Tanzania Kuiuzia Umeme Kenya Bwawa la Nyerere Likikamilika. AfDB Yataka Mikataba ya Mauziano isainiwe haraka

Tanzania Kuiuzia Umeme Kenya Bwawa la Nyerere Likikamilika. AfDB Yataka Mikataba ya Mauziano isainiwe haraka

Aliyekwambia hatujafika nusu ya Kusambazia umeme ni nani?

Mahitaji yanazidi kuongezeka lakini sio Kwa Kasi ya kuweza kuzitumia hizo megawatt zote ndani ya miaka 4 ijayo.

Tuko uhuru Hadi Leo tuko kwenye megawatt 2,000 , unadhani hiyo ziada ya 1600 tunaweza ifikia Kwa miaka 4 ijayo?
Sihitaji kuambiwa kama umeme umeenea kote au bado, ninaona kwa macho yangu mkuu.
 
Tuko uhuru Hadi Leo tuko kwenye megawatt 2,000 , unadhani hiyo ziada ya 1600 tunaweza ifikia Kwa miaka 4 ijayo?
Hii sio hoja sahihi. Kama toka 2016 hadi 2023, umeme ulifika vijiji vingi zaidi kuliko 1960 hadi 2015, Si ajabu kufika 2030 vitongoji karibu vikawa na umeme, ni suala la vichocheo vya uchumi na uongozi.
 
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imezitaka Tanzania na Kenya kusaini mikataba mitatu ya Mauziano ya umeme haraka Kufuatia kukamilika Kwa mradi wa kuunganisha gridi ya Nchi hizo mbili ambao umefadhiliwa na African Development Bank.

View: https://www.instagram.com/p/C27F55go1Cz/?igsh=emo4eGo4cDQ3d3li

My Take
Kenya wangekuwa wameunganisha grid Yao na Ethiopia,shida za upungufu wa umeme tunazopta saizi zisingekuwepo.

Umeme haututoshi wenyewe stori za kitoto za kuuza 😂 Treni ya umeme mnafikiri tatizo mpaka leo ni nini? Umeme hatuna😂 ndiyo maana mradi unasubiri umeme. Yaani kwa umeme wote pamoja na bwawa haututoshi kabisa hasa ukizingatia vijijini hakuna umeme kwenye kaya
 
Huu upuuzi ulikuwa tangu enzi za JK, ni story za baba kumwambia mwanae atamnunulia ndege
 
Kazi ya JPM ila kwenye kuuza msivyovitolea jasho mpo vizuri
 
Bwawa la umeme litazalisha megawatt zaidi ya 2,000 ambapo ukijumlisha na zilizopo Kwa Sasa itakuwa zaidi ya megawatt 3,600.

Uwezo wa Tzn kutumia umeme sio zaidi megawatt 2,000 so ziaid tutauza Kenya.

Kabla ya kutukana shirikisha ubongo.
Huu ndio mtaji wa ccm unaoifanya iendelee kuwa madarakani.
 
Bwawa la umeme litazalisha megawatt zaidi ya 2,000 ambapo ukijumlisha na zilizopo Kwa Sasa itakuwa zaidi ya megawatt 3,600.

Uwezo wa Tzn kutumia umeme sio zaidi megawatt 2,000 so ziaid tutauza Kenya.

Kabla ya kutukana shirikisha ubongo.
Kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba tatizo la tanzania kwa sehemu kubwa na mara nyingi huwa halitokani na uchache wa umeme bali linatokana na uchakavu na ubovu wa miundo mbinu yake kwa hivyo inawezekana tu tanzania kuuza umeme kenya
 
Mradi wa umeme wa JNHPP tumeujenga kwa fedha zetu wenyewe kwa gharama isiyopungua $ 5 billion. Hata kama tulikopa ni sisi ndio tutakaoulipa huo mkopo kwa bajeti yetu na siyo Kenya.

Sasa mradi tumeukamilisha na tunategemea utakuwa full operational kuanzia mwezi June 2024. Sasa hawa AfDB wanatulazimisha kuupeleka haraka umeme huo Kenya, just because walitukopesha ujenzi wa connection line kati ya Kenya na Tanzania ya $ 309 million tu.

