Umenena vema sana
JF palikuwa ni mahali patakatifu kwa kubishana, kukosoana, kuangana mkono kwa hoja. Bahati mbaya, siku zilivyokwenda, waliingia wengi ambao nadhani hawana uwezo wa kujenga hoja au wana uwezo lakini wanafurahia kujitoa ufahamu. Wanachoweza ni kutukana kwa sababu hicho ndicho kilicho rahisi sana kwa mtu ambaye upeo wake na uwezo wake wa kufikiri, ni mdogo. Kutukana, hata mwendawazimu anaweza, lakini hawezi kujenga hoja.
Kuna watu humu, tangu wajiunge, hawajawahi kuleta hoja ya maana wala kutoa mchango wenye hoja. Wao ni kutukana, kukejeli au kuleta mipasho.
Maovu yanayotendwa na watawala na mifumo yetu mibovu, haitawaathiri watu fulani tu, wajue itawaathiri watu wote wa sasa na hata wa vizazi vijavyo.
Magufuli alipoanza kutumia mamlaka yake ya Urais yasiyo na mipaka, hata familia Kikwete na familia yake, Kinana, Makamba, Membe, Lowasa, Sumaye na vigogo wengine wengi waliumizwa hasa mioyoni mwao. Lakini wakiwa kwenye madaraka, waliamini kuwa ubaya wa katiba unagusa kundi fulani tu. Na hata Samia, anaweza kuona hakuna umuhimu wa katiba mpya kwa sababu hii ya sasa inampa uhuru wa kuwa dikteta, asichokijua uhuru huo wa Rais kuwa dikteta, siku moja unaweza kutendeka dhidi yake, wanawe au wajukuu zake.
Jamii Forum, ilistahili pawe mahali pa hoja nzito, siyo majali pa kuleta ushabiki.