Huruma sana, mfanyakazi wa taasisi binafsi kafukuzwa kazi bila kulipwa kiinua mgongo, amefanya kazi miaka 22. Kosa eti kwa nini hajamripoti meneja wake kwenye kamati ya maadili kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyakazi wa chini yake. Jamaa anasema binti ndio aliyemwambia kuwa anatoka na boss wake. Inaonekana ni kama binti hakupewa kitu alichokubaliana na meneja, ndio akaamua kuripoti kwenye kamati ya maadili ya kampuni. Huko kwenye kamati wakati akieleza akamtaja yule mfanyakazi aliyemjurisha kwamba anatoka na boss wake. Huyu mfanyakazi aliyefukuzwa kazi ni msaidizi wa meneja aliyekuwa akitoka na huyo binti. Sasa kamati ya maadili ikawafukuza wote wawili yaani meneja na msaidizi wake. Sasa jamaa anaumia na ameamua kufungua shauri CMA kulalamika kwa nini afukuzwe kwa kosa alilolifanya meneja wake. Yeye sio mmoja wa watu waliopewa kazi ya kupokea kesi za kingono lakini binti alipomjulisha kwamba anatoka na boss wake alimshauri akaripoti kwa wahusika wanaopokea kesi za aina hio na binti akaenda kuripoti. Baada ya kikao cha nidhamu akaachishwa kazi kwa gross negligence. Hivi hapo haki ilitendeka kweli au ni mpango wa kudhurumu kiinua mgongo cha jamaa, maana alikuwa ndio anakaribia kustaafu.