Tanzania Mbioni Kununua Umeme Kutoka Ethiopia

Tuna change kutoka kuuza na kwenda kununua
 
Kwahiyo Ethiopia watatuuzia Nini kama Kila mtu ana umeme?! Au mmeshiwa na uongo Hadi mnaanza kujichanganya. Ndio maana ccm inaeleweka zaidi na wajinga.
Majirani kama Ethiopia na Uganda Wana umeme mwingi.
 
Bi tozo hata maji tu ameshindwa ku supply.

Yani hata mabomba ambayo alikuta mwenzake ameshayaweka ameshindwa kufanya yatoe maji.

Huku Pugu sisi tuna mabomba tu ya siyo na maji.

Taka tupu
 
CHAMA CHA MAFISADI (CCM)
 
Hii ni habari njema. Hongera Naibu Waziri Mkuu cum waziri mpya wa nishati. Harakisha kuleta huo umeme toka Ethiopia na kumaliza hili janga la kitaifa la mgao mkali wa umeme lililolikumba taifa letu.

Umeme huo wa Ethiopia ni wa bei nafuu sana, 6.5 usd cents per unit ukilinganisha na huu wa Songas wanaotuuzia 15.5 usd per unit. Tuachane na huo umeme Songas unaozalishwa hapo Kinyerezi unless nao wateremshe bei hadi 6.0 usd cents wakati tunasubiri umeme wetu wa bwawa la Nyerere utakaokuwa wa bei ya 3.0 usd cents per unit. Huo umeme wa Songas uuzwe nje hususani Zambia. Akina Makamba na Maharage walikuwa wamepanga kuuuza ule umeme wa bwawa la Nyerere Zambia na sisi kubaki na huu wa Songas wa bei kubwa.

Tumekuwa tuna export to Kenya mahindi na mchele wetu halafu tuna import mahindi na mchele toka Zambia na kwingineko kwa matumizi yetu ya ndani. Hii ni Bashe philosophy. Kwa philosophy hiyo hiyo tutakuwa tuna import umeme toka Ethiopia na tuna export umeme kwenda Zambia na kwingineko.
 
Ndio utajua Tanzania ni comedian,maana nchi imezungukwa na maziwa makuu,mito,maporomoko kila Kona ila umeme utanunuliwa toka Kushi.
Issue siyo wingi wa maziwa na mito, issue ni flow ya kutosha ya maji pamoja na height drop (how far the water falls) ili pessure ya maji iweze kuzungusha turbines za kuzalisha umeme.
Ndiyo maana huwezi kukuta hydrostations kule Ziwa Victoria.
 

Yale mambo yetu ya kuuza umeme nje yamekuwa je tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…