Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Jamani jamani...Biashara ya Ndege ni ngumu sana...Hao KQ wenyewe wana survive kwa sababu wana ndege nyingi....Precision wanapumulia mashine

Hii biashara inahitaji watu wengi wenye uchumi wa kati...wanaoweza ku afford....kama economy haina hao watu...usitegemee kusafirisha watu wa nchi za wenzako...........

Je...Tanzania ina hao watu wa kuwezesha shirika letu li survive?
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!

Sawa...lakini hilo soko lipo?

Kumbuka Fastjet waliingia kwa Price Penetration strategies....Je Air TZ itatumia strategy ipi?

Pia kumbuka Hio strategy ilikuwa ina work vizuri kwa Fastjet kwa sababu Mother Company iliyopo UK inatengeneza faida hivyo kuweza kuzibeba subsidiaries kama hii ya huku

Economy ina middle income class ya kutosha ku endesha shirika letu....

Ikumbukwe hii ni kati ya Industry ngumu Duniani
 
Biashara sasa ivi ni ushindani sana na mashirika ya ndege ni mengi so inaitajika ubinifu wa hali ya juu ili tufanikiwe teka soko na faida tupate,pili menejimenti na wafanyakazi wajitume wawe na uchungu wa kuendeleza shirika wafanye kazi kwa bidii na ikiwezekana hata expert aajiriwe sio kila cku tunabaki nyuma na mashirika mengine yanasonga mbele.
 
Duh....Kweli sie ni hamnazo..
Wakati IRAN inanunua ndege 150 za Airbus zenye kubeba abira kuanzia +150 sie tunahangaika na vidaladala..

Unachosahau ni kwamba 100 billion US Dollars za Iran hii ni karibu Uchumi wote wa TZ zilikuwa frozen na Wazungu na washirika wake sasa zimeachiliwa na hivyo Iran wana fedha ya kwenda Shopping!
Usijaribu kulinganisha Iran na TZ hata siku moja kiuchumi na kial mtu anajikuna anapofikia!
 
..........LET TAKE CARE OF MIDDLEMEN.......
AFTER SALES CARES GUARANTEE
 
Another compiters is united african airline soon inakuja watapambana na fastjet na shirika la atcl ni vizuri tuwe na makampun mengi kama mabasi ya mikoani ili huduma iwe bora na zaid..visit us www.flyuaatz.com
 
Utasikia shirika limekodisha ndege kutoka South Africa/Kenya.....hili shirika ni kama tanesko tu
 
Jamani jamani...Biashara ya Ndege ni ngumu sana...Hao KQ wenyewe wana survive kwa sababu wana ndege nyingi....Precision wanapumulia mashine

Hii biashara inahitaji watu wengi wenye uchumi wa kati...wanaoweza ku afford....kama economy haina hao watu...usitegemee kusafirisha watu wa nchi za wenzako...........

Je...Tanzania ina hao watu wa kuwezesha shirika letu li survive?
Mkuu unataka kuniambia wakati huo Tanzania inamiliki Boeing watu wa uchumi wa kati walikuwepo wa kutosha ??? Kama iliwezekana wakati wa Nyerere ndio tushindwe sasa hivi
 
Mkuu unataka kuniambia wakati huo Tanzania inamiliki Boeing watu wa uchumi wa kati walikuwepo wa kutosha ??? Kama iliwezekana wakati wa Nyerere ndio tushindwe sasa hivi

Mkuu...mimi sisemi kwa ubaya...Napenda sana shirika letu li perform

Lakini uliza challenge wanazopata mashirika ya ndege siku hizi hapa Tanzania

Ni kwamba watu hakuna ...wanaowezesha wao kufanya biashara endelevu especially kwa Safari za ndani
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Fastjet ibakie ili ATC wasitoze nauli kubwa, ushindani wao ndo manufaa kwa abiria.
 
