Tanzania kuanza kununua umeme kutoka Ethiopia

Wiki iliyopita Biteko alisikika akisema tuna ziada ya megawatt 400, sasa mnatuambia kuwa tutanunua megawatt 100, hivi mnataka tuelewe lipi?!
 
Mbona ilisemekana bwawa la Nyerere litazalisha mpaka umeme wa ziada?
 
Ngoja nipite kimya maanake naweza kutukana nikamletea Max Melo matatizo ambayo sio yake wala yeye aliesababisha.
 
Labda anaeelewa atusaidie kufafanua maana nikama tunarudi rivasi
 
Serikali kama chombo !hakina Nia ya dhati ya kutatua changamoto za wananchi kama hili la umeme!

Haiwezekani miaka zaidi ya 40 tunahangaika na umeme TU,Bado afya,elimu mbovu isiyojiajiri n.k!
 
Walisema Sasa hivi umeme unaozalishwa ni mwingi kuliko matumizi,hivyo umeme mwingine utauzwa nje ya nchi ie,Malawi,Zambia,na Kenya,Sasa inakuaje Tena tununue umeme wakati sisi tunauza?
 
Walisema Sasa hivi umeme unaozalishwa ni mwingi kuliko matumizi,hivyo umeme mwingine utauzwa nje ya nchi ie,Malawi,Zambia,na Kenya,Sasa inakuaje Tena tununue umeme wakati sisi tunauza?
Na mimi nilisikia vivyo hivyo!
 
Kwani ile mitambo yote Tisa haijakwisha kuwashwa...na sisi tuweze kuuza umeme nje ya nchi...?
 
Tuache tu. Hamna hata haja ya kujadili.
Cha muhimu ulipe kodi,pesa zikusanywe,ziende hazina,zichukuliwe na baadhi ya vuongozi wetu,wazitumie watakavyoona INAFAA.
Tuendelee kuhimizana kulipa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…