Unapokuwa Likizo yako ya mwaka mshahara wako unapokea kama kawaida as if ungekuwepo kazini (paid leave); sasa Kifungu cha 5(2) cha Waraka wa Mishahara ya Kisekta (Labour Institutions Wage Order) kinatamka hivi...............An employee shall in addition to annual paid leave, be entitled to leave travel assistance once in every two years of continuous service with the same employer.
Kwamba kila baada ya miaka 2 ukiwa na mwajiri wako huyo huyo, utakuwa unapewa "leave travel assistance" (hii inajumuisha nauli yako na mwenza na watoto wako plus gharama mnazoweza kukutana nazo njiani mfano kulazimika kulala njiani mpaka kufika nyumbani unakoenda likizo pamoja na gharama za nauli ya kurudi). Tunaposema kila baada ya miaka 2 means mwaka huu ukienda likizo na ukapewa hizo leave travel assistance basi mwaka ujao hupewi, mwaka unaofuata unapewa, unaofuata hupewi.
NB: Hapa mshahara wako uko pale pale hata kama upo likizo.(annual leave)
Hii inaapply kwa watumishi wote wa Serikali na Private.