Tanzania limekuwa taifa la wacheza kamari (Tanbet)

Msimu umeishawa hela..tunaangalia hizi friendly matches.

Njoo kwenye bet na akili na hela usije kijinga kijinga.
 
Jifunze kupambana na hali yako wengne wanasema kla mtu ashinde mechi zake wacha wakubet wabet na ww zako peleka unakojua ni pesa zako
 
Jifunze kupambana na hali yako wengne wanasema kla mtu ashinde mechi zake wacha wakubet wabet na ww zako peleka unakojua ni pesa zako
Mimi sijamkataza mtu kubet bali natoa angalizo tu mkuu; hasa pale serikali na vyombo vyake wanaposhadadia mambo ya betting. Inauma sana.

Hata paketi za sigara zimeandikwa UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO lakini bado watu wanavuta. Ni uamuzi binafsi. Everyone does whatever s/he feels at his/her own risk. Ngoja kila mtu ajilipue kwa hasara yake mwenyewe.
 
Watu wanabet roho za watu..
Hakika nchi hii imefika mahali pabaya sana kwenye suala la kamari. Hadi roho za watu zinachezewa kamari. Huku serikali inachezea kamari rasimali za taifa, huku wananchi wachezea kamari roho za watu. Hili ni tatizo kubwa sana.
 

Dar es Salaam. Uraibu wa kamari na michezo ya kubeti, wadaiwa kuwa chanzo cha ugomvi uliosababisha mauaji ya Mwanahamisi Pauline (Mwana Mjeshi).

Inadaiwa kuwa Omary Herman (39) maarufu kwa jina la Komi au Mjeshi, jana Jumatano Juni 28, 2023 alimuuwa mkewe β€˜Mwana Mjeshi’ kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali, na baadaye kujirusha kwenye treni iliyokuwa ikitoke Ubungo kwenda Gerezani, eneo la Ubungo Maziwa na hivyo kupoteza uhai wake.

Jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kusema: β€œTaarifa hizo ni za kweli na yeye amejirusha kwenye treni, lakini tunaendelea kufuatilia kwa karibu, taarifa zaidi nitazitoa,” alisema Muliro.

Hata hivyo siku moja kabla ya kutekeleza tukio la mauaji hayo Komi aliandika jumbe mbili tofauti katika mtandao wa kijamii, wa Facebook zilizosema "Ndiyo imeshatokea na imebaki story" na nyingine "Yale maisha ya furaha yamekwisha sasa yamebaki ya huzuni". Leo Juni 29, 2023; Mwananchi Digital ilifika msibani ambapo ilidaiwa kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu kutokana na kile kilichoelezwa ni malalamiko ya mwanamke huyo kutokana na kitendo cha mumewe kucheza kamari, kubeti kiasi cha kushindwa kuihudumia familia.

Ally Godoro ambaye ni mjomba wa marehemu Mwanahamisi, ameiambia Mwananchi Digital kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi wa ugomvi wa muda mrefu hadi kufikia hatua ya kwenda mkoani Morogoro kwa baba mzazi wa mwanamke kupata suluhisho la mgogoro wao. "Mgogoro huu umekuwa wa muda mrefu na ulikuwa ukipelekwa kwa mzee kwa ajili ya kumaliza matatizo yao lakini haikusaidia hadi kufikia hatua ya kupeana talaka," alisema Godoro.

Naye dereva wa bajaji Imani Omary maarufu (Madega) ambaye alimsaidia marehemu Mwanahamisi kuhamisha vitu vyake siku moja kabla ya tukio la mauaji amesema, aliombwa na marehemu kumpeleka katika chumba kipya alichopanga na kuomba asimwambie mumewe Mjeshi mahali alipopanga.

"Mama Imani (marehemu) aliniomba nimbebee kitanda na godoro na alisema nisimwambie mumewe alipohamia, licha ya kuwa siku ya kuhamisha vitu vyake alisaidiwa na mumewe wake kubeba hadi barabarani," amesema Madega na kuongeza;

"Mwanamke alikuwa analalamika sana kuhusu tabia ya mumewe ya kuvuta bangi, kucheza kamari alimvumilia kwenye bangi lakini kwenye kubeti waligombana sababu pesa zote za mshahara ziliishia kwenye kubeti.”
Kwa upande wa Jeniffer Java, dada wa Komi; amesema taarifa za msiba wa wifi yao walizipata saa 2 asubuhi, na baadaye walienda eneo la tukio na kukuta mwili wake ukiwa chini umelala.

Hata hivyo licha ya kaka yao kutekeleza tukio hilo, waliweka vikao kwa ajili ya kujua namna ambavyo kama familia wangehusika katika msiba huo, na kwamba wakati wakiwa kwenye maandalizi hayo, alipokea taarifa ya msiba wa mdogo wake kuwa amejirusha kwenye treni.

