Kama hujapewa notis ya miezi mitatu na umeshtukizwa siku moja kabla ukapewa barua ya kuachishwa kazi inakuwaje haki za msingi mimi nimeshtukizwa hata sijapewa barua ya miezi mitatu na wamenipa hela ya miaka miwili je ni haki nikipewa hizo za mahesabu ya siku saba ya mwaka mzima?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ya kuzingatia hapa ni;
1. Je mkataba wako wa ajira umetaja kipindi cha notice period ni miezi mingapi pale ambapo upande wowote unataka kusitisha makubaliano ya mkataba? kama ni miezi mitatu kama ulivyotaja hapo juu, na ukaondolewa kazini pasina kupewa muda wa notice uliotajwa kwenye mkataba, basi mwajiri analazimika kukulipa mshahara wa muda ambao ungeendelea kuhudumia ukiwa kwenye notice period (miezi 3)........i.e payments in liue of notice
2. Umesema umedumu kazini kwa muda wa miaka miwili; basi utastahili tena kudai malipo ya kiinua mgongo ambao
unakokotolewa mshahara wa SIKU 7 kwa kila mwaka uliokamilika (Formula hii hutumika pale ambapo mkataba haujataja njia nyingine bora zaidi ya ukokotoaji wa kiinua mgongo eg. kwa asilimia/gratuity)
NB: Stahiki zako kama una mashaka nazo kwamba hazikuchanganuliwa kwa usahihi, ama umenyimwa stahiki zako; inafaa kufungua kesi ya madai ktk Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ktk kipindi kisichozidi siku 30 kuanzia tarehe uliposimamishiwa ajira yako. Aidha unaweza kuwasilisha madai yako ukisimamiwa na Wakili utakayemchagua ambaye pia atakuongoza ktk kudraft madai yako kupitia form maalumu, au unaweza kutumia Chama cha Wafanyakazi ktk kusimamia kesi yako (kama wewe ni mwanachama), vyama ninavyozungumzia hapa ni kama TALGWU, TUGHE, TUICO, CHODAWU, COTWU (T), RAAWU, TAMICO, CWT, TEWUTA, etc. Kama hukuwa mwanachama wao bado unaweza kuwatumia (ingawa utachajiwa gharama za kusimamia kesi yako maana wewe sio mwanachama wao)