Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
HIi nchi tuna pesa ya kuchezea, kuna wakati vyeo vinatolewa siyo kwa sababu eneo hilo linahitaji mtu, bali kwa sababu kuna mtu fulani anatakiwa apewe uongozi, ndipo nafasi inatengenezwa.
Fikiria, ni nchi gani ina Rais mtendaji, ina Makamu wa Rais mtendaji, halafu tena ikawa na Waziri Mkuu mtendaji, halafu iwe na naibu waziri mkuu mtendaji?
Tanzania tuna Rais mtendaji, siyo ceremonial, tuna Makamu wa Rais, halafu tena tuna Waziri mkuu, halafu tena tuna naibu waziri mkuu. Ni nchi gani uliwahi kusikia ina mpangilio wa viongozi wa ngazi za juu, kundi kubwa la namna hiyo? Hayo maajabu yapo Tanzania tu!!
Tunavyoenda, usishtuke utakaposikia tuna waziri na naibu waziri, wasio na wizara maalum!! Siyo kwamba wizara isiyokuwepo inahitaji hao watu, bali kuna watu lazima wawe mawaziri hata kama hakuna wizara. Kuna watu ni lazima wawe mabalozi hata kama nchi za kuwapeleka, hazipo. Hawa wanatafutiwa uhalali wa kula pesa ya wajinga Watanzania, hata kama hawana kazi ya kufanya.
Kuna mataifa mengine, ama wana Rais Mtendaji halafu wana Makamu wa Rais, lakini hawana waziri mkuu (USA ni moja ya nchi hizo).
Baadhi ya nchi zina ceremonial president, hazina makamu wa Rais, halafu zina waziri mkuu (Malaysia ni mojawapo).
Nyingine zina mfalme, halafu waziri mkuu, hazina Rais wala Makamu wa Rais (Uingereza ni mfano mmojawapo).
Lakini sisi Taifa la viongozi watapanaji wa kodi za wananchi, ni msululu viongozi wanaopewa uongozi kama zawadi.
Serikali ya CCM ni mkoba wa kutunzia pesa uliojaa matobo ya kuvujisha pesa ya umma. Hata tuchange vipi, pesa haiwezi kukusanyika kwa sababu pakacha la kutunzia pesa lina matundu mengi.