Serikali za Tanzania na Saudi Arabia zimeingia makubaliano ya kusaidiana katika kukabiliana na uhalifu ikiwemo uhalifu wa mitandaoni.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano huo kwa upande wa Tanzania jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Akibainisha maeneo mengine ya ushirikiano huo, Waziri Masauni amesema pia makubaliano hayo yatahusisha namna ya kukabiliana na majanga ya moto, ajali za barabarani na ajali za majini.
Hati za makubalino hayo kwa upande wa SaudI Arabia zimetiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudia, Mwanamfalme Abdul Aziz Bin Saud Al Saudi.
Waziri Masauni yuko nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi.