Deadline ya returns ni tarehe 20 ya kila mwezi, shida sio kutuma returns tu Bali baad ya returns kutuma Kodi ikitoka pesa ya kulipa Kodi hiyo unayo? Mfano watu wa kampuni wana supply, terms of payment may be 2 months or 3 months after delivery, Leo nime uza labda tarehe 6 ya mwezi na nime print receipt, uki print efd receipt Ina soma kwenye system ya TRA kuwa huyu mtu kauza na Kuna Kodi yetu hapo, mwezi unao fuata unafanya returns, baadae TRA wana control number ulipe Kodi Yao, wewe hujalipwa na kukusanya hiyo pesa utalipaje hiyo Kodi?
Case nyingine, labda una fanya biashara na taasisi za serikali mfano janga kubwa liko Temesa, una waletea spares na una print receipt umeuza hivyo tena wana kuambia malipo ni haraka sana lakini unaenda zaidi ya miezi sita zero zero , wewe una fanya returns na control number una tumiwa na TRA hizo Kodi utazilipa vipi? Ndo maana nikasema yawape mawasiliano mazuri kati ya TRA na wafanya biashara, TRA ijue nature za biashara na isikilize wafanya biashara, biashara ni ngumu , kina chotakiwa ni uelewa wa pande mbili na kulipa Kodi pole pole kadri pesa zinavyo ingia , Niki kuambia print control number amount 2M print kiasi hicho achana na issue ya wewe tuna kudai mil50 mbona una lipa mil2? Mimi ndo najua nature ya biashara na mwishowe deni litalipwa na kuisha.