Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

K.m. Ethiopia ni nchi masikini kuliko yetu lakini shirika lao linaongoza kwa kupata faida Afrika..
Chifu, pamoja na kukubaliana nawe katika uliyoyaongea, lakini ili la kusema Ethiopia ni nchi maskini kuliko Tanzania haupo sawa.
Check latest GDP ranking za World Bank (December 29 2015) http://databank.worldbank.org/data/download/GDP.pdf
Ethiopia wapo nafasi ya 79 kati ya chumi 214 wakiwa na GDP ya USD 55.61 billions. Tanzania ipo nafasi ya 88 kati ya chumi 214 ikiwa na GDP ya USD 48.06 billions.
Check hapa takwimu nyingine za kiuchumi na kimaendeleo za Ethiopia: Ethiopia | Data
Halafu angalia na za Tanzania: Tanzania | Data

Licha ya kutokuwa muumini wa GDP kama kipimo cha maendeleo, lakini ndicho kinachotumiwa kwa bahati mbaya.
 
Habari kutoka chanzo kisicho rasmi sana.. inasemekana ATCL inategemea kuleta ndege 5 (regional jets) aina ya Bombadier zenye uwezo wa kubeba abiria 50 hadi 70 ili kufufua biashara yake hasa kwa safari za ndani na nchi za jirani.

Fedha hiyo inasemekana ni mkopo toka TIB..
Boeing au
Airbus ndio mpango mzima hizi zingine sio nzuri
 
hv lakini ni lazima tuwe na atc?? mbona tuna ushamba sana. serikali inataka kufanya kila kitu? ushaona wapi?
 
Roho mbaya haijengi, sina hakika na uwezo wako wa kufikiri, maake pointing zako nyingi ni fitna kama za wake wenza

Bora roho mbaya inayoakisi Uzalendo; zama za mipasho, ngonjera na kejeli ziliisha Novemba 5; 2015 na kuzikwa msoga!
 
Watanzania ni watu wepesi sana kusahau na rahisi sana kudanganyika

Miaka 3 iliyopita ATC walikodi ndege, tukaona viongozi wakiwa na mashada ya maua eti wanapokea ndege ya kukodi. Hatujui imeishia wapi

Jk alisema Oman inachukua shirika kwa ubia. Hatujui mpango huo umeishia wapi

Leo tunasikia ndege 5, akina baba na njuga miguuni ,wamama na vibwebwe, mabinti vigele gele na hoi hoi
Hata hawajaziona na wala hawajui mpango ukoje, vijana wameshupaa kama vile wametangaziwa ujio wa ngoma za vigodoro

Inasikitisha, hata samaki hawana usahaulifu wa namna hii.

Hatuhitaji ndege, tunahitaji mtu wa kutusaidia kujitambua
 
Huyu jamaa umemjibu vizuri, inaonesha hajajua madhara ya tanesco kukosa mshindani, (monopoly) kwa karne hii ni bora mchawi.
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!



Nikweli kabisa usemacho mashirika mengi ya ndege yameimarika kwa kutete a maslahi ya ndege ndani niaibu sana kwa shirika la kigeni kufanya safari kama shirika la nchi ikumbukwe kwamba hawa fastjet walikwenda kenya kutaka kufanya wanachokifanya kwetu walikataa kwakulinda shirika la Kenya airways hata ndugu zetu wanatushinda kwa kuwa smart tumekalia majungu na kujenga hoja sizizo na msingi Airtanzania haiwezikuendelea kwakuruhushi hawa fastjet panya kutoka nje na kusujudu wawekezaji kuliko uzalendo.
 
Hata ziletwe 100, mradi ni shirika la umma la Kitanzania na linaendeshwa na Watanzania litakufa tu.

Watanzania, ni wezi, wavivu, waongo, wazembe. Kuanzia msafishaji hiyo ndege atataka kuiba mpaka marubani mpaka Mkurugenzi.

Tanzania bila kuwekwa sheria ya kifo kwa wezi wa mali ya umma hatutaweza kuendesha kitu chenye tija.
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Sasa ufinyu wa mawazo unawapelekeafa lumumba kuwa wavivu wa kufikiri na mmebobea kwenye utaalamu na uzandiki wa uporaji
 
... UncleBen, kwa kuanzia hii shirika lazima liendeshwe kwa ruzuru -au namna yeyote itakavyotaka kuitwa hiyo financing ya shughuli zake- ili liweze kusimama lenyewe baadae, likifanikiwa.

