Nenda ofisi za NSSF kama ulivyoelekezwa hapo juu na Iceberg9,ukifika omba updated statement ataenda nayo ofisi ya ukaguzi kama ilivyoelezwa hapo juu,na watakupa Adjustment form(Fomu ya marekebisho ya michango)ambayo utapaswa kupeleka kwa mwajiri ili aijaze au kuingiza hiyo michango ambayo hakupeleka,ila pia hakikisha unakuwa na salary slip zako ilikuthibitisha kuwa ulikuwa unakatwa kiasi fulani kutoka katika mshahara wako na mwajiri kwa ajili ya NSSF au nakala ya makubaliano endapo mwajiri angelipa kiasi chote cha asilimia 20(20%)mwenyewe pasipo kukata katika mshahara wako.