Tanzania na Burundi haziko miongoni mwa nchi zitakazopewa chanjo ya corona

Bro unaonata tunashindwa stiki na miswaki sembuse chanjo vitu vingine tuwa achie mabeberu tu
Utaona naota tu ukiwa umelala.

Sasa mimi sijalala ndio maana najaribu kuwaamsha wote waliolala.
 
WHO ni wahuni tu kwa mujibu wa trump!
Trump alikuwa mjinga kama wajinga wetu lakini Wamarekani wenye akili wamemtupilia mbali sasa anahaha na WHO wamerudi kwenye nafasi yao ya kuwahudumia wanachama wao Wamarekani. Chanjo WHO iliyofanikiwa kupata kwa wanachama wake wa Afrika ni kidogo sana kutosheleza nchi zote kwa hiyo wanachama wajinga wakijitokeza kuzikataa, kuna nchi wanachama za wenye akili zitanufaika na ujinga huo. Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi!
 
Hamto safiri kokote duniani bila cheti cha chanjo.
JPM mwenyewe hasafiri, we ukitaka kachomwe ili uweze kusafiri.
33828D6C-8F2E-434F-BCBF-9A3301DBADCF.jpeg
 
Waende zao sie hatutaki masindano yao, tuna nyungu+ nimri hapa nisha piga kikombe cha tangawizi na malimao sindano ya nini.
 
Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza mpango wa muda kuhusu jinsi nchi zitakavyopewa chanjo za corona mwaka huu, huku Tanzania na Burundi zikiwa hazimo.

WHO imesema kuwa chanjo hizo ambazo ni dozi milioni 336 za AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa muhula wa kwanza na wa pili wa mwaka 2021.

Katika awamu hii, nchi zitapewa kwa sawa na 3.3% ya watu katika kila nchi katika mpango huu, kulingana na malengo ya shirikisho la chanjo duniani (GAVI) ya utoaji wa chanjo kwa 3% ya wakazi wa dunia katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2021.

Wiki iliyopita Rais John Pombe Magufuli aliwatahadharisha viongozi kutopokea chanjo za corona ambazo alisema zinaweza kusleta athari kwa raia.
Baada ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Covid,hivi karibuni serikali ya Burundi militangaza mkakati mpya wa kupambana na Covid-19, ikiwa ni pamoja na kufunga mipaka ya maji na nchi kavu na uvaaji wa barakoa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Katika orodha ya awali kuhusu mpangilio wa nchi zitakazopata chanjo katika eneo la Afrika Mshariki Tanzania na Burundi hazimo.

Nchi nyingine za Afrika ambazo hazimo katika orodha ya upokeaji wa chanjo ni pamoja na, Equatorial Guinea, Eritrea, Gabon, Lesotho, Madagascar na Ushelisheli

Shirika hilo la afya duniani linasema kuwa nchi ambazo hazimo katika orodha yake ya kupewa chanjo ya corona ni kwasababu "zilijinunulia chanjo zake zenyewe, hazikuomba chanjo, au hazijawekwa bado katika orodha ya nchi zitakazopewa chanjo ".

Kulingana na orodha hiyo ya WHO za kanda hii ya Afrika Mashariki na Kati zitapewa dozi kama ifuatavyo:

DR Congo: 6,948,000
Kenya: 4,176,000
Rwanda: 1,098,960
Sudan Kusini: 864,000
Uganda: 3,552,000
 
Kwan WHO ni kina nani?? Hawa si ni genge la wahuni flan wenye ku moderate kila uhalifu wa kiafya!!? They use their world famous mass medias to brand and terrify the world, let us wake up and think our own ways on how to save from their way,

We shall over come.
 
Umesomeka mkuu
 
Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza mpango wa muda kuhusu jinsi nchi zitakavyopewa chanjo za corona mwaka huu, huku Tanzania na Burundi zikiwa hazimo.

WHO imesema kuwa chanjo hizo ambazo ni dozi milioni 336 za AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa muhula wa kwanza na wa pili wa mwaka 2021.

Katika awamu hii, nchi zitapewa kwa sawa na 3.3% ya watu katika kila nchi katika mpango huu, kulingana na malengo ya shirikisho la chanjo duniani (GAVI) ya utoaji wa chanjo kwa 3% ya wakazi wa dunia katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka 2021.

Wiki iliyopita Rais John Pombe Magufuli aliwatahadharisha viongozi kutopokea chanjo za corona ambazo alisema zinaweza kusleta athari kwa raia.
Baada ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Covid,hivi karibuni serikali ya Burundi militangaza mkakati mpya wa kupambana na Covid-19, ikiwa ni pamoja na kufunga mipaka ya maji na nchi kavu na uvaaji wa barakoa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Katika orodha ya awali kuhusu mpangilio wa nchi zitakazopata chanjo katika eneo la Afrika Mshariki Tanzania na Burundi hazimo.

Nchi nyingine za Afrika ambazo hazimo katika orodha ya upokeaji wa chanjo ni pamoja na, Equatorial Guinea, Eritrea, Gabon, Lesotho, Madagascar na Ushelisheli

Shirika hilo la afya duniani linasema kuwa nchi ambazo hazimo katika orodha yake ya kupewa chanjo ya corona ni kwasababu "zilijinunulia chanjo zake zenyewe, hazikuomba chanjo, au hazijawekwa bado katika orodha ya nchi zitakazopewa chanjo ".

Kulingana na orodha hiyo ya WHO za kanda hii ya Afrika Mashariki na Kati zitapewa dozi kama ifuatavyo:

DR Congo: 6,948,000
Kenya: 4,176,000
Rwanda: 1,098,960
Sudan Kusini: 864,000
Uganda: 3,552,000
Kuna shida mgosi

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuna siku tumewaambia mabeberu kuwa tunataka chanjo au ndio wanajitongozesha kwetu?
Kwasasa Nchi ina Changamoto ya upungufu wa Madarasa, upatikanaji wa maji upungufu wa Matundu ya vyoo na Changamoto hii ni yamiaka ming sanaa miaka60 ya Uhuru bado tunaongelea hizo changamoto Halafu Anatokea Mjinga Mmoja Anasema eti Rais aongezewe muda hata kama hatak Alazimishwe!
 
Back
Top Bottom