... Hamna kinachoshindikana. Ila, sekta ya utalii ni muhimu sana kwa ukuaji wa shirika hili. Maana yake ni uboreshaji wa vivutio vya utalii, huduma za hoteli (skills, services, and assets), n.k..
Ruzuku ndiyo imeifikisha hapo lilipo maana halifanyi kazi kwa ufanisi kwa sababu litapata ruzuku. Ukiangalia kwa umakini mashirika yote yanayoendeshwa kwa kutegemea ruzuku ya serikali yanakosa ufanisi katika uendeshaji ndo maana yanaendeshwa kwa hasara na hayawezi kujiendesha yenyewe bila kuyegemea ruzuku.

Ukisema kuwa shirika linashindwa kuimarika kwa sababu hatujaboresha miundombinu ya utalii itakuwa umekosea, kwa mfano Rwanda wanakitu gani walichotuzidi katika utalii mbona shirika lao linazi kuimarika??
 

Kama hilo linapaswa kufanyika ili Shirika letu likuwe na kumea basi na iwe hivyo, Dunia nzima wanafanya hivyo!
Hivi unafahamu ni kwa nini Mashirika ya Uarabuni kama Emirates, Qatar &Co. yanashamiri? Unafikiri yanafwata kanuni za kibiashara?
Yanashamiri kwa sababu yanaendeshwa na ruzuku kubwa ktk Serikalini yaani hayajiendeshi jambo ambalo halitakiwi kulingana na taratibu za WTO na ndio maana Umoja wa Ulaya unataka kuwapiga faini hasa kwenye njia zao za Ulaya!

Amka wewe Dunia haiendi hivyo, kila mtu anatetea chake, hata Wazungu wanalinda vyao kuua washindani wageni, unafahamu ni kwanini Mkulima wa Ulaya analipwa fedha na Serikali yake?
Ni kwa sababu aweze kushindana na bidhaa za bei rahisi ktk nje, yaani maziwa kama yalipaswa yauzwe shili 1000 yanauzwa 300 halafu Serikali yao inamlipa shilingi 700 zilizobakai, sasa hii utaiita ni nini?

Kweli kabisa watanzania tumejipatia ulemavu wa fikra kwa kuona kwamba kila kitu sahihi lazima tufanyiwe na mwekezaji huku tukiwatukuza wakati uchumi wetu ukizidi kuporomoka kutetea maslahi yashirika letu la ndege ni muhimu sana . Ukweli nikwamba tumapenda shortcuts hatutaki kufikirisha bongo zetu. Ndio maana hatuna tunachojivunia zaidia yakusifia vya wenzetu
 
Management itabadilika ?

Waangalie tatizo la kufika hapo kabla ya kukabidhi ndege mpya....
 
Chifu, pamoja na kukubaliana nawe katika uliyoyaongea, lakini ili la kusema Ethiopia ni nchi maskini kuliko Tanzania haupo sawa.
Check latest GDP ranking za World Bank (December 29 2015) http://databank.worldbank.org/data/download/GDP.pdf
Ethiopia wapo nafasi ya 79 kati ya chumi 214 wakiwa na GDP ya USD 55.61 billions. Tanzania ipo nafasi ya 88 kati ya chumi 214 ikiwa na GDP ya USD 48.06 billions...

Mkuu uko sawa kabisa. Ila ukiangalia kwa upana, kama mwelekeo wa miaka 10 iliyopita, ndipo utakapoona Ethiopia ikiipita Tanzania katika uwekezaji na uzalishaji na hivyo kutuzidi kwa GDP. Wametupita kutokana zaidi na utawala mbovu ambao tumekuwa nao kwa miaka mingi licha ya kuwa na "potential" kubwa zaidi.

Ethiopia ina rasilimali chache kuliko Tz lakini ina uendeshaji makini sana wa uchumi. Habari ya rushwa na ufisadi ni kama haipo na kila senti inayopatikana inaelekezwa kwenye shughuli maendeleo. Upotevu wa mapato ni mdogo sana. Katika kipindi cha karibia miaka 10, Ethiopia imefanya uwekezaji na ujenzi mkubwa wa miundombinu kwa kasi ambayo imekuza GDP yao na kutupita haraka katika kipindi hicho.
 
