Tanzania na Misri wakubaliana juu ya kuendelea na mradi wa uchimbaji wa visima na mabwawa

Tanzania na Misri wakubaliana juu ya kuendelea na mradi wa uchimbaji wa visima na mabwawa

Kwani hayo mabwawa ni ya maji ya miamba au ni yale kutegemea chanzo cha mvua za msimu.
 
Let's be open-minded about this agreement; isitoshe kusema, kiujumla, Wamisri wana utaalamu au teknolojia ya tokea enzi ya namna ya kuvuna au kunufaika kwa nanmna mbalimbali kutokana na vyanzo vya maji. Tusiwadharau sababu labda siyo Wazungu.
Basi hiyo technlojia yao waitumie nchini kwao wana eneo kubwa tu la kuchimba visima na mabwawa sisi tuna ziwa let.
 
Katika mambo ambayo Edward Lowassa atakumbukwa akiwa waziri wa maji ni kutetea haki ya Tanzania kutumia maji ya ziwa Victoria. Miradi yote ya maji ya Victoria ni zao la EL kutilia ngumu Egypt kutoruhusu maji

Lowassa alikataa Riparian states kutumia mkataba wa 1929 unaowapa Egypt haki ya maji ya Victoria kuliko nchi husika. Kupitia Nile basin initiative (NBI) nchi ziliamua kutumia maji ya Victoria kwa maendeleo yake
Ethiopia wamewekea ngumu Egypt kiasi cha kutishiwa kuwa na vita lakini hawakubabaika

Hiki kinachofanyika sasa kuhusu visima kilianza miaka ya 2000 kama utapeli ili kuifanya Tanzania yenye influence katika ziwa Victoria iende kinyume na makubaliano na washirika wengine! huu si mradi ni utapeli

Nashangaa kuna viongozi wa nchi hii wanaukubali utapeli huu hadharani! inasikitisha sana

Kwahili tumshukuru Edward Lowassa na ni legacy yake licha ya zigo la madudu alillobeba

JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla
kwa kweli inashangaza sana.mambo kama haya huwezi kuyaona hata kwa nchi ndogo kama malawi.
 
Ninachofahamu ni kwamba kina cha maji kikishuka kwa futi moja huchukua miaka 50 kurudia hali yake ya mwanzo. Tena wakati huo ukiwa huendelei ku pump maji kutoka kwenye kisima.
Ndio maana ikaja Artificial recharge. Ambapo maji sasa yanatoka nje yanaingizwa ndani ya ardhi. Au tuseme opposite ya kupump maji.
 
Mradi huu huwa unaletwa pale ndugu zao katika imani wanapokuwa madarakani. Nchi isiyoweza kuitumia rasilimali yake ya maji katika ziwa victoria na kuruhusu wengine watumie.

Sasa hao wapuuzi wameenda hapo riz calton wamepewa massage wanaanza kuleta upumbavu wa mabwawa na visima. Kuna umuhimu watu kama hawa wawe wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

kaka kuwa muelewa wamisri ni wakristo na waislamu sio waislamu woote nenda shule ya tabia au sivyo utaumia
 
nia ya misri hataki uguse maji ya victoria yupo tayari akuchimbie kila kona mabwawa ya maji
 
Let's be open-minded about this agreement; isitoshe kusema, kiujumla, Wamisri wana utaalamu au teknolojia ya tokea enzi ya namna ya kuvuna au kunufaika kwa nanmna mbalimbali kutokana na vyanzo vya maji. Tusiwadharau sababu labda siyo Wazungu.
Utaalamu wa kushinikiza nchi ambamo mto Nile umepitia zisitumie maji ya huo mto ndiyo unakupa kujisikia open minded? Mbona unatushangaza sana. Kama wanautaalamu wa kuchimba visima wachimbe huko kwao waziachie nchi nyingine ziendelee kuyatumia maji ya mto Nile kama ambavyo Mungu ameiumba dunia. Kitendo cha Misri kujimilikisha mto Nile ni cha kishenzi na ni dharau kwa nchi zote za Africa na AU kwa ujumla.
 
Kwa kweli ipo haja Viongozi wanaohusika na maamuzi kama haya wawe wanatakiwa kuweka majina yao bayana ili huko baadaye hatua ziwe zinachukuliwa pindi wanapoondoka madrakani. La sivyo nchi nzima tunageuzwa mazuzu.
 
