Tanzania Military Intelligence vs TISS

Status
Not open for further replies.

Ni kweli jeshini kuna mfumo mzuri sana hasa kwenye check and balance, lakini kwa mfano any senior general akiamua kukinukisha kazi inakuwa siyo ngumu sana ukilinganisha na vyombo vingine usalama.
Sababu ni kwamba hawa maofisa wa juu wote ili uwe general kuna vitu wanasoma/somea (naomba nisivitaje kwasababu za kiusalama) vinavyowapa nguvu ya kufanya chochote watakacho hata kama watapata upinzani kwa wengine.
Ila kwa mfumo wa nchi yetu generals wote wamekuwa trained kuwa wazalendo wa hali ya juu, ndo maana hata mafao yao ni tofauti na watumishi wengine wa uma. Wanaendelewa kutunzwa, kulindwa na hata kuombwa ushauri wa jambo lolote wanapostaafu mpaka wafe. Kwa mfumo huu na mwingine ambao siwezi kuutaja hapa ni wazi nchi yetu ni salama na si rahisi huenda ikachukua miaka mingi sana jeshi letu kuja kuasi.
Kwa kifupi kama kuna chombo cha usalama nchi hii ambacho kina uzalendo wa hali ya juu ni jeshi, ndo maana mi nilikuwa ni mmoja wa watu niliyenshangaaa sana rais na amiri jeshi mkuu ndugu JK kusema Jeshi litapindua nchi kama serikali tatu zitapita.
 
mkuu toa facts ni uzalendo upi walio nao TISS kuhusu viongozi wanaoliangamiza taifa..

Mkuu watu wa usalama I mean TISS and MI hufundishwa uzalendo wa hali ya juu kuhusu nchi yao na wamebeba siri kubwa za nchi na kuna mambo n ya siri hayawez kusemwa hapa ,ila kiuhalsia wao hufanya kaz zao kutokana na weledi juu ya taifa lao, na unapoona tukio lolote la kihalifu au uhujumu uchumi taarifa zinakuwa tayari zishafka mahala husika ,sema viongoz ndio u delay kuchukua maamuzi hvyo kuonekna kuwa wao ndio wanapwaya la hasha,
E.g n ishu ya Richmond taarfa juu ya mipango haramu iliyokuwa inafanyka juu ya huo ufisadi taarfa zilifka mapema na tena zilifkishwa na tiss senior na ndio Raman nzima ilijulikna japo kuna mambo n confidential,pia kumbuka ishu ya kusafrisha madawa ya kulevya kupitia maiti ktoka Zambia ikaja kamatwa ikikarbia iringa
So TISS wako vizuri mkuu ila ishu n uadilifu wa viiongoz kuchukua maamuz ya kudhibiti ,kwani wao kaz yao ya usalama na udukuz hufanyika kwa wakati
 
Unajua kazi ya kikundi cha FFU?

Ninavyo elewa mimi ni hii ya kutuliza ghasia kama tunavyo waona wakifanya kwenye maandamono yasiyo fuata sheria. Lingine ni ulinzi wa viongozi kama tunavyo waona kwenye misafara ya viongozi na majumbani mwao.
 
Ninavyo elewa mimi ni hii ya kutuliza ghasia kama tunavyo waona wakifanya kwenye maandamono yasiyo fuata sheria. Lingine ni ulinzi wa viongozi kama tunavyo waona kwenye misafara ya viongozi na majumbani mwao.

Dhima kubwa ya wao kukaa lindo ni kwa sababu wanamafunzo ya hali ya juu kukabiliana na ghasia..iwe kwenye ziara, msafara au nyumbani kwa kiongozi...ndiomaana unawaona wapo kwenye msafara wa Rais pia.

Uwepo wa MP kutoka JWTZ kwenye msafara wa Rais wakati hayupo kwenye eneo la kambi ya jeshi ni ishara kua eneo husika sio salama sana...hapo ndio utawaona wanajeshi wenye mafunzo ya kutosha kulinda viongozi wa ngazi za juu wanakuwepo ulingoni..

