Dogo Tundu
JF-Expert Member
- May 25, 2009
- 448
- 189
oooh safi sana. Sasa Mwamnyange anaweza vipi kukinukisha wakati inaonyesha masuala ya kiusalama jeshini yana check and balance katika muondo na mfumo wake ya hali ya juu. Inaonyesha kabisa kuna mageneral wakubwa wajeshi ambao wanaweza wasimtii kama sio amri halali, kufanya uhaini kwa mfano.
Ni kweli jeshini kuna mfumo mzuri sana hasa kwenye check and balance, lakini kwa mfano any senior general akiamua kukinukisha kazi inakuwa siyo ngumu sana ukilinganisha na vyombo vingine usalama.
Sababu ni kwamba hawa maofisa wa juu wote ili uwe general kuna vitu wanasoma/somea (naomba nisivitaje kwasababu za kiusalama) vinavyowapa nguvu ya kufanya chochote watakacho hata kama watapata upinzani kwa wengine.
Ila kwa mfumo wa nchi yetu generals wote wamekuwa trained kuwa wazalendo wa hali ya juu, ndo maana hata mafao yao ni tofauti na watumishi wengine wa uma. Wanaendelewa kutunzwa, kulindwa na hata kuombwa ushauri wa jambo lolote wanapostaafu mpaka wafe. Kwa mfumo huu na mwingine ambao siwezi kuutaja hapa ni wazi nchi yetu ni salama na si rahisi huenda ikachukua miaka mingi sana jeshi letu kuja kuasi.
Kwa kifupi kama kuna chombo cha usalama nchi hii ambacho kina uzalendo wa hali ya juu ni jeshi, ndo maana mi nilikuwa ni mmoja wa watu niliyenshangaaa sana rais na amiri jeshi mkuu ndugu JK kusema Jeshi litapindua nchi kama serikali tatu zitapita.