Kwa sasa tutaweza kufanikiwa iyo biashara ya usafirishaji maana ukiwa na utawala mbovu kila kitu kinaenda ovyo watu sio makini ni kuiba na kutegemea wakitoa Ripoti tuu watapewa Ruzuku..Ruzuku futa kabisa ajili watu wachache wenye uzalendo ku run biashara ya Ndege ni Rahisi kufanikiwa kama utafata kanuni zake na si vinginevyo na tusitegemee faida inapoanza mwaka wa kwanza ni kutengeneza jina kwanza na tungeanza na ndege za ndani ili twende kupambana soko la nje kuriko kukimbilia nje wakati hela zipo hapa kwanza..
 
Barabara zilikuwa mbovu kwahiyo watu ambao walikuwa na kipato kidogo waliopt kusafiri kwa ndege kwa kujibana hivyo hivyo.. Sasa hivi barabara zinapitika nchi nzima kwahiyo kama sio safari ya haraka mtu anaopt kutumia basi au usafiri binafsi
Nilikuwa sijui kumbe kule Kenya, Ethiopia ,,,afrika kusini,,ulaya hata america kuwa barabara zao ni mbovu ndo maana mashirika yao ya ndege yanafanya vizuri,,nashukuru mkuu kwa kunijuza
 
Ruzuku ndiyo imeifikisha hapo lilipo maana halifanyi kazi kwa ufanisi kwa sababu litapata ruzuku. Ukiangalia kwa umakini mashirika yote yanayoendeshwa kwa kutegemea ruzuku ya serikali yanakosa ufanisi katika uendeshaji ndo maana yanaendeshwa kwa hasara na hayawezi kujiendesha yenyewe bila kuyegemea ruzuku.
...Ruzuku hutolewa kwa kipindi fulani na lengo maalum. A means to an end. That "end" being shirika kujiendesha lenyewe baadaye.

...Emirates na Qatar wanapata ruzuku kwa namna tofauti tofauti, kama kupewa viwanja bure na kuuziwa mafuta yenye ruzuku (bei ndogo kuliko ya soko) kuboresha huduma zao na kuhimili ushindani.

Ukisema kuwa shirika linashindwa kuimarika kwa sababu hatujaboresha miundombinu ya utalii itakuwa umekosea, kwa mfano Rwanda wanakitu gani walichotuzidi katika utalii mbona shirika lao linazi kuimarika??

...Sijasema! Ungeeleza kama tafsiri yako binafsi. Tatizo la ATCL si rocket science, watu wanajua.

...Rwanda hawana wanachotuzidi kwa ujumla kwenye utalii. Sekta hiyo kwao inazidi kukua kila mwaka na kuzidi kuongeza mapato. Ni mipango makini kwamba Shirika la ndege hukuzwa na hunufaika na utalii. Tuna nafasi kubwa ya kukuza utalii, na tutafaidi zaidi kwa kuwa na carriers wetu wenyewe.
 
Tabutupu naona kwanza
Habari kutoka chanzo kisicho rasmi sana.. inasemekana ATCL inategemea kuleta ndege 5 (regional jets) aina ya Bombadier zenye uwezo wa kubeba abiria 50 hadi 70 ili kufufua biashara yake hasa kwa safari za ndani na nchi za jirani.

Fedha hiyo inasemekana ni mkopo toka TIB..
Tabutupu mi naona kwanza Mheshimiwa aende akawatumbue kwa kufilisi Shirika la ndege la Tanzania maana majipu yao yameota midomo miwili na kila siku yanapakwa mafuta yanameremeta ile mbaya,vinginevyo hizo ndege zitahujumiwa tena
 
Nilikuwa sijui kumbe kule Kenya, Ethiopia ,,,afrika kusini,,ulaya hata america kuwa barabara zao ni mbovu ndo maana mashirika yao ya ndege yanafanya vizuri,,nashukuru mkuu kwa kunijuza
Hivi sisi hatuna shirika la ndege lenye uwezo kwasababu eti tuna Barbara nzuri kuliko mataifa kama Kenya,Marekani na nchi za ulaya? Mimi sijaona barabara yenye uwezo wa kukidhi sekta ya usafirishaji Tz. hatuna barabara bali tunajifariji tuu.

Wenzetu wamewekeza katika sekta ya usafirishaji wa majini, ardhini na angani na zote zinafanya kazi. sisi tunatumia barabara tuu tena hazina ubora unaofaa. wenzetu wana highway zenye ubora wa hali ya juu.

sekta ya usafirishaji inamchango mkubwa katika uchumi. sisi tunatumia barabara tuu ambayo ni gharama sana kuliko reli au usafiri wa majini
 
Back
Top Bottom