Tanzania na Sweden kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo

Tanzania na Sweden kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Tanzania na Sweden kuimarisha ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo.

Tareh 19 Machi 2025 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, amekutana kwa Mazungumzo na Waziri wa Uhamiaji wa Sweden Mhe. Johan Forssell.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamegusia namna za kuboresha ushirikiano kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo na uchumi ili kuimarisha uhusiano uliopo kwa takribani miaka 63 sasa.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo viongozi hao walijadili pamoja na mambo mengine kuongeza uwekezaji baina ya pande mbili na kushirikiana zaidi katika masuala ya uhamiaji.

Viongozi hawa kwa pamoja wameazimia kutafuta pamoja na washirika wengine suluhisho la kudumu la kuondokana na wakimbizi na kushirikiana zaidi kuongeza uwekezaji kwa maendeleo endelevu ya pande zote mbili

Mhe. Forssell anahitimisha ziara yake ya siku tatu nchini ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mkoa wa Kigoma kujionea jinsi Serikali kwa kushirikiana na mashirika na nchi nyingine zinavyoshughulikia kwa weledi masuala ya wakimbizi.
 

Attachments

  • publer-1742578833692.jpg
    publer-1742578833692.jpg
    78 KB · Views: 38
  • publer-1742578831683.jpg
    publer-1742578831683.jpg
    76.4 KB · Views: 31
  • publer-1742578821212.jpg
    publer-1742578821212.jpg
    97.2 KB · Views: 32
  • publer-1742578830422.jpg
    publer-1742578830422.jpg
    131.6 KB · Views: 37
  • publer-1742578823122.jpg
    publer-1742578823122.jpg
    126.7 KB · Views: 38
  • publer-1742578825186.jpg
    publer-1742578825186.jpg
    151.2 KB · Views: 32
  • publer-1742578827313.jpg
    publer-1742578827313.jpg
    142.5 KB · Views: 41
Mbona mapema tena

 
Back
Top Bottom