Tanzania limekuwa taifa la wacheza kamari (Tanbet)

Tanzania limekuwa taifa la wacheza kamari (Tanbet)

Mtoa mada ni mcheza kamari mzuri sanaView attachment 2665762View attachment 2665763
Screenshot_2023-06-22-21-43-18-657_com.quoord.jamiiforums.activity.jpg
 
Kabla ya kuilaumu serikali tujilaumu sisi wananchi ngazi ya familia. Wazazi wako bize na kutafuta hela na kushindwa kuwafundisha watoto kwamba kamari ni mbaya. Kila mzazi angetimiza wajibu kusingekuwa na wateja wengi wa betting. Kamari zilikuwepo toka enzi na enzi. Nikiwa kijana mdogo pale Arusha karibu na soko kuu kama unaelekea St Thomas Hospital kulikuwa na sehemu zenye hizo mashine ila wateja walikuwa ni watu wazima na huwezi kukuta mafuriko ya watu. Ila kutokana na mmomonyoko wa maadili kuanzia ngazi ya familia ndo siku hizi kila kona kuna kamari.
 
Kamari inajenga uchumi. Haya mambk ya maadili hiyo ni dini lakini kama serikali inapaswa kuangalia kodi basi
 
Kabla ya kuilaumu serikali tujilaumu sisi wananchi ngazi ya familia. Wazazi wako bize na kutafuta hela na kushindwa kuwafundisha watoto kwamba kamari ni mbaya. Kila mzazi angetimiza wajibu kusingekuwa na wateja wengi wa betting. Kamari zilikuwepo toka enzi na enzi. Nikiwa kijana mdogo pale Arusha karibu na soko kuu kama unaelekea St Thomas Hospital kulikuwa na sehemu zenye hizo mashine ila wateja walikuwa ni watu wazima na huwezi kukuta mafuriko ya watu. Ila kutokana na mmomonyoko wa maadili kuanzia ngazi ya familia ndo siku hizi kila kona kuna kamari.
Haya yote yamesababishwa na serikali ya kifisadi ya CCM pale inapoweka kamari kama chanzo chake kikuu cha kujipatia fedha. Inauma sana.
 
Haya yote yamesababishwa na serikali ya kifisadi ya CCM pale inapoweka kamari kama chanzo chake kikuu cha kujipatia fedha. Inauma sana.
Mlee mtoto wako katika njia impasayo. Kamari zilikuwepo enzi na enzi. Humu JF kuna nyuzi kibao za watu kutelekeza watoto. Je ni CCM pia imehusika?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kuwachosha. Inasikitisha kuona kwamba nguvukazi ya taifa inapotea bure kwa kujikita kwenye uchezaji wa kamari. Kwa utafiti mdogo niliofanya, kamari imekita mizizi kila mahali. Mara nyingi watu wanapobishana kuhusu jambo fulani utawasikia wakiwekeana dau (kamari). Hiki ni kiashiria kuwa kamari imeingia damuni mwa kila mtanzania.

Redio zote nchini Tanzania, ikiwemo TBC, wanachezesha kamari, na nyingine huchezesha kwa saa 24 na kutoa matokeo kila baada ya nusu saa. Tunajenga taifa la wacheza kamari kwa lazima kisa tu serikali inapata mapato. Kibaya zaidi na serikali inaweka mkazo kwenye kamari kuliko kutafuta mbinu mbadala za kujenga ajira kwa vijana ili kuokoa taifa linalotopea kwenye uraibu wa kamari.

View attachment 2665544
Kijana aliyelemewa na uraibu wa kamari (Chanzo: JamiiForums Facebook page)
Niliwahi kutembelea kijiji kimoja ambako wizi wa mazao, mifugo na mali umeshamiri kwa kiasi kikubwa. Nilipofanya utafiti nikagundua chanzo cha wizi ni vijana ambao huiba mali za wananchi ili wapate fedha za kuchezea kamari. Tunajenga taifa la namna gani? Wallah miaka michache ijayo hata serikali nayo itaanza kucheza kamari kwa kutumia kodi za wananchi!

Katika hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24, jedwali namba tano linaonyesha mgawanyo wa bajeti kisekta. Sehemu inayoonyesha "Maendeleo ya Uchumi", utaona kuwa Vijana, Kazi na Maendeleo ya Kukuza Ujuzi, fedha ambazo zimetengwa ni Sh20.3 bilioni. Zikiwa zimepungua kutoka Sh31.2 bilioni, mwaka wa fedha unaoishia, yaani 2022-2023.

Taarifa hiyo itakushitua mno ukisoma ripoti ya uchumi wa michezo ya kubahatisha Tanzania. Mwaka wa fedha 2018-2019, mapato ya michezo ya kubahatisha yalikuwa Sh96 bilioni, yakiwa yamepanda kutoka Sh78 bilioni mwaka uliotangulia. Hiyo ni ripoti ya Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Mtandao wa utafiti na takwimu za kibiashara kwenye tasnia mbalimbali duniani, Statista Market Forecast, inaeleza kuwa mapato ya michezo ya kubahatisha Tanzania mwaka 2023 yanatarajiwa kufikia dola 75.09 milioni (Sh180 bilioni).

Kwa mujibu wa Statista, thamani ya soko la michezo ya kubahatisha Tanzania itakuwa dola 110.1 milioni (Sh260.4 bilioni), ifikapo mwaka 2027. Hali ikiwa hivyo, Serikali inapunguza fedha kwenye eneo la upishi wa vijana kuwa wataalamu.

