Tanzania mwenyeji mkutano mkubwa wa Kilimo Afrika, Rais Samia kuuzindua Ijumaa

Tanzania mwenyeji mkutano mkubwa wa Kilimo Afrika, Rais Samia kuuzindua Ijumaa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Bwanku M Bwanku.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Afrika wa masuala ya chakula na kilimo utakaofanyika Septemba 5 mpaka 8 mwaka huu.

Ijumaa wiki hii (Machi 17), Rais Samia Suluhu Hassan atazindua maandalizi ya mkutano huo Ikulu, Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Zuhura Yunus.

Mkutano wa Afrika wa chakula wa Septemba unatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani 3,000 kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika na duniani, ikiwemo marais, mawaziri na wakuu wa taasisi za kimataifa.

Mkutano huo utaweka msisitizo kwenye Vijana na Wanawake kama Msingi wa Mfumo Endelevu wa Chakula.

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na hatua kubwa za kimageuzi ambazo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imezichukua tangu alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Hatua hizo ni pamoja na kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mara nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu tupate uhuru.

Serikali ya Rais Samia pia imetambuliwa kwa mradi wake wa ubunifu wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), ambao unalenga kuwawezesha vijana, ambao ndiyo nguvu kazi kubwa nchini, kuingia katika kilimo.

Serikali yake pia imewekeza kwenye miundombinu ya umwagiliaji, huduma za ugani, pembejeo na ruzuku ya mbolea na mbegu kwa viwango ambavyo havijawahi kufanyika miaka ya nyuma.

Serikali ya Rais Samia pia imekuwa ikitekeleza mpango wa kilimo unaojulikana kama Ajenda 10/30 yenye lengo la kufanya kilimo kiwe cha biashara na kikue kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka ifikapo 2030.

IMG-20230315-WA0000.jpg

IMG-20230315-WA0001.jpg

IMG-20230315-WA0003.jpg

IMG-20230315-WA0002.jpg

IMG-20230315-WA0004.jpg
 
Hii mikutano mikubwa isiwe kama kutufanya kama taifa picha isiyo na somo.

Nilidhani hapo kabla tutumie ardhi yetu vizuri kutokana na ukubwa wake kufanya kilimo cha kisasa ambacho akisubiri hadi mvua inye.

Teknolojia imefika mbali ambapo hao tunaojifunza kwao wanalima mwaka mzima pasi kumsubiri Mwenyaazi Mungu ashushe maji.

But kuna kilichozinduliwa majuzi huko dodoma, kiwe kilimo kweli na tufikie lengo ndipo na huu mkutano utakuwa na uhalisia yakinifu.


Note; Kwa sasa siwezi kutoa sifa wakati ardhi inatoa machozi kwa kutokutumika, toka iumbwe!.
 
Mbona kama nimeshauona huu mkutano wakati namfuatilia mrembo Zuhura Yunus?
 
Back
Top Bottom