Prof Griff
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,772
- 5,258
Sawa Mtaalam Mzalendo.Utafiti na uchimbaji wa visima umekuwepo toka miaka ya 70 katika mradi uliojulikana kama HESAWA. Mradi huu ulikuwa mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga. Lengo la mradi huu ilikuwa kupata maeneo ambayo yana uwezo mkubwa kuzalisha maji mengi kama ilivyo katika bonde la Makutapora Dodoma. Lakini ilishindikana na kuishia kuchimba visima vifupi vilivyofungwa pampu za mkono aina ya Nira na SWN70. Pia mabwawa yalichimbwa maeneo mbalimbali ambayo hivi sasa mengi yamejaa tope.