Nimepewa kesi ya wizi wa kuaminiwa na boss wangu hii ni baada ya migogoro ya kikazi na baada ya mm kuwa nafanya kazi Kwa muda mrefu bila mkataba na nikaomba kuacha kazi
pesa ninazo tuhumiwa nazo sikupewa kama ilivyoelezwa na hakuna sehem au ushahidi wowote kwamba pesa hizo nimezipokea na sikuwa nafaham lolote , siku nimefikishwa police maelezo yaliandikwa na police Kwa matwaka yake yeye Mimi nililazimishwa kuweka sahihi na sikuwa na namna kama mjuavo police wetu, .. nilipewa na nasubiri kama kuna kwenda mahakamani ama vp,
Naombeni kama kuna msaada hapa..
Tajiri anatumia pesa kuninyanyasa na police kwani nafaham mambo mengi ya office na ananilazimisha kufanya kazi , kikubwa nilikataa kuendelea na kazi