Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Tanzania na Uganda zapigwa marufuku na Ulaya kuendeleza Miradi ya Mafuta na Gesi

Salaam Wakuu,

Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia Azimio linalozitaka Tanzania na Uganda kusitisha mara moja uendelezaji wa Miradi ya mafuta na Gesi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Wanadai miradi hiyo inaharibu mazingira.

Wakati Bunge la Tanzania likiwa kimya, Bunge la Uganda limelaani azimio hilo walilodai ni kiwango cha juu cha Ukoloni Mamboleo na ubeberu dhidi ya Uhuru wa Uganda na Tanzania
View attachment 2358292

Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Kabaale – Hoima Nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani Mkoani Tanga Nchini Tanzania, ni Mradi wenye urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania.

Bomba linapita katika mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, vilevile linapita katika wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.

Matokeo ya utafiti uliofanywa na kampuni za kimataifa za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za TOTAL, TULLOW na CNOOC ulibaini uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5. Kutokana na ugunduzi huo imebainika uwezekano wa kuvuna mapipa kati ya bilioni 1.2 hadi 1.7. Kutokana na mahusiano ya ushirikiano ya muda mrefu na faida za kupitisha bomba nchini Tanzania Serikali ya Uganda na wawekezaji wa mkondo wa juu waliamua kujenga mradi huu kupitia Tanzania kutoka Hoima Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Lengo la Mradi
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.

Gharama za kukamilisha ujenzi wa mradi wa bomba zinatarajia kufikia takribani Shilingi Trilioni 8 za Kitanzania. Bomba hili lilitarajiwa kujengwa na kuendeshwa na kampuni za TOTAL ya Ufaransa, CNOOC ya China na TULLOW ya Uingereza, kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Waache uhuni
  1. Huenda haya yanakuja baada ya kuombaomba misaada yao
  2. Huenda wana maslahi binafsi watakayokosa kutokana na uwekezaji huo mkubwa
  3. Tufanye kama kule bwawani stiglers watupige wakitaka, vinginevyo watulipe fidia
  4. Kabudi na timu yake tengenezeni vifungu twende mbele
 
Isifike mahali tukaona tunaweza kukabiliana na mabeberu bado tupo nyuma Sana kupata maendeleo ya nchi inategemea zaidi juhudi za mwananchi mmoja mmoja
 
Mama sasa aupige Mwingi tumuome!
Wewe Nimekwambia ujenzi inaendelea na uko hatua mbali mbali..

Ingia hapo EAC forums fungua Uzi wa EACOP utaona Kazi zinaendelea..

Wataishia kupitisha maazimia na hakuna kitu watafanya kuzuia,hizo ni kelele za chura..

Waambie Total wajitoe tunaenda kwa Mchina fasta kuchukua pesa.
 
Hivi ndani ya bunge letu la michongo ni mbunge gani anaweza kujenga hoja juu ya hilo? Pengine kukaa kwao kimya kumeepusha aibu kubwa zaidi maana kama wangeongea hatuna hakika wangeropoka nini
Hawa wanaokuja kujenga hilo bomba wawili wanatokea Ulaya. Mmoja EU mwingine UK sasa wangewauliza kwanza hao halafu wamwendee mchina waulize ni kwa vipi mazingira yatapona.
Mdachi alipoharibu maji ya watu wa Nigeria ya kusini alifanywa nini na je, Nigeria ilisitisha kuuza mafuta yake? Je nigeria iliongea chochote?

Uharibifu wa mazingira tumeufanya sisi kwa mno kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Tuanze sisi bila kusikiliza hao wengine maana hata ukiwaita majina, wenyewe mpaka walipofikia wamepigana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakachoka.
Walitumia mkaa wakachoka ndo wakagundua mafuta kwa waarabu ndo ahueni yao na Mwingereza ndo aligundua hayo mafuta na tunaona mwarabu anavyotamba duniani.
Hakuna mwaribifu wa mazingira kama USA je wamemfanya nini?
 
Hawa wanaokuja kujenga hilo bomba wawili wanatokea Ulaya. Mmoja EU mwingine UK sasa wangewauliza kwanza hao halafu wamwendee mchina waulize ni kwa vipi mazingira yatapona.
Mdachi alipoharibu maji ya watu wa Nigeria ya kusini alifanywa nini na je, Nigeria ilisitisha kuuza mafuta yake? Je nigeria iliongea chochote?

Uharibifu wa mazingira tumeufanya sisi kwa mno kwa kukata miti ovyo na kuchoma misitu. Tuanze sisi bila kusikiliza hao wengine maana hata ukiwaita majina, wenyewe mpaka walipofikia wamepigana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakachoka.
Walitumia mkaa wakachoka ndo wakagundua mafuta kwa waarabu ndo ahueni yao na Mwingereza ndo aligundua hayo mafuta na tunaona mwarabu anavyotamba duniani.
Hakuna mwalibifu wa mazingira kama USA je wamemfanya nini?
Shikamoo dada
 
Tutawapa hao wazungu Simba mmoja na chui watulie.
Asilimia kubwa ya mradi umebebwa na Uganda kwa hiyo muamzi mkuu ni Uganda but sioni dalili ya chochote kusimama,hizo kampuni za mzungu zinaweza wekewa vikwazo ila tutaendelea na Wachina na pesa za Nchi za Tanzania,Uganda na Sasa DRC 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220916-084606.png
    Screenshot_20220916-084606.png
    107.9 KB · Views: 4
Hapa ndio tutajua tofauti ya JPM na SAMIA
JPM ndio anatoa pesa za EACOP,kwani in case wenye mradi ambao ni Uganda wanasanda huyo JPM atafanya nini sasa?

Kwanza sio mradi wa Tzn bali Uganda na Total na Uchina,Tzn tuna shareholder ya 15% tuu so hatuna uamzi popote..

Sie tuko hapa kuunga mkono Ili tuje kunufaika ila Wenye mali ndio hao hao..

Mwendazake alinza uzinduzi na uzinduzi lakini hakuna hata contractor mmja alikuwa site ila Leo hii ujenzi umeshaanza toka mwaka Jana👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220916-083135.png
    Screenshot_20220916-083135.png
    97.6 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220916-083316.png
    Screenshot_20220916-083316.png
    98.7 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220916-083329.png
    Screenshot_20220916-083329.png
    92.3 KB · Views: 5
Mama anafungua nchi. Kwa Fitna za Kenya utasikia Mradi umepangwa kupitia Kenya ili kulinda mazingira. #mama anafungua nchi.

Umeona ehh!
Maana wakenya ni watumwa pasee walahi, sijapata ona mijitu imesoma lakini ikiona mtu mweupe yeyote hata mtoto mdogo watampigia magoti na kuukunja mkia kama mbwa koko [emoji3062]
Fools walahi [emoji2959]
 
Waambieni hao Wazungu wenu ujenzi unaendelea hatuna mda wa kufanya makelele na mapovu yao Wala kujibizana..

Sisi ni Kazi na Kazi inaendelea 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220916-084002.png
    Screenshot_20220916-084002.png
    98.9 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220916-084035.png
    Screenshot_20220916-084035.png
    138.3 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220916-084215.png
    Screenshot_20220916-084215.png
    165.7 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220916-084732.png
    Screenshot_20220916-084732.png
    102.8 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220916-083744.png
    Screenshot_20220916-083744.png
    109.4 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220916-083908.png
    Screenshot_20220916-083908.png
    115 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220916-083714.png
    Screenshot_20220916-083714.png
    140.8 KB · Views: 4
  • Screenshot_20220916-083726.png
    Screenshot_20220916-083726.png
    128.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom