Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Mkuu Deonova, ahsante sana kwa madini murua kabisa. Kuna baadhi ya makampuni huzuia baadhi ya wafanyakazi Kuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi kwa kigezo Kuwa wao wapo kwenye kundi la management! Je, hiyo ni sahihi kwa mujibu wa sheria??
 
Mkuu Deonova, ahsante sana kwa madini murua kabisa. Kuna baadhi ya makampuni huzuia baadhi ya wafanyakazi Kuwa wanachama wa vyama vya wafanyakazi kwa kigezo Kuwa wao wapo kwenye kundi la management! Je, hiyo ni sahihi kwa mujibu wa sheria??

Nadhani wanarefer kifungu cha 9-(1) (c) kinachosema "a senior management employee may not belong to a trade
union that represents the non-senior management employees of the employer."
Sheria nnayoquote hapa ni ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004

Sasa senior management employee ni yule mfanyakazi ambaye ameshafikia ktk ngazi ya kuwa afisa mwandamizi wa taasisi husika ambaye ana power ya kurepresent taasisi nje ya hiyo taasisi na ana power ya kutunga sera on behalf ya hiyo taasisi. Kama upo kundi hilo basi wewe unaweza kujumuishwa kwenye kundi la chama cha Waajiri manake waajiri nao wana chama chao (Association of Tanzania Employers - ATE), sasa kama unakuwa umeshakuwa vested power ya kuweza kuwakilisha taasisi yako kwenye forum kama hizi huwez at the same time kuwa kwenye chama cha wafanyakazi manake utakuwa sasa kwenye chama cha wafanyakazi lets say unalalamika kule mfano kwa mambo ambayo taasisi haifanyi vizuri, while ukiwa huku ATE kama mwakilishi wa taasisi unatakiwa kuja na solution. Unaona sasa inavokuwa ngumu kuplay role mbili zinazokinzana.

Sijui utakuwa umenipata hapo mtumishi.
 
Mimi nilikuwa mfanyakazi wa sekta binafsi,waliniajili nikiwa kitua A baadae wakaniamishia kituo B,kwa sasa wameniachisha kazi kwa madai gharama za uendeshaji kuwa kubwa,wakati ananiachisha ameshindwa kuniludisha kituo A ambacho aliniajili,nimeludi kwa gharama zangu baada ya kusubili kwa mwezi mzima bila mafanikio,je nastaili haki gani nataka nikadai.
 
naomba kuuliza kwa anayejua namna hesabu ya gharama za kumsafirisha muajiriwa aliyevunjiwa mkataba na muajiri wake.
 
Mimi nilikuwa mfanyakazi wa sekta binafsi,waliniajili nikiwa kitua A baadae wakaniamishia kituo B,kwa sasa wameniachisha kazi kwa madai gharama za uendeshaji kuwa kubwa,wakati ananiachisha ameshindwa kuniludisha kituo A ambacho aliniajili,nimeludi kwa gharama zangu baada ya kusubili kwa mwezi mzima bila mafanikio,je nastaili haki gani nataka nikadai.

Unastahili kulipwa repatriation costs to the place of recruitment, kama wanakwepa kulipa fungua shauri CMA ktk mkoa ulipo mkuu.
 
Unastahili kulipwa repatriation costs to the place of recruitment, kama wanakwepa kulipa fungua shauri CMA ktk mkoa ulipo mkuu.
unajua namna ile hesabu ya malipo kwa kilomita inavyofanywa?!
 
Villky_J,
hii nimetoa kwenye nyaraka zangu ambazo nimezisave kwenye pc kwa ajili ya kazi na hizi tunaandaa kutokana na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya Mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za Ajira Namba 7 ya Mwaka 2004 na kutokana na maazimio mbalimbali ya ILO na miongozo ya wizara.

in short mimi hizi ndo kazi zangu za kila siku chief kama Labour Officer (Ofisa wa Kazi)
Nimekuwinda labour officer nmekupata
Naomba unsaidie katika mshahara wa mfanyakazi ni sehemu hipi inakatwa makato ya SOCIAL SECURITY FUND, PAYE, na makato mengine, je ni basic salary au gross yote...allowances, bonus, incentives je zinakata kodi kwny mshahara???
 
Nimekuwinda labour officer nmekupata
Naomba unsaidie katika mshahara wa mfanyakazi ni sehemu hipi inakatwa makato ya SOCIAL SECURITY FUND, PAYE, na makato mengine, je ni basic salary au gross yote...allowances, bonus, incentives je zinakata kodi kwny mshahara???

Social security inakatwa kabla ya makato yoyote (ukiachilia mbali hii ya bodi ya mikopo "loan board" ambayo inakatwa before any deduction hata kabla ya social security). Baada ya social security kukatwa kinachofuata kukatwa ni PAYE.

Kuhusu allowances kama ni allowance ambazo ziko fixed zinatozwa kodi. Labda bonus tu ambayo haiko fixed manake mwez huu unaweza kuipata, mwezi ujao usiipate kutegemeana na performance. Ila hapa watu wa TRA wanaweza kuongezea ufafanuzi mzuri zaidi kuliko mimi mkuu.
 
Smamahani mkuu naomba kuuliza
Hivi mkataba wa mwaka mmoja una malipo ya kiinua mgongo
Ufafanuzi tafadhali....
Najee kama kila mwaka unasaini mkataba wa mwaka mmoja mmoja kuna malimbikizo ya kuto kulipwa kinua mgogo?
 
Smamahani mkuu naomba kuuliza
Hivi mkataba wa mwaka mmoja una malipo ya kiinua mgongo
Ufafanuzi tafadhali....
Najee kama kila mwaka unasaini mkataba wa mwaka mmoja mmoja kuna malimbikizo ya kuto kulipwa kinua mgogo?

Ndio, ukishatimiza mwaka mmoja unastahili kiinua mgongo manake hata ktk ukokotoaji wake ni lazima uwe umefanya kazi kwa mwajiri huyo sio chini ya miezi 12 (unless otherwise iwe kwamba mlikubaliana kulipana kiinua mgongo kwa ukokotoaji wa asilimia ya kila mwezi "Gratuity")

Lakini sasa ili ustahili kiinua mgongo nilichoelezewa hapo mwanzo ni lazima;
1. Usitishwaji wa ajira yako uwe umefanywa na mwajiri. (termination has been initiated by employer). Hii ina maana ukiacha kazi mwenyewe ama endapo mkataba umeisha/umefikia kikomo basi hautastahili kulipwa kiinua mgongo
2. Uwe umefanya kazi kwa mwajiri huyo mfululizo/hata kama sio mfuliluzo basi vipindi tofauti tofauti ulivyofanya naye kazi vikunganishwa visiwe chini ya miezi 12

Kuna swali umeuliza hapo kuwa kama unasaini mkataba wa mwaka mmoja mmoja je kuna malimbikizo ya kiinua mgongo?
Jibu ni ndio manake ajira yako ilikuwa endelevu maana ulikuwa unarenew mkataba kila mwaka so itaunganishwa miaka yote uliyofanya kazi, mwajiri atakapositisha ajira yake basi ukokotoaji wa kiinua mgongo utachukulia miaka yote uliyofanya kazi.

Kitu kingine kikubwa cha kuangalia hakikisha unasoma mkataba vizuri kabla ya kuusaini, manake kuna waajiri wanaweka vifungu vya kujihami na malimbikizo mfano unakuta kipengele kinasema "Mkataba huu unafuta makubaliano mengine yoyote yaliyowahi kufanyika huko nyuma" au "kwa makubaliano hayo ninakiri sina madai mengine yoyote ya nyuma" lazima uwe makini na ikiwezekana omba ushauri/ufafanuzi kwa mwajiri au mwanasheria yoyote kabla ya kusaini mkataba wako. Kama umeandikwa kwa kiingereza na huelewi basi mwajiri ana wajibu wa kukufafanulia kipengele kwa kipengele ili uelewe. Usikimbilie tu kusaini mkataba kwa sababu uko desperate na kupata hiyo ajira.

Katika moja ya career training nilizowahi kupata nikiwa chuo miaka ya nyuma trainer alikuwa anatuambia unapoenda mahali kufanya usaili ama kusaini mkataba hakikisha hauna njaa, make sure umekula na umeshiba vizuri, kwa sababu ukiwa na njaa unajikuta unajibu maswali ya usaili hadi unatia huruma au unasaini mkataba fasta bila hata kuusoma kwa sababu una njaa. Ukiwa umeshiba unakuwa na confidence kwenye usaili na kama ni mkataba unasaini ukiwa umerelax.

BTW...sorry kwa maelezo ya zaida, nilikuwa najaribu kupanua mjadala tu.
 
Asante mkuu...
Je, kulipwa kiinua mgongo ni haki kisheria kwa kila mfanyakazi paspo kutokea ulalamishi waaina yoyote.. Iwe
Natambua amasitambui juu ya sheria ya mikataba ya kazi...naikitokea kama nafanyiwa dhuluma yakuti kupewa kiinua mgogo changu nichukue hatua gani?
 
Asante mkuu...
Je, kulipwa kiinua mgongo ni haki kisheria kwa kila mfanyakazi paspo kutokea ulalamishi waaina yoyote.. Iwe
Natambua amasitambui juu ya sheria ya mikataba ya kazi...naikitokea kama nafanyiwa dhuluma yakuti kupewa kiinua mgogo changu nichukue hatua gani?

Ingawa sijakuelewa vizuri swali lako hapa.......ila ngoja nijaribu kujibu vile nimeelewa kama ntakuwa sijakidhi hitaji la swali utaniuliza tena mkuu. Kiinua mgongo ni haki ya mfanyakazi aliyesitishiwa ajira yake na mwajiri (ajira iliyositishwa na mwajiri kabla ya mkataba kufikia ukomo wake wa muda). Nasema ni haki yake kwa msingi wa section 42 of Employment and Labour Relations Act No. 6 of 2004 imeeleza vizuri pale.

Kama unafanyiwa dhuluma ya kutokulipwa stahiki hiyo (wakati unastahili) basi huna budi kumfungulia mwajiri kesi katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kikazi {Commission for Mediation and Arbitration (CMA)} katika mkoa uliopo.

NB: Nimeandika 'kama unastahili' kwa sababu hii....

(2) An employer shall pay severance pay on termination of emploment if-
(a) the employee has completed 12 months continuous service with an employer; and
(b) subject to the provisions of subsection (3), the employer terminates the employment.
 
Asante deonova kwa hii thread, unastahili pongezi za dhati maana kweli unatusaidia kwenye swala la haki za kazi.
Naomba msaada kwa yafuatayo, sijui sheria inasemaje?
Niliajiriwa na muhindi, sina mkataba na miaka 3 imepita sasa, nimesoma natambulika kisheria kuwa na haki zote kikazi.
Niliahidiwa kuanza na mshahara wa lak8, na baada ya miezi utapanda hadi 1.2m, kumbe zilikuwa story za kunivuta, kazi ni ya ukandarasi.

1. Nilipelekwa kigoma kusini toka dar, nikawa napokea lak8 kwa mwezi na lak1 ya chakula, kulala kambini kazini.
Je, nafaa kulipwa daily allowance? hata kama nilikuwa sijui sheria inasemaje, nilikaa kule miezi 9 mfululizo na kazi kila siku isipokuwa siku za mvua na baadhi ya sikukuu. Bado naweza kudai?, maana kwa siku ni 40,000 x miezi9

2. Niliomba mkopo wakati niko kazini kigoma kipindi hicho, nikapewa 2m, ambayo ilianza kukatwa mwezi huo huo, na nilikatwa lak5 kila mwezi, na nilishaomba deni nianza kulilipa baada ya miezi3 ili kujipa muda wa kutatua shida lakini nikawa sina budi maana pesa zilikatwa juu kwa juu. Je sheria inasemaje kwenye ulipaji deni na kwa asilimia ngapi maana naona ilikuwa ni kiwango cha juu na nikajipata nina shida zaidi kutokana na hilo.

3. Miezi miwili baada tu ya kumaliza miradi na kurudi dar, nikapunguziwa mshahara kiasi cha lak3, nilikataa kitendo hicho na boss mwenyewe akasema kama sikubaliani na mshahara nitafute kazi kwingine. Sababu ya punguzo alidai biashara imekaa vibaya na sababu ni utawala mpya kukaza vyuuma, je bado naweza kudai kiasi nilichopunguziwa kisheria? miaka miwili imeshapita tangu punguzo, na boss alitoa ahadi atalipa biashara ikiwa nzuri, cha ajabu kampuni inaiingiza pesa na yeye kila siku analia njaa, sheria inaweza kunisaidia kulipwa lak3 zangu nilizokatwa kwa miaka 2 sasa?

4. Likizo sijaenda miaka 3 yote ya ajira, na wiki iliyopita baada ya kuona hali mbaya nikaamua kwenda kudai pesa za likizo za nyuma, maana niliona ni bora kuliko kuomba mkopo tena, boss kama mbogo na kusema badala ya kunilipa eti nichukue likizo ya miezi hiyo 3 mfululizo, nikagoma na kwa mara nyingine kuambiwa kama siwezi kazi nitafute nyingine. Je, nina haki ya kupata pesa za likizo hizo?

5. Kazini kwetu, ingawa ni kampuni kubwa, lakini hatulipiwi nssf,wcf,sijui paye wala chochote cha uzeeni, miaka 3 sasa bila mafao, je hii imekaaje? Ninahaki nazo bado?

6. Naona kuuna mazingira yanawekwa kuufanya kazi iwe chungu kwangu nijiachishe, jambo ambalo siwezi bila kupata haki zangu nilizouliza hapo juu, yyaani naingizwa umaskini na boss. Je, naweza kujiachisha kazi kwa msingi wa "constructive dismissal" na bado kulipwa madai yangu?

Samahani kwa uzi mrefu na maswali mingi. Ushahidi ninao wa vitu kibao utokanao na madai yangu, je muda unaruhusu kudai ama siku nyingi tayari zimepita na imekula kwangu?

Pia huyo boss ana kampuni mbili ambazo kazi zinaiingiliani, na huwa nafanya kutokana na shida na majukumu, lakini kama nitaamua kupeleka madai yangu mahakamani, je naweza kushinda, ama nitakuwa napoteza muda tu?

Nashukuru kwa muda wako, nawasilisha.
 
Habari mkuu, naomba ushauri kuhusu suala langu hili, Mimi ni mfanyakazi katika kampuni binafsi...nimefanya kazi mwaka mmoja na nusu na katika kipindi hicho sikupata mkataba wa ajira licha ya kuomba mara nyingi kupewa mkataba na nyongeza ya mshahara, kwa bahati nyingine nimepata nafasi ya kazi kwenye kampuni nyingine. Je itanilazimu nimpe taarifa bosi kwa barua au nimwambie ana kwa ana?

Maana nimempa taarifa ya kwamba naenda kujiendeleza kimasomo na sikutokuwepo kazini baada ya siku 28 zijazo ameonyesha kutoridhika na taarifa hiyo. Naomba kujua kama ni lazima niandike barua juu ya taarifa hiyo?

Nawasilisha..
 
Nimeelewa sana mkuu sorry unaweza nisaidia majukumu ya baraza la wafanya kaz na jukumu la members wake katika halmashaur?
 
moneymakerman,

Asee ishu yako ni ndefuuuu....uko mkoa gani mkuu ili nikuunganishe na mtu/afisa anaweza kupokea nyaraka zako na kuzichambua na kuona namna tunaweza kusaidia mkuu?
 
Habari mkuu, naomba ushauri kuhusu suala langu hili, Mimi ni mfanyakazi katika kampuni binafsi...nimefanya kazi mwaka mmoja na nusu na katika kipindi hicho sikupata mkataba wa ajira licha ya kuomba mara nyingi kupewa mkataba na nyongeza ya mshahara, kwa bahati nyingine nimepata nafasi ya kazi kwenye kampuni nyingine. Je itanilazimu nimpe taarifa bosi kwa barua au nimwambie ana kwa ana? Maana nimempa taarifa ya kwamba naenda kujiendeleza kimasomo na sikutokuwepo kazini baada ya siku 28 zijazo ameonyesha kutoridhika na taarifa hiyo. Naomba kujua kama ni lazima niandike barua juu ya taarifa hiyo.??
Nawasilisha..

Ukisoma kifungu cha 61 cha Labour Institutions Act No. 7 of 2004 kinachoeleza "Presumption as to who is an employee", mojawapo au vipengele kadhaa kati ya vilivyotajwa pale kikiwepo basi hata kama hauna mkataba wewe unahesabika kuwa mwajiriwa halali wa hiyo taasisi mkuu.

Kinasema hivi...

For the purposes of a labour law, a person who works for, or renders service to, any person is presumed, until the contrary is proved, to be an employee, regardless of the form of the contract, if any one or more of the following factors is present

a) The manner in which the person works is subject to the control or direction of another person;

b) The person’s hours of work are subject to the control or direction of another person;

c) In the case of a person who works for an organization, the person is a part of that organization;

d) The person has worked for that other person for an average of at least 45 hours per month over the last three months;

e) The person is economically dependent on that other person for whom that person works or renders service;

f) The person is provided with tools of trade or work equipment by the other person; or

g) The person only works for or renders service to one person.


Kuhusu hilo suala la kuomba ruhusa ya kimasomo wakati unaenda kufanya kazi sehemu ingine, mwajiri akigundua hilo anaweza kuterminate ajira yako 'due to misconduct' manake kumdanganya mwajiri pia ni misconduct na utapoteza stahiki zako nyinginezo
 
Back
Top Bottom