Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Mm nimwajiliwa kampun( xx) inayotoa huduma ya chakula katk mgodi wa madin hapa nchin,mwajir kasitisha ajira kwakutangaza and then akaitaj wafanyakaz twende medical ku re-check up bt wafanyakaz tumeshindwa kukubaliana nae coz anadai twende medical and then turud kazin kufanya kaz?,je hii ni sahihi na vp tunaenda medical kabula hatujapewa termination letter???
(Kabula) ndo nini?...ndo maana mmefukuzwa kazi
 
Una mkataba wa aina gani, muda au wa kudumu? Kama ni wa muda utakuwa umeisha na ndiyo sababu kaamua alichofanya.
 
Kupima afya ni sheria ya nchi. Especially nyie mnsofanya kazi kwenye vyakula.
Na wewe utakuwa umeajiriwa na kampuni ya mbunge wa kibaha?
Yule jamaa anapiga sana pesa
 
Mm nimwajiliwa kampun( xx) inayotoa huduma ya chakula katk mgodi wa madin hapa nchin,mwajir kasitisha ajira kwakutangaza and then akaitaj wafanyakaz twende medical ku re-check up bt wafanyakaz tumeshindwa kukubaliana nae coz anadai twende medical and then turud kazin kufanya kaz?,je hii ni sahihi na vp tunaenda medical kabula hatujapewa termination letter???
kabula= kabla

halafu unamaanisha nini kusema umesitishiwa ajira halafu unaambiwa ukapime urudi kazini? itakuwa hamtaki kupumwa nyie kapimeni afya ni jamboo la kisheria na ni kwa manufaa yenu mkoje?
 
Tanzania sheria zote za mikataba iwe ya mdomo au ya maandishi huongozwa na Employment and Labour Relation Act of 2004.
Kama mfanyakazi hakuachishwa kazi kwa sababu ya misconducts, basi kuna kuachishwa kazi ya aina mbili

1. Redunducy wafanyakazi wanatakiwa kwanza watangaziwe nia na sababu za redunducy, pili kuwepo na majadiliano kati ya mwajiri na mfanyakazi anayefanyiwa redundacy akisindikizwa na mwanasheria wake au mwakilishi wa vyama vya wafanyakazi. Makibaloano ya mazungumzo yatakita kwenye fidia ya mkataba uliosalia, compesation za likizo ambazo hazikuchukuliwa, barua ya utumishi na mafao mengine yaliyotajwa kwenye mkataba.

2. Mfanyakazi pia anaweza achishwa kazi kama mkataba wake umefika mwisha. Mwajiri anatakiwa kutoa notice angalau ya siku 30 kabla ya mkataba kuisha. Hapa mafao ni malipo ya likzo ambazo hazikuchukuliwa, barua ya utumishi basi.

Kama mwajiri alikuwa halipi pension basi atatakiwa kulipa gratuity ya 25% ya mshahara wa mwisho mara miezi ambayo mtumishi alitumika. Pia mwajiri anatakiwa kutoa mchanganuo wa malipo yote ya pension na kama kuna miezi ambayo haikupelekwa kwenye taasisi husika mwajiri anatakiwa kupeleka pesa hizo sio chni ya 10% ya mshahara
 
Mm nimwajiliwa kampun( xx) inayotoa huduma ya chakula katk mgodi wa madin hapa nchin,mwajir kasitisha ajira kwakutangaza and then akaitaj wafanyakaz twende medical ku re-check up bt wafanyakaz tumeshindwa kukubaliana nae coz anadai twende medical and then turud kazin kufanya kaz?,je hii ni sahihi na vp tunaenda medical kabula hatujapewa termination letter???
Medical check up haina umuhimu wowote ukiachishwa kazi, labda km anataka kuwaajiri tena kwa conditions nyingine
 
Katika hali iliozoeleka Tanzania watu wengi hukimbilia kazi au ajira kabla ya kujifunza na kujua sheria za kazi nchini na kimataifa ILO. Watu wengi hukimbilia pia kusaini mikataba ya ajira bila kujua mkataba unasema nini kati ya muajiriwa na muajiri.

Hali hii imepelekea watu wengi sana kupoteza ajira kwa kushindwa kumudu kasi ya ajira yake na shughuli anapaswa kufanya kila siku na kuingia na kutoka

Wengine hushindwa kusema chochote wawapo kazini kwa kuogopa kufukuzwa kazi na muajiri wake.

Jambo hili hupelekea watu hao kufanya kazi chini ya kiwango cha kazi kwa kuogopa ajira zao kuwa hatarini.

Wafanyakazi wengi husoma sheria za kazi baada ya kufukuzwa na kutaka kujua sheria inasema nini baada ya kufukuzwa au kuacha kazi.

Katika hali hii kumekuwa na uzembe wa kuwajibika kwa kutojitambua na msimamo wa ajira zao.
 
Attachments

Wadau mimi ni mwajiri, kuna mstaafu anataka mafao ya kustaafu. Nimeuliza naambiwa sheria hiyo imerekebishwa 2010, na sasa hakuna fao hilo. Nimesoma sheria ajira 2004 sioni mabadiliko.

Naomba msaada wenu, ni kweli fao hilo halipo tena? Je naweza kupata nakala marekebisho 2010 ktk soft copy?
 
Hayo marekebisho yanasema kiinua mgongo hakitatolewa kwa mwajiriwa ambaye mkataba wake wa ajira umefikia ukomo ama amestaafu

Nanukuu....

The principle Act is ammended in section 42 by adding immediately after paragraph (b) of subsection (3) the following new paragraph:

"(C) to an employee who attains the age of retirement or an employee whose contract of service has expired or ended by reason of time."

Kwa hiyo ukisoma kile kifungu cha 42-(3) cha sheria mama ya mwaka 2004, baada ya kipengele (b) ongezea hapo hiki kipengele (c) kipya mkuu. So kama amestaafu hastahili mafao ya kiinua mgongo labda tu kama mlikubaliana kulipana mafao ya kiinua mgongo kwa mfumo wa gratuity...so hapa inategemeana na makubaliano yenu kwenye mikataba yenu
 
Back
Top Bottom