deonova
JF-Expert Member
- Apr 22, 2013
- 742
- 419
safi safi mtoa uzi sasa tujiulize kwanza humu ndani ya JF wangapi wetu tuna mikataba na wasaidizi wetu kwenye majumba yetu(domestics helpers) je tunawatendea haki ya kuwapa mishahara inayositahili?tunawapa likizo zao?muda wao wa kazi kwa siku upo kisheria?nini marupurupu yao kama chakula ,malazi je vipo above board?tukumbuke wote tumetoka kwa Mungu na tutarudi kwake kumnyanyasa binadamu wenzako kisa hakuwa blessed the way we are ni mbaya mno.
Haa haaa asante kwa kuibua changamoto ambayo hata sisi inatusumbua ktk kazi zetu, ni bahati mbaya kuwa kwa Tanzania bado hatujawa na muongozo mahsusi wa kukagua hii domestic sekta kutokana na changamoto ya hiyo sekta mathalani unaweza kwenda mwenye nyumba asifungue geti, na hata ukienda lazima ushirikishe uongozi wa mtaa usije zuliwa jambo kwamba umeenda kumhoji beki 3 bila boss wake kuwepo ukaambiwa umechukua vitu ama umemfanya jambo...so ni sekta nyeti kidogo. Lakini hii haizuii wao kuwa binded na Sheria za kazi kama kupewa mkataba wa Ajira na stahiki zote
Kwa faida ya wengi, hawa domestic workers nao wana kima chao cha chini cha mishahara kama ifuatavyo;
- Tsh. 80,0000/= kwa mwezi kwa mfanyakazi ambaye halali kwa mwajiri wake, yaani yule ambaye anakuja kukufanyia kazi halafu jioni anarudi kwake/kwao
- Tsh. 40,000/= kwa mwezi kwa mfanyakazi ambaye analala kwa mwajiri. Hili kundi ndio lipo kubwa, na iko ndogo kuliko anayerudi kulala kwao kwa sababu tunaamini huyu anayelala kwa mwajiri wake ina maana gharama za chakula, malazi, mavazi na matibabu ni juu ya mwajiri wake na ni nje ya mshahara wake huu.
Hivi vima vya chini vya mishahara ya kila sekta ni kwa Mujibu wa Tamko la Serikali Namba 196 la mwaka 2013