Tanzania, mmedhibiti mijadala kwenye radio na Televishen, wanaharakati na wapinzani wamehamia space na zoom mmewafuata kuomba mic; It's Shame

Tanzania, mmedhibiti mijadala kwenye radio na Televishen, wanaharakati na wapinzani wamehamia space na zoom mmewafuata kuomba mic; It's Shame

Tatizo lipo wapi? Kuna mtu ameshikiwa mtutu kwenda upande wowote? Mnapigania uhuru lakini mnataka uhuru uwe upande mmoja tu. Kama wao wanafanya mijadala yao na wanapata watu wachache, nyie mnaopata watu wengi (hadi kutoka KENYA[emoji4]) mnapata hofu ya nini? Serikali iache kuongea na wananchi kisa kwa kufanya hivyo inaingilia uhuru wa "wanaharakati"? [emoji849]
Ovyo kabisa...jambo hili dogo tu umeshindwa kuelewa,?kweli?
 
Serikali na chama tawala wamedhibiti watu kusema na kujadiliana kwenye TV na Radio Kwa manufaa ya afya ya akili ya Watanzania. Wakafungia magazeti na baadhi ya online tv. Wakatunga sheria Kali na kuajiri TCRA wapambane na wakosoaji wa serikali.

Kwa kuwa wanaozuiwa kusema ni wale wenye akili timamu, wametafuta mbinu mpya ya kujadiliana bila kuvunja sheria ; wameanzisha club house, space na other online meetings. Kwa roho zetu mbaya tukaamua kuwazimia internet wakahamia kwenye VPN somehow expensive but walijua bure ni ghali. Baada ya mbinu zenu kukwama na tv kukosa mvuto mkanuna.

Kipindi mmenuna mkasikia Maria Sarungi space Ina host thousands of people world wide, mkasikia space ni zaidi ya mkutano wa siasa. Wapinzani na wanaharakati wakanunua Uhuru wao kwa mlango wa nyuma msioweza kudhibiti, wakaanza kuimarika na Sasa wameimarika mara dufu.

What's next, badala mdai Uhuru wa vyombo vya habari mkarudi kwao kuwaomba mjiunge nao. Mkawa observers lakini kwa kuwa mnakerwa na ububu mliojipa mkaamua liwalo na liwe Bora mfukuzwe chama lakini mseme. Sasa hivi mnang'ang'ania kupewa Mic na msipopewa mnalalamika space IPO biased. Kwa kuwa wanaondesha midahalo Wana hekima n wamesoma wakaeleimika wamekuwa wakiwapa mic na kuwafundisha hata namna ya kutumia technology mpya. Shukuruni.

Leo hii ambapo Kuna radio na Televishen nimeshtushwa kusikia hata miadala ya serikali kuhusu rasimali na see mbalimbali mmeipeleka space, zoom nk Je mnaona ubaya Gani kufungulia radio na Televishen I Hadi mkaongelee space ambapo Kuna kundi ya walioelimika TU? Mtawafikiaje wanyonge? Mmepeleka umeme wa REA then mkazima maoni, wanNchi wananufaikaje na habari?

Jaribuni kufikiri ni namna Gani mmekosa Uhuru wa Habari na kutoa maoni kwa makatazo yenu yasiyo n tija. Jiulizeni Kati yenu na wao Nani analoose? Wameanza kujirekodi na kusambaza kupitia WhatsApp so wananchi wanapata one side info ambazo nivigumu kwenu CCM na serikali kuzidisprove coz mijadaala kwenye TV mnakuwa wenyewe. Tafute
Eti radio one kila saa ni kurusha nukuu ya rais! Nimewahama kabisa sina mda wa kusikiliza utumbo
 
We nae kule twitter unapiga block watu hovyo hovyo tu huo uhuru unaozungumzia ww mbona huanzi nao shame on you.
Kanichapa block kitambo 😂😂, jasusi my foot!!!

