Tanzania na Misri wakubaliana juu ya kuendelea na mradi wa uchimbaji wa visima na mabwawa

Waziri anafanya kazi kwa maelekezo ya rais,acha kumsifia bwege wako,suala la kimataifa Kama Hilo unamsifia Waziri!?
 
Hivi kwa nini huwa tunajiaibisha kwa kuomba vitu vidogo vidogo sana? Kweli hata visima lazima tuombe Wamisri watusaidie? Ile wakala ya uchimbaji visima na mavifaa yote waliyonayo kazi yake ni nini?

Au ukishaingiwa na pepo la kuomba omba huwa halikutoki tena?
 
Njaa mbaya sana..yani maji ya ziwa Victoria ndio hatuyagusi tena..viongozi wa hii nchi sijui hawaoni kama huu ni mtego.

#MaendeleoHayanaChama
 
Misri ni rafiki wa Tz kwa muda mrefu. Lakini hii omba omba hata kwenye kuchimbiwa visima na mabwawa?
Waafrika tujiheshimu kiasi, Misri yenyewe inategemea misaada toka ndugu zao nchi za Ghuba.
 
Hiki kinachofanyika sasa kuhusu visima kilianza miaka ya 2000 kama utapeli ili kuifanya Tanzania yenye influence katika ziwa Victoria iende kinyume na makubaliano na washirika wengine! huu si mradi ni utapeli
Tumesema, tumeonya, tumeshauri, tumepiga kelele lakini nani atusikilize? Ndugu zangu Watanzania tunakoelekea si kuzuri. Watu pekee ambao kwa sasa wanaruhusiwa kuzurura ndani ya nchi hii wakitafuna kodi zetu na kuwadanganya wananchi wasiojua kinachoendelea ndio hao hao wanatuingiza kwenye mikataba ya hovyo kama hii.

Hivi sasa wenye mawazo tofauti wamepigwa stop hayo mawazo yao yasiwafikie wananchi na kuwazindua pesa zao zinavyochezewa na serikali hii. Tunawekeana mikataba na matapeli ambao hawana nia yoyote ya kutukwamua bali kutudidimiza hapo hapo tulipo. Eti Misri leo watuchimbie visima huku tukitembelea ma V8, tunamdanganaya nani?

Kuchimbiwa visima ili turuhusu maji ya ziwa Victoria yawanufaishe Waarabu wa Misri, hizi akili amekuja nazo nani kama si hao hao wanaotembelea ma V8? Visima gani hivyo tunashindwa kuchimba wenyewe hadi tusaidiwe na Wamisri ? Wao wenyewe ili wajiendeleze wanahitaji misaada kutoka kwa watu wengine wenye uwezo na sifa zaidi yao?

Huu ni uendawazimu!
 
Tunataka tutumie maji ya Ziwa victoria. Misri waache Janja yao ya kutuchimbia visima ili tusivune maji ya ziwa victoria
Ndiyo kitu cha kwanza kilichoingia kichwani kwangu, janja janja tuwekwe wazi kama jaotatubana kuvuna maji 'yetu' yaliyo ndani ya ziwa Victoria.
 
Mkuu kwanza niseme 'sikubaliani' nawe kwamba sisi ni wendawazimu! nadhani sisi tuna daraja letu kama si la misukule ni la ndondocha ! Kuna watu waliowahi kusema Watz wana IQ ndogo, tufikirie sana si kuwapinga

Misri wanapata USD Billion 10 kwa mwaka kama msaada kutoka USA ili kulinda interest zao.
Misri wanatoa milioni 200 au 300 kuja kutuchimbia ''swiming pool' ili watu wetu wasitumie rasilimali ya ziwa Victoria kwasababu Waarab wanapanda machungwa , Mpunga na Boat za Watalii pale Cairo! insane

Nyerere na wenzake walitumia Land Rover 109 wakajenga Nyumba ya Mungu, Kidatu, Mtera, wakaongeza Pangani na kwingine

Leo tunasubiri Wamisri waje kutujengea mabwawa mawili kama lile la Mindu pale Morogoro halafu tunapiga picha na kushangilia Mkataba. Miaka 60 ya Uhuru tunafurahi kujengewa swimming pool! insane

Tunaweza kununua V8 hadi kwa makatibu wa CCM wa Wilaya kwa mujibu wa Mheshimiwa Slowslow hatuwezi kuchimba visima hadi waje Waarabu watuchimbie! Hii aibu kwanini hawaioni hawa viongozi?