"Majira ya saa 11 jioni tulipigiwa simu na msamaria mwema, kupitia simu ya wifi yetu (mwanamke aliyeuwawa) ambaye alituambia mwenye simu amefariki kwa kujirusha kwenye treni na kufa papo hapo," alisema na kuongeza;
"Tulipofika kwenye eneo la tukio mashuhuda walituambia, alikaa muda mrefu eneo lile na aliziweka simu zake pembeni, ilipokuja treni aliacha kichwa na behewa la kwanza na la pili lipite ndipo alipojirusha kwenye behewa la tatu," alisema Jenifer.

Jenifer ameliambia Mwananchi Digital kuwa: "Komi alikuwa na ugomvi wa mara kwa mara na mkewe, sababu kubwa ni kubeti kwani pesa zote za mshahara zilikuwa zinaishia huko na mkewe hakuweza kuvumilia na kuamua kuomba talaka ili akanzishe maisha yake."

Aidha baada ya kuachana alisema marehemu (Mwanahamisi) alienda kwao Ngerengere, na alivyorudi Dar es Salaam alipanga chumba maeneo ya Gongo la Mboto na baadae kuamua kurudi Manzese kutokana na shughuli zake za ususi kuwa mbali na wateja wake.

"Wifi yetu ni msusi aliona kutoka Gongo la Mboto hadi Manzese ni mbali, alikuwa akitumia nauli nyingi akaamua kupanga jirani na shughuli zake, alivyopata chumba juzi na kuondoka alisaidiwa na mumewe, lakini jana (juzi) alimpigia simu mkewe aende kwake kuna mteja anahitaji kusuka na ndipo kulipotekeleza mauaji hayo," alisema na kuongeza.

Imeelezwa kuwa, wawili hao kabla ya kutengana; waliishi pamoja kwa miaka tisa, na kwamba wameacha watoto wawili Haiman Omary (7) na Abdulaziz Omary (2).

Chanzo: Mwananchi (30/06/2023)
 
Hivi sasa hivi Tanzania kuna makampuni mangapi ya Kamari. Ninajua kuwa kwa Marekani, kamari imedhibitiwa sana; kuna makampuni machache sana ya kamari Marekani na yana mipaka ya wapi yanafanyia shughuli zao ukiachia yale mawili makubwa bahati nasibu ya Mega Millions na Powerball ambayo shughuli zake zinasimamiwa pia na serikali za state husika. Inaonekana kwa Tanzania yeyote mwenye pesa milioni 300 anaweza kuanzisha kampuni ya kamari na kuwakamua watanzania nchi nzima.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£
 
Tunatengeneza taifa la ovyo sana. Miaka michache ijayo watanzania 99% watakuwa waraibu wa kamari na mateja wa kubet wa kutupwa!
 
Kama watawala wanafurahia mavuno kwa njia ya kodi bila kufikilia impact inayotokea kwa vijana unategemea nin., maana kuna nguvu kazi kubwa sana inapotea kwa ujinga wa betting.
 
KAMARI ILIVYOMUUA MWANAFUNZI

Mwanafunzi wa kidato cha nne, shule ya Sekondari Nkomolo, Nkasi mkoani Rukwa, Fredy Pupa (19) ameuawa kwa kuchomwa kisu wakati akicheza kamari baada ya kudhulumiana fedha na mwenzake.

Mkuu wa wilaya ya Nkasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 29 majira ya saa 11 jioni wakati mwanafunzi huyo akiwa na kijana mwenzake, Samwel Nkoswe (20) wakicheza kamari.

Amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo, alikuwa ameacha shule na alikuwa anaishi mtaani huku akijihusisha na vitendo vya kinyume na sheria kikiwepo cha kucheza kamari.

Imeelezwa kuwa wakiwa wanacheza mchezo huo, mtuhumiwa alikula hela za marehemu lakini alikataa kumpa pesa hizo na kuamua kutoa kisu alichokuwa nacho mfukoni na kumchoma Pupa ubavuni karibu na tumboni.

Baada ya kujeruhiwa mwanafunzi huyo alivuja damu nyingi kitendo kilichompelekea kupoteza maisha muda mfupi baadaye.

Baada ya kuona amefanya tukio hilo, mtuhumiwa alikimbia na kwenda kujificha kwenye mashamba yaliyopo kijijini hapo lakini wananchi walimsaka mpaka kumkamata na kisha kuanza kumshambulia, hadi sasa yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa nduguzake kwaajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi hospitali.
 
Kama watawala wanafurahia mavuno kwa njia ya kodi bila kufikilia impact inayotokea kwa vijana unategemea nin., maana kuna nguvu kazi kubwa sana inapotea kwa ujinga wa betting.
Hata hii serikali bora tuibetia kwa waarabu tukiliwa tuliwe tu. Nchi imekuwa ya kipumbavu sana hii.
 
Tbc a media state wakihimiza cheza pesa. Sijui madam boss ten sijui djaro arungu.. n.k. for sure tupo kwenye vicious cycle [emoji22]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…