Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Mkataba wangu kwanza ni wakudumu hivyo haki zangu hazijafafabuliwa sawasawa kuna kipengele kimoja kimeandika kuwa (a)mshahara wa mwajiriwa kabla ya makato ya ppf,nssf na paye havijaandikwa ni shilingi ngapi hivyo hiyo ni moja ya utapeli
(b)Na vipengele vingine ni kuhusu saa za kazi hakuna maelezo meengi kama mikataba ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app

Upo Mkoa gani mkuu (kama hutojali) ili niweze kukuelekeza pa kuanzia
 
Mkuu! Binafsi nimefaidika sana na hii elimu uliyojitolea. Ninaomba msaada, mimi ninafanya kazi katika sekta binafsi ambapo niliingia mkataba wa miaka miwili mara ya kwanza, na ulipoisha nikaongeza mkataba mwingine wa miaka mitatu japo na wenyewe umeisha sasa hivi nipo tu nafanya kazi ila hatujasaini mkataba mwingine sasa hivi no mwezi was nane tangu kumalizika kwa mkataba wa pili.

Hii mikataba yote ambayo imeishaisha haikuwa na kipengele chochote kinachoonesha gratuity wala kiinua mgongo. Je endapo mwajiri wangu amehamua kusitisha ajira yangu, ninaweza kuclaim hicho "kiinua mgongo changu?" au naweza pia kuclaim gratuity yangu ambayo haikuoneshwa kwenye mkataba?

Ahsante
 
Mkuu! Binafsi nimefaidika sana na hii elimu uliyojitolea. Ninaomba msaada, mimi ninafanya kazi katika sekta binafsi ambapo niliingia mkataba wa miaka miwili mara ya kwanza, na ulipoisha nikaongeza mkataba mwingine wa miaka mitatu japo na wenyewe umeisha sasa hivi nipo tu nafanya kazi ila hatujasaini mkataba mwingine sasa hivi no mwezi was nane tangu kumalizika kwa mkataba wa pili. Hii mikataba yote ambayo imeishaisha haikuwa na kipengele chochote kinachoonesha gratuity wala kiinua mgongo. Je endapo mwajiri wangu amehamua kusitisha ajira yangu, ninaweza kuclaim hicho "kiinua mgongo changu?" au naweza pia kuclaim gratuity yangu ambayo haikuoneshwa kwenye mkataba?

Ahsante

Ndio mkuu, endapo ajira yako itasitishwa na mwajiri utastahili kulipwa kiinua mgongo, na kwa sababu mkataba haukutaja kama ukokotoaji utafanyika kwa utaratibu wa asilimia (gratuity) basi default formula itakayotumika ni ya Mshahara wa Siku 7 kwa kila mwaka uliokamilika (kuanzia mwaka ulipoanza kazi).......(i.e Daily Salary x 7 x Years of Service)
 
ni sahihi kwenda likizo bila mshahara yaani nimeenda likizo 1febr2019, nikapewa hela yangu ya likizo niliporudi nikaulizia salary nikaambiwa hakuna ni ileile ya likizo niliyopewa je hii ni sahihi
 
Nashukuru sana
 
ni sahihi kwenda likizo bila mshahara yaani nimeenda likizo 1febr2019, nikapewa hela yangu ya likizo niliporudi nikaulizia salary nikaambiwa hakuna ni ileile ya likizo niliyopewa je hii ni sahihi

Unapokuwa Likizo yako ya mwaka mshahara wako unapokea kama kawaida as if ungekuwepo kazini (paid leave); sasa Kifungu cha 5(2) cha Waraka wa Mishahara ya Kisekta (Labour Institutions Wage Order) kinatamka hivi...............An employee shall in addition to annual paid leave, be entitled to leave travel assistance once in every two years of continuous service with the same employer.

Kwamba kila baada ya miaka 2 ukiwa na mwajiri wako huyo huyo, utakuwa unapewa "leave travel assistance" (hii inajumuisha nauli yako na mwenza na watoto wako plus gharama mnazoweza kukutana nazo njiani mfano kulazimika kulala njiani mpaka kufika nyumbani unakoenda likizo pamoja na gharama za nauli ya kurudi). Tunaposema kila baada ya miaka 2 means mwaka huu ukienda likizo na ukapewa hizo leave travel assistance basi mwaka ujao hupewi, mwaka unaofuata unapewa, unaofuata hupewi.
NB: Hapa mshahara wako uko pale pale hata kama upo likizo.(annual leave)

Hii inaapply kwa watumishi wote wa Serikali na Private.
 
shukrani mkuu hawa jamaa wamenipiga
 
Naomba kujua ikiwa mtu umeajiriwa kwa mkataba wa makubaliano ya mdomo bila maandishi( oraly contract or agreement) yakufanya kazi bila kupewa muda wa matazamio na mwajiri wako, halafu baada ya miezi mtatu tu mwajiri akakuandikia barua ya kukufukuza kazi bila hata kukupatia sitahili zako zozote, je unayo haki ya kumshitaki? Na kama utamshitaki ni kwa sheria gani utamshitaki?

