Tanzania kuna tabaka tawala na tabaka tawaliwa. Je, familia yako iko katika tabaka gani?

Tanzania kuna tabaka tawala na tabaka tawaliwa. Je, familia yako iko katika tabaka gani?

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Tanzania kuna matabaka 2 makuu, tabaka tawala na tabaka tawaliwa.

1. Tabaka tawala

Hili ni tabaka ambalo wengi husomesha watoto nje ya nchi licha ya wananchi wa tabaka tawaliwa kusotea msosi wa kila siku.
Imagine, watu wanasema vyuma vimekaza lakini Ukraine pekee ilipokea vijana wa Kitanzania zaidi ya 300.

Tabaka hili watoto wao wengi wanasoma Marekani.

Hili tabaka huwezi kuwakuta wakifundisha Namtumbo Secondary school.

Hili tabaka huwezi kuwakuta wakifanya kazi kituo cha police Stakishari.

Hili tabaka huwezi kuwakuta Kariakoo wameinama wanachagua t-shirts za elfu 7 .

Hili tabaka huwezi kuwakuta kwenye daladala kwa namna yoyote labda kwa sababu za kisiasa tu.

Tabaka hili kazi huchagua kwa kuzingatia taasisi, kituo cha kazi na kiwango cha mshahara.

2. Tabaka tawaliwa

Hili tabaka lina mambo mengi, tabaka hili ndilo tunawapata;

-Bodaboda

-Wajasiriamali

-Watumishi wasaidizi kama wanajeshi, police, walimu, madaktari n.k. tena wanaofikia angalau hizi level ni wenye bahati au waliotokea familia zenye unafuu.

- Tabaka hili ndilo huwa mtaji kwa tabaka tawala. Sera za elimu, kilimo, ufugaji wanatungiwa hili tabaka na mtungaji hufanya makadirio tu maana hajui uhalisia wa mateso na mahitaji ya kundi hili.

Je, uko kundi lipi?
 
Ukishakubali wewe ni mnyonge utatawalwa.
 
Nilijua nipo kwenye tabaka tawaliwa ila nimesoma hapo kuna baadhi ya vigezo sijatimiza, sijaona kigezo cha tunaoendesha maisha kwa kubeti 🐒
 
Tabaka mateka
3013964_IMG-20211126-WA0137.jpg
 
Chaajabu hata sisi tabaka la chini tukipata upenyo huwa tunafunika kombe mwanaharamu apite, tunaanza kuwadharau tuliohustle nao,
Yaani watawaliwa akishamiliki kibanda hapa mjini anajiona kamaliza Kila kitu.

Sisi watu weusi Roho zetu nyeusi pia
 
Back
Top Bottom