Tanzania limekuwa taifa la wacheza kamari (Tanbet)

Tanzania limekuwa taifa la wacheza kamari (Tanbet)

Tbc a media state wakihimiza cheza pesa. Sijui madam boss ten sijui djaro arungu.. n.k. for sure tupo kwenye vicious cycle [emoji22]
Inasikitisha sana unapoona chombo kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi kinajihusisha na masuala ya kamari. TBC ndio waasisi wa kamari hapa nchini chini ya maelekezo ya CCM; ndio walikuwa wa kwanza kuchezesha kamari kwenye TV kwa jina la 'vunavuna' na waliwavuna kweli watanzania kabla ya wananchi kushtuka na kuachana na huo ushetani.

Serikali ya CCM kwa maana hiyo, pamoja na kuwalemaza wananchi kiuchumi wameona hiyo haitoshi wameanza kuwachezesha kamari za kipumbavu na kuwasababishia uteja usiokuwa wa lazima.
 
Illiteracy IPO kubwa Tanzania,inasikitisha sana kuona vijijini mpaka zile 200Tsh zao watu wanazitamani Kwa kuwaketea madude kama haya.





View attachment 2665574
Hii dhambi imeenezwa na CCM hadi kijijini. Wananchi wanatopea kwenye umasikini lakini hata ile Tsh 200 waliyobaki nayo kujikusuru na ukali wa maisha, CCM wanaimezea mate na kuichukua. Inauma sana.
 
kwakweli hili tama mimi nilkuwa naliwaza mnoo. yaani tbc redios mdq wote wanahimiza kamali badala ya kuhimiza watu wafanye kazi. inakera mnoo mnoo. viongozi ebu mwambie huyo mkurugenzi wa tbc kama hawezi kazi aondoke mara moja mjinga mmoja tu. tunajenga taifa gani hili?
Inakera mno tena sana. Na kibaya zaidi kamari inachezeshwa 24/7. Hii nchi CCM wameiharibu sana. Itachukua miaka 100 kusahihisha huu uraibu ulioingizwa vichwani mwa watanzania. Sijawahi kuona uongozi wa kiqumer hapa ulimwenguni kama uongozi wa CCM. Hawa jamaa ni zaidi ya mbwa!
 
Kamari imeharibu vijana. Wengi wanapenda sana mtelemko. Kamari imezaa vibaka wengi mitaani wana ulaibu kuliko hata watumiaji wa mihadarati. Wazazi tushituke. Tuwafanyie concealing vijana wetu.
 
Kila mtu afanye kile anachodhani kwake kitampa maisha na faraja ilimradi tu usimkwaze mwingine na kuvunja sheria.
Tatizo wacheza kamari wanatukwaza kwa kutuibia mali na kutukaba kutupora pesa ili wapate pesa ya kuchezea kamari. Wewe huoni hili ni tatizo mkuu?
 
Kila mtu atavuna alichopanda,kama wao wamepanda mbegu ya betting basi watavuna betting,na wewe kama umepanda kutobetting basi utavuna kuto betting!.
Hawa vijana wadogo, wengine under 18, wanaoharibiwa na betting sio uchaguzi wao bali wamemasikinishwa na CCM hadi wakawa hawana chaguo lingine zaidi ya kujiingiza kwenye betting.

Pia yapaswa utambue kwamba bila serikali ya CCM kuhalalisha huu ujinga kusingekuwa na betting. Kwa hiyo usitetee udhalimu wa CCM kwa kisnigizio cha maamuzi binafsi. Wacheza kamari hawajaamua kucheza kamari kibinafsi bali wamelazimishwa na umasikini uliosbabishwa na CCM.

Kama unadhani kubet ni jambo la faida mbona akina Mo na Bakhressa hawabeti? Ni kwanini masikini tu ndio wamejazana kwenye betting? Usitetee ujinga mkuu.
 
Las Vegas

Macao

UK

Spain

Germany

Hizo nchi zaongoza kwa kamari


Afu kingine msifatilie maisha ya watu
Hawo unaojifananisha nao wanalingana na wewe kiuchumi au unataka kutetea ujinga kwa hoja dhaifu?
 
Kamari imeharibu vijana. Wengi wanapenda sana mtelemko. Kamari imezaa vibaka wengi mitaani wana ulaibu kuliko hata watumiaji wa mihadarati. Wazazi tushituke. Tuwafanyie concealing vijana wetu.
Asante mkuu kwa kugundua hili. Wazazi inabidi wachukue maamuzi ya kuwazuia watoto wao wasijiingize kwenye kamari kwa kuwa lengo la serikali ni kuharibu kizazi cha vijana kwa kuwabetisha kamari ili waendelee kukaa madarakani. Inauma sana.
 
Uchambuzi mzuri.
Mwenyewe sifurahishwi TV ya taifa kuhangaika na kamari. Pia sifurahishwi na kamari kama tatu mzuka sijui Biko! Zimekaa kiwizi wizi.

Note: Mimi kamari nacheza -Football. Ina changamoto zake kama ulivyosema lakini ni maamuzi ya mtu, pia ni burudani, na pia napiga pesa kiasi (sio za kujenga)
 
We fanya yako usiingilie maisha ya watu
Mbona sisi raia wacheza kamari wanaingilia maisha yetu kwa kutukaba na kutunyanganya fedha za kuchezea kamari? Ina maana mpaka hapo hujaona madhara ya kamari kwenye jamii au mpaka uje upigwe roba uvunjwe meno ndipo ujue ubaya wa kamari?
 
Back
Top Bottom