Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

Tetesi: Tanzania kununua Ndege mpya 5(regional jets) aina ya Bombadier

S
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
siungi mkono hoja yako kwa kuwa tunahitaji ushindani Ili kufanya vizuri mambo ya monopoly Kama Tanesco no. Kama kweli wananunua ndege Ni habari njema Sana wapambane na walioko sokoni.
 
Serikali Ilikataa......If I correctly remember this
Sasa kwanini hiyo ya kuwa bail out PW haikua benchmark ya wao kufanya biashara ya ndege kama tatizo ni kutengeneza mazingira mazuri kwanza nyumbani ndio waweze kwenda kimataifa ?? Si wangekaa na Shirima na wenzake na kumwambia kwa sababu wewe umeshatengeneza jina ,tunalipa hiyo hela then tunafanya kuchukua hisa kadhaa ,na sisi tutatoa mathalani Boeing 2 kwa kuanzia ,kidogo kidogo tungesogea tu
 
Mkuu unataka kuniambia wakati huo Tanzania inamiliki Boeing watu wa uchumi wa kati walikuwepo wa kutosha ??? Kama iliwezekana wakati wa Nyerere ndio tushindwe sasa hivi
...Wakati wa JKN mashirika mengi yaliendeshwa kwa ruzuku. Lengo likiwa ni kutoa huduma. Kama nilimsikia vizuri msajili wa hazina, mashirika yanatakiwa kujiendesha kwa faida. Hapa ndio ilipo changamoto anayoongelea Freeland.

...Actually, baada ya mageuzi ya uchumi, mashirika mengi yalidorora kutokana na ruzuku kukatwa na mengine ilibidi kubinafsishwa, sera ikitaka hivyo.

...Fedha ya ruzuku kwa viwanda na mashirika enzi zile ilitoka kwenye sekta ya kilimo. Mauzo ya bidhaa za kilimo nje yaliwezesha kujenga viwanda na kutia ruzuku kwenye mashirika.
 
Kama tatizo ni barabara mkuu nadhani Heathrow ,au LAX zingekua zimeshafungwa siku nyingi mkuu ,nadhani kwa usafiri wa usalama zaidi ni ndege kuliko vitu vyombo vingine vyote
Sasa hapo tunarudi palepale kwenye kipato cha wananchi wako
 
Alafu kuna uzi fulani humu nyumbu wamechachamaa wakati Membe alishindwa kurudisha mjusi kutoka Ujerumani! viva Magufuli #HapaKaziTu
Haha hili la mjusi umenikumbusha mbali hivi bado yupo Ujerumani au ??
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Unaomuogopa adui yako inamaana wewe ni dhaifu, kinachotakiwa ni kuboresha huduma na kuweka bei shindani, nilitegemea ndege tano mbili kati ya hizo ziwe zinabeba abiria 100+ za kutoka nje ya nchi, sasa 50-70 tayari ni failure..
 
Aisee TIB ndo wanasimamia show eeeh!
Safi sana kama hii mipango itakua kweli
 
...Wakati wa JKN mashirika mengi yaliendeshwa kwa ruzuku. Lengo likiwa ni kutoa huduma. Kama nilimsikia vizuri msajili wa hazina, mashirika yanatakiwa kujiendesha kwa faida. Hapa ndio ilipo changamoto anayoongelea Freeland.

...Actually, baada ya mageuzi ya uchumi, mashirika mengi yalidorora kutokana na ruzuku kukatwa na mengine ilibidi kubinafsishwa, sera ikitaka hivyo.

