Tanzania kupokea mkopo wa dollar million 150

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Kuna habari nimeiona mtandaoni,nimeona niilete jukwaani.

Shirika la fedha la IMF ,litaikabidhi Tanzania mkopo wa dollar millioni 150 ili kuweza kukabiliana na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dollar...
Kuanzia tarehe 17 May 2024,mkopo utakuwa tayari ushaanza kupokelewa.


Lucas Mwashambwa
ChoiceVariable
GENTAMYCINE

source:the citizen
 
Unaweza labda kuniambia sababu Kubwa ya Mimi kunitaja hapa ni nini / ipi hasa?
 
Nchi mufilisi , hiyo mikopo inaishia kumrejesha matumbo ya wapumbavu wachache
 
Safi Sana, vizazi vijavyo vitalipa tu, mbona mwaka 2020, ndiyo tulimaliza kulipa mkopo wa barabara ya uhuru, toka toka clock tower mpaka Buguruni?, na barabara hiyo ilijengwa, 1970s.....
#Tuchukuwe mikopo bila hofu yoyote!
 
Ukisoma hizi takwimu hapa za imports huwezi shangaa,

punguzeni kuzaana hovyo,ongezeni uzalishaji(long term process) na anzeni kuwaamini wakandarasi wenu wa ndani ikiwemo kuwawezesha Ili pesa nyingi mnazowalipa Wachina Kwa Dola msevu Kwa kuwalipa wazawa Kwa Shilingi vinginevyo shida itaendelea licha ya uchumi kuimarika ila hauendeani na Kasi ya ongezeko la watu na uzalishaji.
 
Kama kawaida tunaendelea kuongeza umasikini Kwa vitukuu vyetu kwa kukopakopa hovyo hovyo na hizo hela zinaishia Kwa wahuni na mwisho wasiku matatizo yanabaki pale pale.
 
Kama kawaida tunaendelea kuongeza umasikini Kwa vitukuu vyetu kwa kukopakopa hovyo hovyo na hizo hela zinaishia Kwa wahuni na mwisho wasiku matatizo yanabaki pale pale.
Umewahi fuatwa kwako kudaiwa hela ya Mkopo?
 
Reactions: Tui
So Waziri Muigulu ndiyo kaona hiyo ndiyo solution...
 
Kwanini nini Tsh inashuka thamani na dola imeadimika? YAANI TUMESHINDWA KULIFANYIA KAZI HILI SWALI NA TUMEONA SULUHU NI KUKOPA?

LOW PRODUCTION ambayo mwisho wa siku inaleta low exportation, matokeo yake tumebaki kuwa Taifa la wachuuzi, wadangaji, na consumers.
Unahitaji watu serious na utawala wa mkono wa chuma kuwaweka watu kwenye mstari na kutoka kuwa wachuuzi na kuwa wazarishaji.

Wengi humu tunapiga zumari na kusifia ujinga ujinga na kusahau in long term huu ujinga unakwenda kutafuta vizazi na vizazi.

WAKOPESHAJI WANAJUA WANACHOKIFANYA ILIHALI WAKOPESHWAJI NI HOHEHAHE HAKUNA WAJUALO.

TUACHE HUU UCCM NA UCHADEMA, TUACHE HUU UKRISTO NA UISLAMU TUSIMAME PAMOJA KUKEMEA UJINGA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU NA VIZAZI KUMI MBELE.
 
Unadhani ni Suala la overnight? Waziri amewahi weka wazi kwamba Nchi inatekeleza miradi Mingi mikubwa ambayo Ilianza Kwa pamoja ,hili nalo ni chanzo.

The root is kule Kwa Mzee wa kukurupuka apate sifa,kaacha msala yeye kajifua lawama Kwa wengine 😁😁
 
Umewahi fuatwa kwako kudaiwa hela ya Mkopo?
Dah aisee, inasikitisha Sana.

Unafikiri kuna Mtanzania atafuatwa nyumbani kudaiwa mkopo wa Serikali? Bali utapandishiwa gharama za maisha wewe na vitukuu vyako kufidia madeni ya wakoloni ilihali mkopo wenyewe ulitumika kuendeshea uchaguzi, kununulia magari ya kifahari viongozi, kujenga Barabara zisizo na viwango, nyingine kuibiwa na kurudishwa hukohuko zilikokopwa, watu kuziiba kulewea na kuhonga malaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…