Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)


Kama mfanyakazi ameajiriwa kwenye taasisi yoyote ya serikali kima cha chini ni 300,000 mkuu, nadhani hii kima ya chini ya serikali ni ile aliyoacha JK kabla ya kuachia madaraka 2015, hivyo nilivyotaja hapo juu ni kwa sekta binafsi tu.
 
Mkuu nimelipata somo apo juu,naomba kujua staiki za mtu anapoamishwa anapaswa kulipwa nini na nini na kanuni ya ukokotoaji wake,asante
 
Naomba kanuni ya ukokotoaji wa uhamisho na staiki zake
 
Deonova naomba ushauri kuhusu shauri kesi ya kazi iliyopo CMA na mfanyakazi kashinda kesi tume imeamuru arudishwe kazini mfanyakazi amekwenda kuripoti kazini tarehe aliyoambiwa chakushangaza mwajiri ana sema kampuni haina utaratibu mfanyakazi akiondolewa kazini imrudishe je?

Hapo mfanyakazi afate utaratibu gani mana mwajiri amemwambia kwa mdomo tu hakuna barua yeyote
 
Karibu sana
Deonova naomba ushauri kuhusu kushinda kesi CMA mimilikua nafanya kazi kampuni moja kubwa sana hapa mjini nimeshinda kesi CMA tume imeamuru nirudishwe kazini tarehe imefika narudi kuripoti muajiri anasema kampuni haina utaratibu mtu akiachishwa arudishwe tena alafu anaongea kwamaneno bila barua yeyote je? nifate taratibu gani? naomba ushauri wa kuu
 
Mkuu nimelipata somo apo juu,naomba kujua staiki za mtu anapoamishwa anapaswa kulipwa nini na nini na kanuni ya ukokotoaji wake,asante

Kama ni mtumishi wa umma hebu pitia vile vifungu vha J.1 had J.26 cha Public Service Standing Orders; 2009 utapata kujua nini unapaswa kulipwa mkuu. Na kama ni mfanyakazi ktk sekta binafsi kwa taratibu za utendaji bora lazima ulipwe nauli na posho ya kujikimu hadi unapofika ktk kituo chako kipya cha kazi, gharama za kusafirisha mizigo (kama ipo), na gharama za malazi angalau kwa siku 7 wakati unatafuta nyumba ya kuishi kule point B (kama kampuni haijakupangia nyumba ya kuishi).

Lakini pia hapa mjadiliane na mwajiri wako kuona namna bora zaidi ya kufanikisha haya.
 

Je, mwajiri alikuwepo siku ya kusomwa Rulling na/au alipatiwa nakala ya ile rulling mkuu?
 
Hatukusomewa hukumu ila nakala kila upande ulipewa na tulisaini
 
Happy mapinduzi day

Nimeguswa kuandika Uzi huu kwa ajili ya kuelimishana kuhusu sheria za kazi,haki za mtumishi na wajibu.

kwanini!!?

ni kwa sababu kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kazi na haki za waajiriwa,hii inatokana na ukweli kwamba waajiriwa wengi wapya wanaanza kazi bila kujua haki zao kitu kinachofanya kuwa watumwa wa ajira lakini pia wengi hawajui wajibu wao.

mfano.

mikataba inayosainiwa na walimu wapya kati yao na serikali,huwa hawatoi hata dakika moja ya mtu kusoma na kuelewa content ya mkataba,huwa inasainiwa kwenye ukumbi wa halmashauri tena kwa kuambiwa nini cha kujaza.

hiyo ni mfano lakini iko mfano mingi zaidi..

karibuni
 
inapogundulika mwajiriwa amekiuka sheria za kazi,utaratibu gani unapaswa kufuatwa ili kumuwajibisha?
 
Mimi kuna kampuni nimefanya Kazi miaka mnne sasa nataka niache kazi kwa sababu ya maslai sio mazuli nifanyeje ilinilipwe haki zangu zote kwasababu nasikia ukiacha kazi mwenyewe unakua umejinyima haki yako ya mafao yako naombeni mwongozo
 
Je? Ni haki kwa kampuni ambayo anafanya shughuli zake ambazo ni endelevu kuwapa wazawa wote bila kujali aina ya kazi yake na cheo chake , mkataba wa mwaka mmoja mmoja. ( ref kifungu cha 14. Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina zifuatazo- (a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa; (b) mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kada za wataalamu na mameneja (c) mkataba wa kazi maalumu. (2) Mkataba na mfanyakazi unatakiwa kuwa wa maandishi ikiwa mkataba unaeleza kuwa mfanyakazi atafanya kazi nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
 
Je? ni haki kwa kampuni ambayo anafanya shughuli zake ambazo ni endelevu kuwapa wazawa wote bila kujali aina ya kazi yake na cheo chake, mkataba wa mwaka mmoja mmoja. Ref kifungu cha 14 cha sheria na mahusioano mahara pa kazi (14) Mkataba na mfanyakazi utakuwa wa aina zifuatazo- (a) mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa; (b) mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa kwa kada za wataalamu na mameneja (c) mkataba wa kazi maalumu. )
 
aisee Kama unayo ktk PDF naomba uni pm
 
Je wewe mleta mada ndio utakao kua unajibu maswali yetu na kutupa ushauri wa kisheria au na wewee hujui unangojea waje wanasheria? Umeulizwa wiki sasa hautoi majibu hapo juu.
 
Ndio ni haki, na pili unapaswa kujua kua formalities za mkataba ni makubaliano ya pande mbili zote, na upande usiporidhia basi usi saini huo mkataba.
 
Mimi kuna kampuni nimefanya Kazi miaka mnne sasa nataka niache kazi kwa sababu ya maslai sio mazuli nifanyeje ilinilipwe haki zangu zote kwasababu nasikia ukiacha kazi mwenyewe unakua umejinyima haki yako ya mafao yako naombeni mwongozo

Sio kweli, kuacha kazi hakuna uhusiano wowote na haki zako za mafao kuathirika, kila kazi ni mkataba, upande mmoja unaweza kuuvunja mkataba usika kwa sababu zake maalumu, na ikiwa vyema mbele ya macho ya sheria basi upande huo uanze kufuatilia mafao na kupewa stahiki zake za pale mafao yalipofikia, tena hii mara nyingi huitwa fao la kujitoa.
 
Unapoitwa kutoka kituo cha kazi kwenda makao makuu lisilo eneo la kazi kwa mahojiano nani anagharimia gharama za usafiri, malazi na chakula? (Mwajiri au Mwajiriwa )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…