Mnasahau kuwa Kenya tulimnyang’anya huo mradi? Na kwa hali ilivyo ni Museveni tu wa kuliokoa maana Akina Makamba sidhaniJamaa wana roho mbaya wanatamani tuendelee kuwapigia magoti hawataki kabisa tupate unafuu kwa kusimama na miguu yetu wenyewe.
Ishu ya Ukraine na Russia imesumbua sana uchumi wa Africa
Jamaa alikuwa determined. Kwani mafuta ni ya Tanzania na Uganda sasa hao mabeberu shida yao nnSana mkuu nadhani hata angekuepo wakasitisha yeye angeendeleza mradi kwa nguvu
Wanaona kama tutajikomboa kiuchumiJamaa alikuwa determined. Kwani mafuta ni ya Tanzania na Uganda sasa hao mabeberu shida yao nn
Waache uhuniSalaam Wakuu,
Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.
Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania
View attachment 2358292
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.
Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.
Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.
Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Ujenzi umeshaanza,ubavu gani? Hakuna watakacjofanya imeshawakata.Ngoja tuone kama tuna ubavu wa kuwapinga kwa vitendo.
AU ni club tu ya viongozi wa Africa kukutana kupinga soga na kuingiza per-diem....hawana jipya haoNa AU walipoaswa kuiingilia kati moja kwa moja kwa kutoa kauli ya kupinga ukwamishwaji huo.
Wewe Nimekwambia ujenzi inaendelea na uko hatua mbali mbali..Mama sasa aupige Mwingi tumuome!
Hapa hakuna tunawaogopa mabeberu wasitunyime misaadaHivi tuna timu nzuri ya kuweza kutoa hoja kama hizi mbele ya hao mabeberu?
Hawa wanaokuja kujenga hilo bomba wawili wanatokea Ulaya. Mmoja EU mwingine UK sasa wangewauliza kwanza hao halafu wamwendee mchina waulize ni kwa vipi mazingira yatapona.Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini
Shikamoo dadaHawa wanaokuja kujenga hilo bomba wawili wanatokea Ulaya. Mmoja EU mwingine UK sasa wangewauliza kwanza hao halafu wamwendee mchina waulize ni kwa vipi mazingira yatapona.
Mdachi alipoharibu maji ya watu wa Nigeria ya kusini alifanywa nini na je, Nigeria ilisitisha kuuza mafuta yake? Je nigeria iliongea chochote?
Uharibifu wa mazingira tumeufanya sisi kwa mno kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Tuanze sisi bila kusikiliza hao wengine maana hata ukiwaita majina, wenyewe mpaka walipofikia wamepigana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakachoka.
Walitumia mkaa wakachoka ndo wakagundua mafuta kwa waarabu ndo ahueni yao na Mwingereza ndo aligundua hayo mafuta na tunaona mwarabu anavyotamba duniani.
Hakuna mwalibifu wa mazingira kama USA je wamemfanya nini?
Asilimia kubwa ya mradi umebebwa na Uganda kwa hiyo muamzi mkuu ni Uganda but sioni dalili ya chochote kusimama,hizo kampuni za mzungu zinaweza wekewa vikwazo ila tutaendelea na Wachina na pesa za Nchi za Tanzania,Uganda na Sasa DRC 👇Tutawapa hao wazungu Simba mmoja na chui watulie.
JPM ndio anatoa pesa za EACOP,kwani in case wenye mradi ambao ni Uganda wanasanda huyo JPM atafanya nini sasa?Hapa ndio tutajua tofauti ya JPM na SAMIA
Mama anafungua nchi. Kwa Fitna za Kenya utasikia Mradi umepangwa kupitia Kenya ili kulinda mazingira. #mama anafungua nchi.