Watanzania tuna kila sababu ya kijitathimini, yaani tunatema big G kwa karanga za kuonjeshwa!
 
Utaalamu wa kushinikiza nchi ambamo mto Nile umepitia zisitumie maji ya huo mto ndiyo unakupa kujisikia open minded? Mbona unatushangaza sana. Kama wanautaalamu wa kuchimba visima wachimbe huko kwao waziachie nchi nyingine ziendelee kuyatumia maji ya mto Nile kama ambavyo Mungu ameiumba dunia. Kitendo cha Misri kujimilikisha mto Nile ni cha kishenzi na ni dharau kwa nchi zote za Africa na AU kwa ujumla.
Maji ya huo mradi yanatoka bahari ya hindi? Wapi imeandikwa lengo la mradi ni kupunguza matumizi ya maji ya ziwa? Ziwa limekuwapo tokea dunia iumbwe lakini maji majumbani kwa maeneo yote yanayozunguka ziwa bado ni shida hadi leo, na tumeshindwa kulitumia ziwa ipasavyo kwa mambo mengi. Sasa Wamisri wanakuja kutuonyesha mbinu za kutumia maji ya ziwa, watu kama wewe mnakuja na hoja hasi na illogical.
 
Wamisri hawaji kutuonyesha mbinu za kutumia maji ya ziwa bali wanakuja kutuzuia kutumia maji ya ziwa!
 
Wamisri hawaji kutuonyesha mbinu za kutumia maji ya ziwa bali wanakuja kutuzuia kutumia maji ya ziwa!
That's your opinion, and you're entitled to it. Tuseme sasa lengo ni kuchimba visima ili kuboresha mifumo ya usambazaj wa maji kwa mikoa inayozunguka ziwa, wewe unapinga tu sababu Wamisri ndiyo Wafadhil. Lakini kama mradi huo ungefadhiliwa na Wajapani kwa malengo hayo hayo ungeshangilia.
 
Utakuwa na matatizo makubwa katika tafakuri yako! Wamisri kwa miaka mingi wamekuwa wakipinga matumizi ya maji ya ziwa Victoria na hasa kwa shughuli za umwagiliaji na kuyapeleka nje ya mikoa inayozunguka ziwa, na badala yake wamekuwa wakitushawishi tuchimbe visima na mabwawa. Kwa bahati mbaya visima vingi vilivyochimbwa havina maji ya kutosha kwa matumizi ya miji na pia mabwawa yamekuwa yakijaa matope kwa sababu ya wingi wa mifugo.

Aidha hata kwa miradi ya visima na mabwawa Misri haina uwezo wa kugharimia hivyo wamebaki kung'ang'ania mkataba wa kikoloni kutuzuia kutumia maji ya ziwa.

Hapa siyo suala la kupendelea Japan au wazungu ni suala la maslahi ya nchi! Wamisri hawana nia njema na sisi kuhusu matumizi ya maji ya ziwa.
 
Una ushahidi wa hayo unayodai kutetea hoja zako?
 
Uliza maswali niweze kutoa ufafanuzi, vinginevyo ni vigumu kwa sababu ni mambo mengi.
Sawa, tuanzie hapa, nanukuu;

Kwa bahati mbaya visima vingi vilivyochimbwa havina maji ya kutosha kwa matumizi ya miji na pia mabwawa yamekuwa yakijaa matope kwa sababu ya wingi wa mifugo.
Jee, una ushahidi gani kwa hoja yako hapo juu?
 
Sawa, tuanzie hapa, nanukuu;

Jee, una ushahidi gani kwa hoja yako hapo juu?
Utafiti na uchimbaji wa visima umekuwepo toka miaka ya 70 katika mradi uliojulikana kama HESAWA. Mradi huu ulikuwa mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga. Lengo la mradi huu ilikuwa kupata maeneo ambayo yana uwezo mkubwa kuzalisha maji mengi kama ilivyo katika bonde la Makutapora Dodoma. Lakini ilishindikana na kuishia kuchimba visima vifupi vilivyofungwa pampu za mkono aina ya Nira na SWN70. Pia mabwawa yalichimbwa maeneo mbalimbali ambayo hivi sasa mengi yamejaa tope.
 
Back
Top Bottom