Vijana waacheni wabeti na kama Kuna namna nyingine wasaidiwe!
Binafsi sijawahi beti ila na marafiki zangu wengi wanabeti Kila siku wanasuka mikeka kupata na kukosa wanajua wao, hv ndugu mwandishi unataka huyu kijana akafanye nini?
Twende pamoja
Graduates kibao wapo mtaani hawana mifumo rasmi ya kupata hela hapakuchi panakucha siku zinaenda kibishi kila siku mnatangaza fursa ni za kujitolea tu (internship) hapati hata mia
Kwenye kilimo hapagusiki huko kulihudumia ekari moja ni inatakiwa uwe na laki tatu na nusu plus ukivuna seke seke lake inalijua vzr sina haja ya kufafanua
Kila anapopagusa panataka awe na connection/ Mkono mrefu ndo asaidike Sasa atafanya nn si bora abeti tu Kwa mtaji wa buku?
Kwenye biashara hakusogeleki mfano mzuri jaribu wewe binafsi Kodi utakayotajiwa utashangaa ni 60% ya Ile hela uliyonayo utafanyaje? Wale jamaa wa tax assessment wanakatwa na dipi weldi 😒😒
We unashauri vijana wafanyeje? Kuna ambae uliwahi mkuta ana uraibu wa kamari ukajaribu kumsapoti apate kazi yeyote asogeze siku? Kama yupo vipi baada ya kumsapoti aliendelea?