Tanzania inalenga kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme nchini kufuatia mpango wa kuanza kununua nishati hiyo kutoka Ethiopia.
Tayari mamlaka za nishati kutoka nchi hizo mbili zipo kwenue meza ya majadiliano kukubaliana kuhusu vifungu, vigezo na masharti ya makubaliana hayo ya miaka 20.
Katika makubaliano hayo, shirika la umeme la Ethiopia litakuwa linaiuzia Tanzania nishati ya umeme, kupitia shirika la TANESCO.
Kwa kuanzia, Tanzania inalenga kununua Megawati 100 za umeme kutoka Ethiopia, baada ya kukamiliaka kwa majadiliano ya awali.
" Lengo la mpango huu ni kuunganisha mradi wa umeme wa Afrika Mashariki na ule wa Kusini mwa Afrika, ambapo Tanzania itakuwa katikati ya miradi hiyo miwili. Kukamilika kwa huu mpango kutafanikisha kuuziana umeme kati ya nchi za Afrika Mashariki na zile za Kusini mwa Afrika." anaeleza Mhandisi Innocent Luoga, Kamishna wa Umeme wa Nishati Jadilifu, kutoka wizara ya nishati nchini Tanzania.
"Mambo yote hayo yapo kwenye hatua za majadiliano ambayo hujulikana kitapları kama "Wheeling Charges Agreement." amesisitiza Luoga.
Kulingana na kamishna huyo, mkubaliano yakikamilika, Ethiopia itaanza kuiuzia umeme Tanzania.
Kupitia mradi huo pia Tanzania itakuwa imejitosheleza katika nishati ya umeme na hivyo kuwa na uwezo wa kuiuzia tena Ethiopia au nchi yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Chanzo TRT Afrika