Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MwajiriUnapoitwa kutoka kituo cha kazi kwenda makao makuu lisilo eneo la kazi kwa mahojiano nani anagharimia gharama za usafiri, malazi na chakula? (Mwajiri au Mwajiriwa )
Aksante!Mwajiri
Mkuu Deonova, ahsante sana kwa madini murua kabisa. Kuna baadhi ya makampuni huzuia baadhi ya wafanyakazi Kuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi kwa kigezo Kuwa wao wapo kwenye kundi la management! Je, hiyo ni sahihi kwa mujibu wa sheria??
Mimi nilikuwa mfanyakazi wa sekta binafsi,waliniajili nikiwa kitua A baadae wakaniamishia kituo B,kwa sasa wameniachisha kazi kwa madai gharama za uendeshaji kuwa kubwa,wakati ananiachisha ameshindwa kuniludisha kituo A ambacho aliniajili,nimeludi kwa gharama zangu baada ya kusubili kwa mwezi mzima bila mafanikio,je nastaili haki gani nataka nikadai.
unajua namna ile hesabu ya malipo kwa kilomita inavyofanywa?!Unastahili kulipwa repatriation costs to the place of recruitment, kama wanakwepa kulipa fungua shauri CMA ktk mkoa ulipo mkuu.
Nimekuwinda labour officer nmekupataVillky_J,
hii nimetoa kwenye nyaraka zangu ambazo nimezisave kwenye pc kwa ajili ya kazi na hizi tunaandaa kutokana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za Ajira Namba 7 ya Mwaka 2004 na kutokana na maazimio mbalimbali ya ILO na miongozo ya wizara.
in short mimi hizi ndo kazi zangu za kila siku chief kama Labour Officer (Ofisa wa Kazi)
Nimekuwinda labour officer nmekupata
Naomba unsaidie katika mshahara wa mfanyakazi ni sehemu hipi inakatwa makato ya SOCIAL SECURITY FUND, PAYE, na makato mengine, je ni basic salary au gross yote...allowances, bonus, incentives je zinakata kodi kwny mshahara???
Smamahani mkuu naomba kuuliza
Hivi mkataba wa mwaka mmoja una malipo ya kiinua mgongo
Ufafanuzi tafadhali....
Najee kama kila mwaka unasaini mkataba wa mwaka mmoja mmoja kuna malimbikizo ya kuto kulipwa kinua mgogo?
Asante mkuu...
Je, kulipwa kiinua mgongo ni haki kisheria kwa kila mfanyakazi paspo kutokea ulalamishi waaina yoyote.. Iwe
Natambua amasitambui juu ya sheria ya mikataba ya kazi...naikitokea kama nafanyiwa dhuluma yakuti kupewa kiinua mgogo changu nichukue hatua gani?
Habari mkuu, naomba ushauri kuhusu suala langu hili, Mimi ni mfanyakazi katika kampuni binafsi...nimefanya kazi mwaka mmoja na nusu na katika kipindi hicho sikupata mkataba wa ajira licha ya kuomba mara nyingi kupewa mkataba na nyongeza ya mshahara, kwa bahati nyingine nimepata nafasi ya kazi kwenye kampuni nyingine. Je itanilazimu nimpe taarifa bosi kwa barua au nimwambie ana kwa ana? Maana nimempa taarifa ya kwamba naenda kujiendeleza kimasomo na sikutokuwepo kazini baada ya siku 28 zijazo ameonyesha kutoridhika na taarifa hiyo. Naomba kujua kama ni lazima niandike barua juu ya taarifa hiyo.??
Nawasilisha..