Tanzania magari yaliyotumika nchini yanauzwa bei kubwa kulinganisha na iliyotumika nje

Kukosa pesa mkuu. Mwajiriwa kapewa na ofisi m7 mkopo anataka anunue gari na chenji ibaki.
Ni sawa hali zetu tunazifahamu lakini kabla hajachukua huo mkopo kwanini asidundulize kwanza hicho kiasi kilichobaki cha milioni 3 halafu ndo achukuwe mkopo wa milioni 7, sababu akinunua hiyo gari kwa mtu kwa milioni 7 au chini ya milioni 7 atajiingiza katika ulipaji wa mkopo mara mbili. Gari ya kununua kwa mtu nyingi ni pasua kichwa ingawa sio zote, tena uzuri wa hawa SBT au beforward haulipi pesa yote mpaka pindi gari yako itakapofika Bandarini ndo unaenda kumalizia gharama za ushuru ila cha kwanza utakamilisha taratibu za CIF tu, gharama za ushuru unalipa gari ikishaingia nchini.
 
Kweli mkuu
 
Gari ndogo ndogo resale value ipo juu maana zina soko na watu wanazitafuta sana sababu hazili mafuta. Gari kama Brevis, mark x watu wanaziogopa maana zinakula mafuta na matengenezo yapo juu so sokoni demand sio kubwa na bei zipo chini. Mark x unanunua 15M au zaidi kuuza around 7
 
Okey mkuu. Nimekuelewa.
 
GARI YA KUNUNUA KWA MTU KWA HAPA KWETU TANZANIA NI MAJANGA TU JAMAA YANGU KWANZA UTAPIGWA BEI, PILI UIMARA WA HICHO CHOMBO BADO HUKO MASHAKANI, SIWEZI MSHAURI MTU ANUNUE GARI KWA MTU LABDA KAMA UNAUZIWA NA NDUGU AU JAMAA WA KARIBU, LKN WALIOBAKI HAWEZI KUKWAMBIA UKWELI KWANINI ANAUZA HIYO GARI.
 
SA SI UAGIZE NA WEWE???
 
Jazba.....
Niliuliza ili nipate majibu na nimeyapata kuwa si magari ya aina zote ni baadhi tu kama ist, runx na raum ndo yapo juu sababu ya demand.
Kwa bei hiyo umeambiwa yapo?? we unataka kulinganisha ni ya ng'ambo?
 
Wanaoharibu hizi biashara ni madalali mkuu wapuuzi sana wanataka piga cha juu kikubwa kuzidi hata muuzaji.....
 
Na wauzaji wa magari mapya yaliyotumika nje, si wanapata changamoto sana kushindana na bei hizi za magari yaliyotumika hapa?
Hakuna Changamoto hapo...ndiyo wanafaidi zaidi, maana wengi watataka kununu ya nje. Isije ikawa wao ndiyo wanafanya magari yaliyotumika ndani yawe ya bei juu!? Ili wao waendelee kuangiza...( Maelezo yangu haya yanategemea kama nimemuelewa sawasawa mleta mada!)
 
Hizo gari zenye cc ndogo zinagombaniwa mno kutokana na ubahili wa kuweka mafuta, chanzo kikubwa ni ubahili wa mafuta, kaulizie gari yenye CC 3000, hata kama ina mwaka tu, unapata kwa hiyo 6.5m
 
Mimi nadhani waongeze ushuru mara mara 10 zaidi, halafu watoe msamaha wa kodi wa miaka mi5 kwa waunganishaji magari (assembly plant) watakaotaka kuja kuanzisha kiwanda, tukiona bado hawataki kuja tunaongeza tena mara 2 yake, hivyo hivyo, hadi kieleweke, tukishapatavile technology transfer, tunaunda wenyewe
 
Hio assembly plant watuuzie bei zilezile kama tununuavyo mtumba. Kuwe na gari za 10M to 15M vinginevyo kiwanda kitakuwa useless.

Kama itashindikana watuachie mfumo huu huu wa kununua gari chakavu zilizo katik kiwango kinachokbalika
 
Hizo gari zenye cc ndogo zinagombaniwa mno kutokana na ubahili wa kuweka mafuta, chanzo kikubwa ni ubahili wa mafuta, kaulizie gari yenye CC 3000, hata kama ina mwaka tu, unapata kwa hiyo 6.5m
Lazma iwe hivyo maana kinachopendwa sokoni ndo chenye thamani siku zote iko hivyo.

Na ndio maana ni rahisi mtu kulanguliwa kwenye uuzaji wa toyota IST kuliko kwenye gari kama Crown,Brevis au Mark X. Dalali anatoa bei ya kuropoka gari ikiwa IST number D hata kama ni gari ya 2015 utalabuliwa 8.5M wakati thamani ya gari hio hio kwa kuagiza ni 10.5M! Kimsingi kwa miaka iliotumika hio gari ilipaswa iuzwe hata 4.5M ila tatizo ni nguvu ya soko.
 
Hizo gari zenye cc ndogo zinagombaniwa mno kutokana na ubahili wa kuweka mafuta, chanzo kikubwa ni ubahili wa mafuta, kaulizie gari yenye CC 3000, hata kama ina mwaka tu, unapata kwa hiyo 6.5m
Mkuu upo sahihi sana, mfano x Nissan Xtray No D unaipata kwa mpaka M 6 mkononi, au Bravis, lakin gari zenye kutakiwa na watu wengi ni low fuel consumption ambazo na bei sasa ibakuwa juu, mfano IST,Allex, Suzuk Jimmy nk
 
Binafsi nilitaka kununua Altezza lakini bei ilikua kuanzia m7.5 na kuendelea wengine wanaweka m8.8..nikaona wakati unakuta Altezza ya 1998-1999 ushuru wake ni m3.97 za 2000-2001 ni 4.2m-4.45 nikaona isiwe tabu ngoja nivute mwenyewe
 
Nimeelewa sana tu. Hii biashara ni nzuri maana gari haliozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…