Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga? Pitia juu huko wenzako wameandika vizuri. Hata kuwa ina tu inakushinda? Halafu unaeingia jukwaa hili kubishana na Wakenya?!
Ahaaa haaa haaa
Hicho ndo pekee akili yako ilichoweza kukielewa?
HATA hizo sentensi zako ulizotumia kunikashifu zina makosa ya uandishi ya aina zote. Namaanisha katika sarufi, muundo, maudhui na herufi za maneno.
Mfano, sentensi iliyoandikwa kwa wino mzito wenye rangi nyekundu inamaanisha nini? Umeleta sentensi yenye muundo mbovu ambayo haileti maana.
Neno lingine ambalo wewe umekuwa miongoni mwa wengi wanaofanya makosa ni lile ambalo limeandikwa kwa wino mzito wa rangi buluu. Kwenye KAMUSI KUU YA KISWAHILI iliyoandaliwa na Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hakuna neno kama hilo. Neno utakalo likuta ni
unayeingia na si
unaeingia.
Maneno mengine ambayo mara nyingi huandikwa kimakosa ni kama ifuatavyo.
Ndio badala ya ndiyo
Sio badala ya siyo
Nae badala ya naye
Sie badala ya siye
Ndie badala ya ndiye
Alie badala ya aliye
Mwandiko badala ya muandiko
Mwandishi badala ya muandishi
Pia neno SWALA linachanganywa sana na neno SUALA.
Swala ni mnyama pori JAMII ya mbuzi. Lakini Suala ni jambo fulani.
Vivyo hivyo kuwa na kua.
Sasa katika uandishi mko wengi sana mnaoangukia kwenye mtego wa aina hii, yaani kuandika maneno yenye makosa.
.... orodha ni ndefu. Mpaka nachelea kusema napaswa kuanzisha uzi kuhusu muktadha huu.
Lastly, I can tell you. You can sometimes out perform the index. That is not because of your skill, but it's by chance.
This is an adage borrowed from behavioural finance.