Tanzania na Utani wa Makabila: Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti ukaumia nafsi yako?

Tanzania na Utani wa Makabila: Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti ukaumia nafsi yako?

Kuna njemba wakati wa msiba wa Babu iliingia kaburini inashinikiza asipumzishwe Babu Hadi ipewe gambe na mkwanja. Nilikasirika Hadi nikataka kupasuka lakini ntafanyaje wakati huo nna miaka 15 tu. Yanakera matani ya kikabila ila nasisitiza yaendelezwe maana Yanaleta mshkamano na kuambizana ukweli bila kuoneana haya.

Jamii inapumua kupitia haya matani na kuishi kwa mshikamano.

Tuliosoma social engineering courses tunaelewa dhima ya hili suala.
 
Watani sio watu wazuri kabisa.....kuna wamama wawili kwenye msiba wa mtoto wa ndugu yangu walinifunga kamba kwenye mti kama mbuzi....wanadai hela wakanunue nyama...ati kwa nini kwenye msiba tumepika wali - maharage!?

Ila wakati mwingine wanasaidia sana kuondoa stress na hata kazi kwenye misiba.
 
hahahahaaaa walikufunga kamba kwenye mti
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwa mimi msukuma ni makabila yapi hapa tanzania na nje ya nchi ya tanzania ni watani zangu?

Nimeuliza tu wakuu
 
Back
Top Bottom