Screenshot_20211219-093512.png
 
Tofauti nyingine Kati yao ni kwamba Chahali kajificha Scotland kaikimbia Tz
Kwenda kuishi nje ya nchi haimaanishi kukimbia and kujificha! And angekuwa amejificha kama usemavyo then usingejua yupo nchi gani
 
Jasusi aliyezulumiwa na kinana hela za kumpigia kampeni Magu 2015 mitandaoni 😁😁😁😁😁😁
Kudhulumiwa jambo la kawaida kwenye kutafuta riziki, may be Chief hujawahi kudhulumiwa maisha yako yote, Hongera
 
Naomba nisimjibu Chahali Kwa sababu Sina uhakika kama yeye ndiye aliyeandika hiyo post au kaandikiwa. Badala ya kumjibu napenda kumwomba atusaidie kwanini space Kenya haina nguvu kama Tanzania? Kenya Kuna Uhuru wa vyombo vya habari hasa tv na radio na hivyo hakuna mtu anatamani kuwekeza kuongelea gizani wakati akiongelea nuruni anasikika.
Msingi wa hoja yangu upo hapo, kwanini Waziri azime Uhuru wa maoni kwenye tv au asisitize sensorship then waziri huyo huyo atamani kupewa MIC kwenye space ambapo anazungumza na watu walewale isipokuwa Kwa kijificha wapiga kura wake kijijini wasimsikie? Kama wanaamini maudhui ya TV zetu yanakidhi kwanini wasiwekeze kuongelea kwenye TV?

Yupo kiumbe kasema namkosoa Mama, napenda kumjulisha kwamba huyu ni mwanamke mwenzangu na natamani kuona anafanya vyema Ili wanawake wengi zaidi wapate Nafasi ya kuibadilisha Dunia kutoka mfumo Dume. Njia moja Wapo yakumfanya afanye vizuri nikurise issues ambazo zitamfanya apate mitazamo hasi na chanya kuboresha utawala wake.
JPM alikosea sana kukubali kusikia upande mmoja wa shilingi , alikosea kuamini watu aliowateua wanamsaidia kumbe walikuwa wanajisaidia. Hawajawahi kumpenda wala kupenda afanikiwe, naamini baada ya kuondoka kwake mliwaona walivyotoka adharani kumdhalilisha Kam vile awakuwahi kufanya- KAZI naye.

Kiuongozi anayetaka kwenda mbele ni yule anayesikiliza sana wabaya wake kuliko watu wake wa karibu. Kumbuka wabaya wa Mama watasema ukweli wakati wote kutokana na kuambiwa na Wazuri wa mama.

Nchi hii vyombo vya habari serious kama star tv na itv vimekufa nakuzaliwa clouds na wasafi ambazo misingi yake ni buruduni. Taifa linaburudika alijadili
 
Tatizo lipo wapi? Kuna mtu ameshikiwa mtutu kwenda upande wowote? Mnapigania uhuru lakini mnataka uhuru uwe upande mmoja tu. Kama wao wanafanya mijadala yao na wanapata watu wachache, nyie mnaopata watu wengi (hadi kutoka KENYA[emoji4]) mnapata hofu ya nini? Serikali iache kuongea na wananchi kisa kwa kufanya hivyo inaingilia uhuru wa "wanaharakati"? [emoji849]
Wakukurupuka
 
Tatizo lipo wapi? Kuna mtu ameshikiwa mtutu kwenda upande wowote? Mnapigania uhuru lakini mnataka uhuru uwe upande mmoja tu. Kama wao wanafanya mijadala yao na wanapata watu wachache, nyie mnaopata watu wengi (hadi kutoka KENYA😊) mnapata hofu ya nini? Serikali iache kuongea na wananchi kisa kwa kufanya hivyo inaingilia uhuru wa "wanaharakati"? 🙄
Usharudi kitengoni mkuu!?
 
Hivi upinzani mnahoja gani mpya mnayoweza kumshinda mtu?
Hoja za kuiga kwa wazungu pasipo kuangalia mahitaji yaki ni yapi?
Wakiwaiga wewe shida yako nini!? Na wewe kaige kwa wengine wasio wazungu.
 
Back
Top Bottom