Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Hii hapa ni stupid suggestion. Eti fast jet iondoke kupisha walanguzi. Shame!
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
 
Biashara sasa ivi ni ushindani sana na mashirika ya ndege ni mengi so inaitajika ubinifu wa hali ya juu ili tufanikiwe teka soko na faida tupate,pili menejimenti na wafanyakazi wajitume wawe na uchungu wa kuendeleza shirika wafanye kazi kwa bidii na ikiwezekana hata expert aajiriwe sio kila cku tunabaki nyuma na mashirika mengine yanasonga mbele.

nasikitika sana maana uwekezaji wowote ni hesabu. hesabu za calculator zikionesha faida ipo basi mtu au mwekezaji hujitosa na kuwekeza. huku akifanya kwa makini investment cost kudhibitiwa na Return of investment(ROI) hapo ROI yaweza rudi hata baada ya miaka 20. kuna factor iliyo nje ya sheria hizi za uwekezaji hapa TZ. hasa kwa mashirika ya umma.
1) ukweli mchungu ni kuwa hatuna rasilimali watu katika sector ya bulk investment.
2) Siasa
3) sheria za kuendesha mashirika haya

mwisho.... hatukuwa na haja wala uharaka wa shirika la ndege. kuna mambo machache yangetazamwa kwanza.
kwa mfano kati ya Reli na ndege ipi inaleta tija hara kwa uchumi wetu ukitizama nafasi yetu kijiografia.
nini kinaua mashirika ya umma je sababu zilizoua shirika la ndege leo bado ni tishio? kama zipo tuzisishughulikie kwanza.
na kama hazipo tukinunua ndege kwa mkopo tutaweza ushindani au itakuwa km MABASI YAENDAYO KASI. au ni ile ishu ya ndege ya abiria 100 kuruka na watu 5 kama abiria.

kwa kifupi shirika hili halitaweza kujiendesha hivo halina tija. napendekeza serikali ingenunua hisa Precision na kuwa mbia.
 
Back
Top Bottom