Ukisoma Sheria ya Michezo ya Kubahatisha Sura ya 41 utaona kuwa mkazo mkubwa kwa sasa ni serikali kukusanya mapato kwenye michezo ya kubahatisha. Na pia serikali inakwenda kupunguza maumivu kwa wachezesha kamari kwa kuwapa punguzo la kodi kwenye mapato ghafi kutoka asilimia 25 hadi asilimia 18. Hapa maana yake waendeshaji wa kamari wataona ahueni zaidi. Hivyo, tutarajie makampuni yanayochezesha kamari kuongezeka hapa nchini.

Ukiachana na bajeti kuu ya Serikali, Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Fedha 2023-2024 inaonesha kuwa hadi Aprili 2023 Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ilishatoa leseni 8,778 za michezo ya kamari. Hii ni sawa na asilimia 114 ya malengo. Mwaka ujao wa fedha leseni mpya 11,880 zitatolewa.

Ufafanuzi huo unamaanisha kuwa mkazo wa kukuza sekta ya kamari ni mkubwa na wakati huohuo uwekezaji kwa vijana ni mdogo. Maneno ni mengi kuanzia nyumba za ibada hadi kwa wapinzani kwamba vijana wasiwe waraibu wa kamari badala yake wafanye kazi za vipato.

Kamari au michezo ya kubahatisha, kama ilivyo jina lake, inapaswa kuchukuliwa kama michezo ya kujaribu bahati na kujifurahisha. Hivi sasa vijana wengi, tena siku hizi hadi wazee, wamegeuza michezo ya kubahatisha kuwa vyanzo vya mapato.

View attachment 2665539
Vijana wakicheza kamari katika kituo cha kuchezea kamari (Chanzo: Mtandao)

Serikali kwa kutambua hilo inapaswa kuwekeza vizuri kwenye eneo la vijana kwa kuwajengea ujuzi na uwezo waweze kujiajiri au kuajiriwa. Wimbi la vijana kuona michezo ya kubahatisha ni fursa za kimaisha, hadi kuwa mateja wa kamari, ni matokeo ya kukosa machaguo (options) ya kimaisha.

Mzunguko wa kifedha kwenye michezo ya kubahatisha, unashawishi vijana kuuona utajiri wa ghafla bin vuu kwa kucheza kamari. Bajeti inayoombwa kwa ajili ya Wizara ya Madini kwa mwaka ujao wa fedha ni Sh89 bilioni. Maana yake inazidiwa mbali na mapato ya michezo ya kubahatisha.

Rejea matarajio ya mapato ya michezo ya kamari kuwa Sh260 bilioni ifikapo mwaka 2027 halafu pitia fungu la Biashara na Viwanda kuwa Sh324.2 bilioni. Je, huoni dalili za michezo ya kubahatisha kuelekea kushindana na sekta nyeti ya Viwanda na Biashara?

USHAURI
Baada ya uchambuzi kuhusu sekta ya kamari na kuonyesha jinsi inavyochochewa na serikali, naishauri serikali iache mara moja kuharibu watoto (na wazee) wa watu kwa kuwajengea uraibu wa kamari. Badala yake serikali itafute fursa za ajira kwa vijana ili waache kucheza kamari wafanye kazi halali zenye staha zitakazowaingizia kipato halali.

Nafahamu watoto wa watunga sera hawahusiki kwenye uraibu wa kamari. Watoto wa wanasiasa wanakula maisha mazuri huko waliko. Ni watoto wa walalahoi tu ndio wamejikita kwenye kamari. Ipo haja ya kuwaonea huruma wapiga kura hawa kwa kuwa ndio wanaowaingiza madarakani. Nafahamu wanawaacha wapiga kura wapigike ili iwe rahisi kuwatumia kisiasa kupitia umaskii na kupigika kwao lakini yapaswa watambue kwamba Mungu anawaona. Hata kama hawawaogopi wanadamu, basi wamuogope Mungu.

Nawasilisha
Screenshot_20230622-223630_1.jpg

 
Nimeshangaa sana kuona muanzisha uzi ni huyo jamaa, hawa ndio wale wanaingia kwenye hizo issue bila kuwa na cashflow ya uhakika tofauti na kamari, wakipigwa hela miaka nenda rudi ni lazima akili ziwakae sawa kama huyu[emoji23].

tpaul nakupongeza sana kuachana na hizi mambo, ilikuwa ni ngumu sana jobless kusurvive. Sasa utulie ujipate kwanza kiuchumi.
Lazima atarudi tu, amini hilo
 
Itakua kaliwa sana. Lakini Uzi wake una uchambuzi mzuri sana
Wadau hawajanielewa kabisa mkuu. Afadhali wewe umengamua uchambuzi wangu. Tatizo watu wanakimbilia kucomment kabla ya kusoma uzi.
 
Nimeshangaa sana kuona muanzisha uzi ni huyo jamaa, hawa ndio wale wanaingia kwenye hizo issue bila kuwa na cashflow ya uhakika tofauti na kamari, wakipigwa hela miaka nenda rudi ni lazima akili ziwakae sawa kama huyu😂.

tpaul nakupongeza sana kuachana na hizi mambo, ilikuwa ni ngumu sana jobless kusurvive. Sasa utulie ujipate kwanza kiuchumi.
Mkuu nina wasiwasi bado hujaelewa maudhui ya huu uzi. Rudia tena kusoma. Hoja yangu ni zaidi ya hii unayodhania mkuu. Soma kwa utulivu utanielewa.
 
2013 to 2016

Ulikuwa uniambii kitu na hayo mabeting , lakini jambo la kushukuru sanaa 2016 mwishon nilipata mwendo mzuri sanaa na kuacha hayo mambo na kuanza mwanzo mpya aisee kamali sio nzuri wapendwa na kuacha pia sio rahisi kabsa yaani kama addicted wa pombe kumuachisha pombe ndio usawa wa kuacha kamali
 
Back
Top Bottom