Ni nani ameidhinisha huu mkataba wa kijinga na ni kiongozi gani atakayeridhia ujinga huu!
Kuna genge la watu 400 wamekaa pale Dodoma na V8 halafu tunaleta Wafuga ngamia kuchimba visima

Waarabu wanachimba visima vya maji, Wajapan wanachimba vyoo vya shule vya matundu marefu kisha wanatukabidhi mbele ya msafara wa V8! Tuna watu wa ajabu sana Taifa hili!

Yes ni watu kwasababu viongozi hao wanaoingia mikataba ya kijinga kama hii wanatoka miongoni mwetu na sisi tunashangilia tu hatukemei

Kama kuna huzuni kwa leo katika Taifa letu basi hii fedheha ya visima vya maji na 'swimming pool' inaongoza

Tuna viongozi wa ajabu sana1 ajabu sana. Hili kweli linahitaji elimu yoyote!
 
Mabwawa mawili yatajengwa wapi? Wananchi watakaofaidika na pia wale watakaopisha mradi kufanyika ktk maeneo yao wanafahamu kuhusu azma ya ujenzi huu au kila kitu ni siri ?
hivi ni vitu muhimu sana kuvijua kuliko wakubwa wa nchi kutupa maelez matup tu
 
Inaamsha hasira kuu
 
Inawezekana Ziwa tunalo, lakini Serikali imeshindwa kulitumia kwa manufaa ya kutatua matatizo ya maji kwa Wananchi. Tuwape fursa Wamisri wafanye yao, huwezi jua, pengine kuna mengi ya kujifunza njiani
 
Let's be open-minded about this agreement; isitoshe kusema, kiujumla, Wamisri wana utaalamu au teknolojia ya tokea enzi ya namna ya kuvuna au kunufaika kwa nanmna mbalimbali kutokana na vyanzo vya maji. Tusiwadharau sababu labda siyo Wazungu.
 
Nadhani huenda kama jamii yetu huenda tuna IQ ndogo kwelikweli na mifano ya IQ yetu ndogo iko reflected kwa viongozi wetu wanaotutawala maana wanatokana na sisi!.
 
Rasilimali tumeikalia karne na karne lakini hata hizo orchards za kilimo cha machungwa hatuna. Si bora Mmisri atuonyeshe amewezaje?
 
Wamisri wana utaalamu au teknolojia ya tokea enzi ya namna ya kuvuna au kunufaika kwa nanmna mbalimbali kutokana na vyanzo vya maji.
What? Hata wewe! Kweli nchi hii tumelaaniwa. Huu mkataba umeingiwa labda kwa sababu dola zimeingia kwenye account za watu. Hii ni awamu ya kuuma na kupuliza kama panya.
Tusiwadharau sababu labda siyo Wazungu.
Kwa akili kama za kwako nilijua ni lazima tu utawaingiza wazungu katika hili. Tumekuwaje Watanzania? Kweli huu ndio mwisho wetu wa kufikiri? Kumbuka kuna historia ndefu katika hili.
 
Nakubaliana nawe kabisa kwamba haiingi akilini hawa watu hawajui nini kinaendelea na Misri.
Si kuna timu ya kujadili mikataba? Ina maana akina Palamagamba hawajui nini kinachotokea!

Ipo siku tutasikia tu walivyolambishwa asali. Hili haliwezi na halina masilahi na Taifa kuna kitu nyuma yake
Kuna shinikizo kuna jambo!
 
Bi tozo anaweza pet issues full stop na hivi anajiona mmanga tutavuna mabua sana.
 
Kuchimba kisima hakusababishi ila over pumping ndio inaweza sababisha kwa kushusha hydraulic pressure.
Japan ishawahi tokea ikabidi waanze kufanya artificial recharge. Maana mji ulianza kudumbukia.
Ninachofahamu ni kwamba kina cha maji kikishuka kwa futi moja huchukua miaka 50 kurudia hali yake ya mwanzo. Tena wakati huo ukiwa huendelei ku pump maji kutoka kwenye kisima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…