**Kwa mtazamo wangu tuu....:A S wink:
 

Mkuu mara nyingi issue hii huwa tunazungumza hapa lakini kama ulivyosema kutokana na sababu za kiusalama hay=uwezi kusema yote.

Kwenye suala la katiba ajabu ni kuwa TISS haikuzungumzwa kabisa kwa sababu ambazo hazijulikani. Ujinga na upungufu kwenye usalama Tanzania hautokani na udahifu wa TISS, bali unatokana na muundo tulio nao wa kufanya maamuzi. Kama kukiwa na njia nzuri ya kuwafanya jamaa wafanye maamuzi na kuchukua kwa muji bu wa Inteligence nadhani tusingekuwa na ujinga unaofanyika leo.

Kwa mfano leo tukiwaomba TISS watuambie hadharani wanajua nini na walijua lini kuhusu ESCROW, Richmond, EPA etc etc etc na walichukua hatua gani na kwanini, kilio kitarudi kule kule kwenye katiba. Labda wanasiasa wengi ambao walitakiwa kufanya maamuzi kutokana na taarifa walizopoewa, leo tutakiwa tunajiuliza kwanini bado wako madarakani.
 

Harnessed!!!!!
 

Gudi gudi! Kwa hiyo kwa mtazamo wako tu maeneo uliyo taja kuwa ffu huonekana ya na dalili kubwa za kutokea ghasia sio?

Pia mp wataonekana katika maeneo ambayo si salama sana. Sasa na shindwa kuelewa kwa nini ghasia zionekane kupewa uzito zaidi ingawa hatuoni lile gari la washwasha kwenye msafara sana sana unaweza kuona gari la wagonjwa.
 
Mko sawa wadau lakini bila kugusa taarifa za ndani kabisa ya hizi taasisi muhimu katika taifa letu. Jambo ambalo linahitajika kufahamika kwa wananchi ni kuhusu tasnia ya uzalendo ktk taasisi hizi juu ya utaifa, nikimaanisha tulipotoka na tunapoelekea ktk nyanja za siasa, uchumi, ulinzi na teknolojia. Na ni hatua gani wanachukua pale mashauri yao yanapochelewa au kutofanyiwa kazi kabisa..??
 
Hivi kuna tofauti gan kati ya Jasusi na Shushushu?
 
Hivi kuna tofauti gan kati ya Jasusi na Shushushu?

Ndio tofauti ipo. Jasusi ni shushushu lakini shushushu sio lazima awe jasusi.
Jasusi ni shushushu/mpelelezi au agent anayekusanya taarifa za siri nje ya nchi yake na kuziwasilisha kwa serikali yake. Mf. Jasusi wa ki-tz anaweza kwenda kukusanya taarifa kenya, uganda nk na kuiletea serikali; Hivyo unaposikia ujasusi ni ushushushu/upelelezi wa kimataifa/nje ya nchi tu na auhusuani na masuala ya upelelezi wa ndani.
 
asante mkuu@The Intelligent nin swal lingine hapo,vp mafunzo yao kat ya TISS na IM kwa maana mafunzo yao ni ya aina moja au kuna tofauti katika mafunzo yao ya ukusanyaji taarif mbalimbali?
 
asante mkuu@The Intelligent nin swal lingine hapo,vp mafunzo yao kat ya TISS na IM kwa maana mafunzo yao ni ya aina moja au kuna tofauti katika mafunzo yao ya ukusanyaji taarif mbalimbali?

MI inahusika na ujasusi wa kijeshi tu/masuala yanayohusiana nayo wakati TISS ina-deal na masuala ya kijamii, siasa na uchumi hivyo TISS inaweza kufanya udukuzi hata kwenye masuala ya kijeshi ila sio kwa kiwango cha kuifikia MI hivyo inategemewa kuwa na tofauti lakini shabaha yao ni moja.
 
dah!hil ni zaid somo mkuu@The Intelligent, ina maana kwa baadhi ya taarif zao hua zinaingiliankw kutegemean na mambo husika ya ndan ya nchi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…