Watanzania wanapaswa kuufaidi mradi huu kwa kupata umeme wa uhakika wa bei nafuu isiyozidi senti moja ya dollar kama ilivyo huko Ulaya, China na USA ili viwanda vyetu viweze ku compete fairly na viwanda vingine duniani na watanzania wafurahie maisha na waweze kutumia umeme kupikia badala ya kuni na gesi.

Watanzania wenyewe ndiyo watakaoamua ni kiasi gani cha umeme wa gesi cha ziada watakachomuuzia Kenya au Uganda na kwa bei gani. Tutawauzia ule wa gesi wa bei kubwa, huu wa JNHPP utakuwa wa kwetu tu.
 
Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imezitaka Tanzania na Kenya kusaini mikataba mitatu ya Mauziano ya umeme haraka Kufuatia kukamilika Kwa mradi wa kuunganisha gridi ya Nchi hizo mbili ambao umefadhiliwa na African Development Bank.

View: https://www.instagram.com/p/C27F55go1Cz/?igsh=emo4eGo4cDQ3d3li

My Take
Kenya wangekuwa wameunganisha grid Yao na Ethiopia,shida za upungufu wa umeme tunazopta saizi zisingekuwepo.

Asante sana JPM!! Maono yako japo yalipigwa mawe lakini soon nchi inakwenda kupona!!

Kuna mbwa walisema eti umefyeka miti kitakuwa na ukame lakini leo nchi inaelemewa na mvua!!

Wakasema huo mradi utakuwa ni white elephant lakini leo hata CHAWA wa Wahuni uliowakataa wanaupigia chepuo mradi.

JPM pumzika Mzalendo wa kweli; ulisingiziwa mengi kuhusu watu kuuliwa, pumzika baba kwani hata Leo kafariki Ole Thadei, kama ungekuwepo wangesema ni wewe.

Pumzika jembe letu, tutakukumbuka kupitia utitiri wa miradi uliyoiacha!!

Ila jua tu kwamba hatuna tena miradi mipya, ila tunauza Mbuga na rasilimali zingine kwa wageni
 
Kwa nini hao AfDB wanataka tusaini mkataba haraka? Kuna nini kimejificha nyuma ya pazia?
Watupe muda tuupitie mkataba tujiridhishe kabla ya kumwaga wino. Tusije tukasaini na kujifunga kwenye opportunities nyingine zitakazojitokeza.
 
Kwa sababu nyie ndio mliwaomba pesa Sasa mnajivuta vuta Kwa sababu zipi?

Kilichojificha na matumizi mazuri ya Rasilimali muda ,pesa na zinginezo
 
Asante sana JPM!! Maono yako japo yalipigwa mawe lakini soon nchi inakwenda kupona!!

Kuna mbwa walisema eti umefyeka miti kitakuwa na ukame lakini leo nchi inaelemewa na mvua!!

Wakasema huo mradi utakuwa ni white elephant lakini leo hata CHAWA wa Wahuni uliowakataa wanaupigia chepuo mradi.

JPM pumzika Mzalendo wa kweli; ulisingiziwa mengi kuhusu watu kuuliwa, pumzika baba kwani hata Leo kafariki Ole Thadei, kama ungekuwepo wangesema ni wewe.

Pumzika jembe letu, tutakukumbuka kupitia utitiri wa miradi uliyoiacha!!

Ila jua tu kwamba hatuna tena miradi mipya, ila tunauza Mbuga na rasilimali zingine kwa wageni
Kwani hata asingemuwepo huyo JPM wako Nchi isingekuwa na umeme? Miradi ya umeme kwani ni lazima iwe bwawa la Nyerere tuu?

Kwani wewe Kwa akili Yako ndogo unadhani bwawa la Nyerere ndio Alfa na omega kwamba hakuna miradi mingine inakuja?

Mwisho Magufuli angekuwepo bwawa lisingekamilika Kwa mda Kwa sababu Hadi anakufa lilishachelewa mwaka Kwa sababu hakuwa na pesa na Kwa vile ni mtaalamu wa fix angewaambia Hilo ni bwawa kubwa sana anahitaji miaka zaidi ya 10 kulikamilisha 😆😆
 
Back
Top Bottom