Yes unayo haki ya kumshitaki kama amekufukuza pasipo kuwa na sababu ya msingi na bila kukupa room ya kusikilizwa kabla ya uamuzi. Kwa mwajiriwa ambaye umefanya kaz kwa miez mitatu tu unaweza kushtaki kwa kitu tunaita kitaalam unfair labour practice.
 
Mkuu nimeitafuta sana sheria ya utumishi wa umma sheria namba 8 ya mwaka 2002 lakini hola hata kwenye website ya bunge hakuna..Kama unaweza kuibandika hapa itakua vizuri sana
wandugu, msihangaike kutafuta sheria. sheria zote za tz kuanzia mpya hadi za zamani, zipo kwenye website ya parliament of tz. nenda kule utaipata kwenye pdf. nashangaa wengine wanasema walikuwa wanatafuta sheria hizi, wakati ziko wazi sana, tena mno.
 
Unapokuwa umeumwa kama mwajiriwa sharti uende hospitali kutibiwa kama unaona hutaweza kutimiza majumu yako kikamilifu.kama hujiwezi utapelekwa na ndugu au jamaa na marafiki zako hospitalini

kama halikuwa jambo la dharula kabla ya kwenda hospitali utapitia hospitali kuomba kibari cha kwenda kutibiwa.utachukua sick sheet.

Sick sheet hii lazima ijazwe na daktari anayekutibu tena mahala pengine ijazwe na medical officer incharge maana ndiye anayesimamima matibabu hapo kituoni.ujazwaji wa sick sheet ni muhimu sana kwa mastakabali wa haki zako kazini .sick sheet yaweza kuchukuliwa na mtu yeyote ( kama sijakosea ) kwa maana hakuna mahala mgonjwa anasaini hivyo isipokuwa tu afisa rasilimaliwatu hivyo sioni sababu mtu mwingine asiichukuwe kwa niaba ya mwenzake.

Sick sheet ikishajazwa ni lazima irudishwe ofisini.
Daktari anaweza kuandikA chochote kwenye sick sheet kulingana na ugonjwa wako.

Utakaposema kuwa ulikuwa unaumwa hata kama ulitoa taarifa kwa simu,au watu walikuja kukuona hospitali,bado ni lazima upeleke sick sheet as an official document to be filed.Hili ni muhimu sana.
Katika swala la Mbunge ambaye amevuliwa ubunge wake je tukienda office za bunge kuna document hii kwenye file lake?
Kusema kuwa mbona katibu wa bunge alimwandikia kaka yangu ,mbona makamo wa rais alikuja nairobi kuniona,ulimwengu wote unajua naumwa,nakadhalika!! hii kwa mjibu wa sheria ya kazi haitoshi kumfanya mwajiri wako ajue uliko!! Ndugu zangu naomba wajiriwa wote kama mimi tulizingatie hili vinginevo tutajikuta tunatimuliwa kazi huku tukisema mbona bosi nilimpigia simu na alikuja kuniona hospitalini?Labda itumike huruma nyengine au busara nyengine napo inategemeana na uhusiano wako na bosi wako!!

Ukiandikiwa barua yoyote ukiwa hospitalini umelazwa ni vyema barua hiyo ikajibiwa vinginevo itaonekana haikufika au umeidharau.

Umelipwa stahiki zako ukiwa umelazwa .sawa.hata aliyekufa bado stahiki zake ziko pale pale.ukisema mlinipaje stahiki zangu wakati hamjui nilipo ??sawa .ofisi ilikosea kukulipa stahiki hizo.twende mahakani unirudishie stahiki hizo.

Tusipoteze haki zetu kwa kutozingatia sheria zetu!!
 
Mwajiri ana wajibu wa kumtibu mwajiriwa mpaka apone

Nakama hii inafanyika lazima mwajiri afahamu existence ya mwajiriwa

Vinginevo mwajiri hajatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria za afya na usalama kazini.
 
Back
Top Bottom