Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kusaini mikataba ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini ili Mikoa hiyo ipate umeme wa uhakika na iondokane na adha ya umeme kukatikakatika.
Rais Samia amesema hayo baada ya kufungua mradi wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwenye hafla iliyofanyika Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo March 09, 2025.
Soma: Rais Samia: Tanzania inayo nafasi ya kuuza umeme nje
Rais Samia amesema "Umeme unakatikatika maeneo ya Kaskazini huku lakini Serikali yenu inachukua hatua ya kununua umeme nje maalum kwa Mikoa hii ya Kaskazini ili umeme upatikane masaa 24 muda wote bila kukatikakatika"
"Tuko kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba ili tuweze kununua umeme ule uungwe Kanda ya Kaskazini na Wananchi wafaidi na umeme, kwahiyo tutakuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika kila pahali, Vijiji vyote vina umeme tunakwenda Vitongojo na umeme wa kutosha tunaununua unaingia ili kazi za maendeleo ziendelee"