...Fedha ya ruzuku kwa viwanda na mashirika enzi zile ilitoka kwenye sekta ya kilimo. Mauzo ya bidhaa za kilimo nje yaliwezesha kujenga viwanda na kutia ruzuku kwenye mashirika.
Sasa mkuu kama pesa ya mauzo ya bidhaa za kilimo peke yake tena kilimo cha jembe la mkono iliweza kutoa ruzuku kwa mashirika ya umma ,hivi sio zaidi kwa sasa hivi ambazo tuna rasimali chungu nzima achilia mbali na gesi na mafuta na pia tuna wataalamu wengi wazawa pengine kuliko wakati wowote ule katika historia ya nchi yetu ?? Hilo la sera ya mashirika kujiendesha kwa faida sioni ni tatizo ,kwani KQ au ET zinajiendesha vipi ???
 
Habari kutoka chanzo kisicho rasmi sana.. inasemekana ATCL inategemea kuleta ndege 5 (regional jets) aina ya Bombadier zenye uwezo wa kubeba abiria 50 hadi 70 ili kufufua biashara yake hasa kwa safari za ndani na nchi za jirani.
Fedha hiyo inasemekana ni mkopo toka TIB..
Hii ni habari nzuri. Lakini haya mashirika yalazimishwe kuweka mahesabu yao wazi kila mwaka kwenye mitandao yao.

Kama boss akivurunda aondoke, sio shirika linaendeshwa na mediocre boss miaka nenda rudi.
 
Mkuu kwa maana hiyo kipato cha wananchi miaka yote inakua constant sio ???
Dhana ya serikali hii ni kubana pesa na kuirudisha serikalini.. Hukumsikia hata Magufuli mwenyewe alivyowaambia wanajeshi juzi juu ya kuwapa tender za ujenzi?? Tusishangae tukarudi kwenye old tendering system tuwe na duka moja tu la serikali... Kwa mtindo huo pesa itabaki serikalini na kiasi kidogo tu cha mishahara ndio kinaingia kwenye system..
 
Jamani jamani...Biashara ya Ndege ni ngumu sana...Hao KQ wenyewe wana survive kwa sababu wana ndege nyingi....Precision wanapumulia mashine

Hii biashara inahitaji watu wengi wenye uchumi wa kati...wanaoweza ku afford....kama economy haina hao watu...usitegemee kusafirisha watu wa nchi za wenzako...........

Je...Tanzania ina hao watu wa kuwezesha shirika letu li survive?
Kwa local flights naona kama Tz iko vizuri tu,tunaweza angalia number of flights mfano, Fastjest wana Flight 3 kwa siku Dar-Mza/Dar, Precisionnao 3 na ATC wanazo 2. Hiyo ni root moja tu,bado kuna KNJARO/MZA,Dar/KNJARO, Dar/Mtwara,Dar/TBR,Dar/Msm/Mza kuna root za kutosha ila kuna uhaba wa ndege.
Waje tu kishindani na wapambane na kina Fastjet.
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Nina kubaliana na wewe kuweka uzalendo mbele lakini sio hujuma.

Ukiangalia mashika karibia yote ya serikali yaliokufa siku za karibuni ni kutokana na hujuma. Tukianza mambo ya hujuma tutakao hadhirika ni sisi wenyewe. Mtanzania anaweza kupewa milioni 5 akasababisha hasara ya mabilioni. Haya mashirika ya nje yana wataalamu wao ambao wameweka uzalendo mbele.
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Hapana fast jet iendelee ili kaweka ushindani. Ndo maana ya soko hulia
 
Mhh...wakuu hizi sio zile DC 10?? Hizi DC 10 ni rejects, pilots wanaziogopa sana mpaka wanaziita "Death Chamber number 10"...kwa wanaofutilia Aircrash investigations watakuwa wanafahamu hilo
 
Kama ni kweli safi sana lkn kwanza FastJet ni lazima wasepe, iwe kwa hujuma ya moja kwa moja au ya chini chini lkn ni lazima waondoke kwetu ili Ndege yetu iweze kumea na kukua, yaani soko la ndani kwa asilimia zaidi 90% liwe la ndege yetu!
Woga wa nini sasa hao jamaa sinawalipa KODI?
 
Back
Top Bottom