Nimekusoma mkuu. .hongera kwa hilo
Je ikitokea kampuni haijawalipa wafanyakazi mishahara zaidi ya miezi 3 hatua gani mwajiriwa unaweza kuchikua na zikakusaidia kupata stahiki zako?!
Nashkuru kwa ufananuzi mzuriKuna option kama 3 za kufanya hapa;
1. Kama nyie ni wanachama wa Chama cha Wafanyakazi basi viongozi wa juu wa Chama (aidha ngazi ya tawi hapo kazini ama kutoka ngazi ya wilaya/mkoa) wanatakiwa kukaa na mwajiri kuona namna ya kumaliza mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo ya kirafiki
2. Kama hilo haliwezekana ama kama hampo kwenye chama cha wafanyakazi basi mnaweza kureport suala lenu kwa Afisa wa Kazi wa Mkoa uliopo ili aje kufanya ukaguzi na kufanya enforcement ya jambo hilo kwa 'Compliance Order'....afisa wa kazi anayo mamlaka hayo
3. Option ya tatu ni kufungua mgogoro ktk Tume ya Usuluhishi na Uamuzi wa Migogoro ya Kikazi (Commission for Mediation and Arbitration - CMA). Lakini hii iwe ni hatua ya mwisho kabisa manake mtakapofikishana na mwajiri ktk hatua hii ukumbuke kuwa mahusiano yenu ya kikazi hayatakuwa mazuri kama awali, so jambo jema ni kutafuta suluhu kwa njia za awali kwanza.
NB;
- Endapo haya madai yako unayadai ukiwa bado ndani ya ajira hakikisha hazipiti siki 60 kabla hujachukua hatua za kuyadai
- Endapo una madai ambayo tayari umeshaacha/kuachishwa kazi na unamdai mwajiri hakikisha unachukua hatua za kuyadai ndani ya siku 30 kuanzia ulipoachishwa kazi manake nje ya muda huo utasababisha Mwajiri alete pingamizi (preliminary objection) kwa hoja kuwa madai yako yapo nje ya muda endapo utafungua shauri CMA.
Mkuu nisaidie kidogo hapa, Mimi ni mwajiriwa serkalini, katika kutimiza majukumu yetu kulitokea mvutano kazini dhidi ya wanafunzi juu ya swala la mimba hivo mkuu aliamuru mtoto apimwe na walimu, mimi nikiwa kama mlezi wa darasa la mwanafunz huska, baada ya hapo ilikuja kuwa kesi kubwa huko tsd na kupelekea kuandikiwa barua ya kutokuwa na maadl kazini kisa tu nilipeleka taarfa kwa mkuu wa shule, wakati huohuo mkuu hakupewa barua yoyote ambapo ndie alie idhinisha mtoto kupmwa, tsd walitutaka maelezo ndan ya sku saba lakini ajabu mpaka sasa ni nwezi mzima na nusu hawajatujibu. Swali langu je tsd wako sawa kushindwa kunijibu ilihali wao walinipa mda wa kuwajibu? Je nimuda gani wanapaswa wawe wamenijibu toka wanituhumu? Je kwanini mkuu wangu hakuchukuliwa hatua ilihali ndie alietoa kibali cha mtoto kupmwa na walimu? Je ntakua sahh nikiwafuata wanipe mrejesho was kile niliwaeleza ikiwa sasa ni siku 45 tangu kuwaandikia na wamekaa kimya? Naomba msaada
Hebu niwekee hapa hicho kipengele make sina source ya kuweza kukipataHii case yako ni complicated kidogo, ila watumishi wa umma namna yao ya kushughulikia kesi zao ni tofauti na watumishi wa sekta binafsi, wa umma inahitaji kufuata mlolongo kidogo.
Lakini kwa haraka haraka hebu pitia Kifungu chote cha 126 cha Kanuni za Utumishi wa Umma (G.N No. 168) za Mwaka 2003; zinaweza kwa kiasi fulani kujibu changamoto yako, halafu kama kuna ziada uje tujadili chief.
Nashkuru kwa ufananuzi mzuri
Hebu niwekee hapa hicho kipengele make sina source ya kuweza kukipata
Mkuu samahani naomba kuuliza je iwapo umefanya kazi kwenye kampuni binafsi kwa zaidi ya miaka mitano bila ya mkataba unaweza pewa stahiki zako kama mfanyakazi mwenye mkataba?
Nashkuru kwa ufafanuzi mkuuKwa mujibu wa Sheria ya Taasisi za Ajira (Labour Instituions Act No. 7 of 2004) kifungu cha 61, wewe ni mwajiriwa halali na utastahili haki zote.......hebu tukisome kwa pamoja (Pressumption of who is an employee)
View attachment 615144
Nashkuru kwa ufafanuzi mkuu
Tsd wilaya Mkuu,Na je mkuu digba sowey hao waliokuambia uwaandikie maelezo ni TSD Wilaya ama TSD Mkoa?