamishna huyo, makubaliano yakikamilika, Ethiopia itaanza kuiuzia umeme Tanzania.

Kupitia mradi huo pia Tanzania itakuwa imejitosheleza katika nishati ya umeme na hivyo kuwa na uwezo wa kuiuzia tena Ethiopia au nchi yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Chanzo TRT Afrika

Tusishangae Tanzania pale kupate pesa ni kuunda miradi isiyo na lazima ndiyo nzia ya mawaziri na wakurugenzi wa mashirika wanavyoiba. Watasema tender za mashine za maji mfano, mabasi ya mwendo kasi, vifaa........ yaani ni wizi mtupu
 
Back
Top Bottom