Mkuu unataka kuniambia wakati huo Tanzania inamiliki Boeing watu wa uchumi wa kati walikuwepo wa kutosha ??? Kama iliwezekana wakati wa Nyerere ndio tushindwe sasa hivi
Barabara zilikuwa mbovu kwahiyo watu ambao walikuwa na kipato kidogo waliopt kusafiri kwa ndege kwa kujibana hivyo hivyo.. Sasa hivi barabara zinapitika nchi nzima kwahiyo kama sio safari ya haraka mtu anaopt kutumia basi au usafiri binafsi
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Kuondolewa kwa fast jet sikubaliani na ushauri huu
serikali inafanya kila linalowezekana kumpunguzia mwananchi gharama
za maisha,ni ukweli usiopingika kwamba fastjet imetusaidia sana
hasa wakazi wa kanda ya ziwa na Mbeya kwa kutoza nauli ndogo,
sasa pamoja na uzalendo wa kuipenda nchi yetu,siungi mkono wema wa mshumaa.

Tumeona viwanda vya cementi vilivyotutesa kwa kuweka bei juu
na kupiga kelele cement isiletwe kutoka nje ya nchi,
sasa angalia baada ya viwanda kuongezeka hapa nchini mbona bei ya cementi imeshuka
wakati hakuna jambo lililobadilika kama tulikuwa hatuibiwi? ATCL ilete ndege lakini ipate
washindani,La sivyo hakuna haja ya kulifufua shirika hilo kama linaogopa ushindani
ambao unaleta faida kwa mlaji/mtumiaji.

Serikali ihakikishe inakusanya kodi,kama yupo mfanya biashara
anaweza akalipa kodi ya serikali,akapata faida huku bei
zake hazimuumizi mwananchi kwa nini afungiwe?
Tukubali kwenda na kaulimbiu mpya ya "hapa kazi tu" kwa kuongeza ubunifu na wala
siyo kukalia stori za ili ufanye biashara wengine wafunge za kwao.
 
Unamaanisha nchi hahihitaji wawekezaji binafsi kisa serikali inafufua ndege zake? Unahisi kwa karne hii tunahitaji kuwa na shirika moja pekee la serikali/ umma kuhudumia wananchi?

Kama hilo linapaswa kufanyika ili Shirika letu likuwe na kumea basi na iwe hivyo, Dunia nzima wanafanya hivyo!
Hivi unafahamu ni kwa nini Mashirika ya Uarabuni kama Emirates, Qatar &Co. yanashamiri? Unafikiri yanafwata kanuni za kibiashara?
Yanashamiri kwa sababu yanaendeshwa na ruzuku kubwa ktk Serikalini yaani hayajiendeshi jambo ambalo halitakiwi kulingana na taratibu za WTO na ndio maana Umoja wa Ulaya unataka kuwapiga faini hasa kwenye njia zao za Ulaya!

Amka wewe Dunia haiendi hivyo, kila mtu anatetea chake, hata Wazungu wanalinda vyao kuua washindani wageni, unafahamu ni kwanini Mkulima wa Ulaya analipwa fedha na Serikali yake?
Ni kwa sababu aweze kushindana na bidhaa za bei rahisi ktk nje, yaani maziwa kama yalipaswa yauzwe shili 1000 yanauzwa 300 halafu Serikali yao inamlipa shilingi 700 zilizobakai, sasa hii utaiita ni nini?
 
Shirka jingne lipo njiani linakuja fununu hzi kwa hivyo na wengne muwe tayari kuwapokea ni uniated african airline limited visit us on www.flyuaatz.com
 
Mkuu...mimi sisemi kwa ubaya...Napenda sana shirika letu li perform

Lakini uliza challenge wanazopata mashirika ya ndege siku hizi hapa Tanzania

Ni kwamba watu hakuna ...wanaowezesha wao kufanya biashara endelevu especially kwa Safari za ndani
Huwezi amini moja ya route ambayo Air Tanzania ilikuwa inapata pesa sana enzi hizo ni route ya Dar-Mtwara... Sasa hivi barabara ziko safi nchi nzima wapanda ndege wamepungua sana..
 
Back
Top Bottom