Tanzania kuna kabila linaitwa Waarusha au ni Wamasai mmeamua kujiita hivyo?

sawa kabisa mkuu ujakosea
 
Hii inaweza kuwa kweli kwa asilimia zaidi ya 90
 
Sijui ulisomea wapi? Eti wewe ndiye msimamizi,sijui hata kazi ulipataje,
Ni hasara kwa Taifa kuwa na watumishi mabumunda ya namna hii yasiyojua hata hisitoria.
 
Enhee tulia hapo hapo, hivi hawa wachagga linipokuja suala la kabila huwa wanajiandikisha kama wachagga…. au kila wao kivyao?

Yaani Mmarangu, Mmachame, Mrombo, Mkibosho etc…. kwa maana inasemekana kila wao na lugha yao!
Huwa ni wachaga ila in short Kuna makabila kama matano ni vile waliunganishwa ni Kama wamasai na waarusha tu
 
pia wanapenda kupiga vyungu
 
alikudanganya...waarusha ni mtoto wa mmasai na mchaga
Aliongea ukweli wale ni wahamiaji wa Waka adopt tabia za kimasai na hao wa Arusha na wamasai waporoni tofauti kabisa, Kwanza waarusha wakorofi na wapenda ugomvi mno tofauti na wamasai wavaa rubega
 
Nimekuwepo nasoma shule y msingi miaka ya 1970. kuna kabila linaitwa waarusha. wao wanazungumza kimasai kilaini yaa hawana rrrr nyingi katka kimadai chao. wanaishi maeneo yanayozunguka arusha mpaka oldonyosambu. wanaishi mpaka mpakani na kenya. wao huwaita wamasai watu wa porini. wanalima ndizi, kahawa, mahindi nk. Ni kama wameru tu ila pia ni wafugaji.
 
Sijui ulisomea wapi? Eti wewe ndiye msimamizi,sijui hata kazi ulipataje,
Ni hasara kwa Taifa kuwa na watumishi mabumunda ya namna hii yasiyojua hata hisitoria.
Acha ukichaa wewe hata neno historia lenyewe hujui kuandika [emoji706][emoji706]
 
Waarusha ni wamasai, ila wao wamepunguza ukali wa Mila za Kimasai.

Unaweza sema ni wamasai walioachana na Mila zao na kuchukua mambo ya mjini. Makazi Yao ni Arusha Mjini. (Manispaa ya Arusha)
 
"kabira" ndio nini?
 
Ni makabila mawili tofauti, tena mahasimu kweli kweli.

Hawapendani hata kidogo. Hata kuoana hawaoani

Makabila Mengi ya kaskazini yanafanana mambo mengi sana, kuna tofauti ndogo ndogo sana.
Acha uongo ndg
mimi ni Mwarusha
Kabila la kiarusha ni kabila dogo lililomeguka kutoka kwa wamasai sio kabisa, wala halikumevuka kiuhasama
tumetofautishwa na wamasai kwenye mambo machache sana
kwanza ni occupation, wamasai ni wafugaji 100% wakati waarusha ni wakulima na wachache wao wanafuga na kulima
Pili wamasai na waarusha tunatofautiana kwenye jando na baadhi ya mila zile za ndani sana
Tunafanana kwenye lugha, rika, koo nk
Kwa jinsi tunavyoushi ni kabila mbili ndani ya moja ndio maana watu wengine wanashindwa kutofautisha. Hakina uhasama wowote kati ya wamasai na waarusha. Infact wakati wa tohara na mambo mengi ya kimila malaiguanani wa pande zote mbili hukaa pamoja hadi wale wa Kenya na sehemu mbalim ali Tanzania kwenye mlima mmoja uko maeneo ya west Kilimanjaro nafikiri maeneo ya Hai au jirani kupitisha maamuzi ya pamoja. mfano tohara ianze lini na rika hilo liitweje. nk
Kabila hili linasadikika kutokea au kumeguka kutoka kabila mama la wamasai miaka ya mwanzoni mwa 1900 au mwishoni mwa 1800
Wamasai waliokuwa wanauza madawa na kufanua biashara ya minada walikuwa wakipita arusha na kifanya kiwa ni kituo cha kupumzikia. kwa sababu ilikuwa ni paradiso ya kweli muda ulivyosonga kidogokidogo wakaamua kusetle na kufanya makazi ya kudumu wakaanza kuzaliana na kufanya shighuli za ufugani na kilimo ndipo kabila la Waarusha au Larusa likatokea
tupo pamoja tena sana. hivyo ndg acha kupotosha mambo usiyoyajua
 
Waarusha ni kabila linaloshabihiana na wamasai Wana asili ya upareni na walikuwa vijakazi wa wamasai ila Waka adopt lugha na tanaduni za kimasai wanakaa Arusha mjini.
N. B hii story nilisimuliwa na Babu wa kimasai.
Stupid lies
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…