Tanzania na Utani wa Makabila: Ulishawahi kutaniwa vibaya na mtu wa kabila tofauti ukaumia nafsi yako?

Nikiwa kwetu kasulu-BUHA sijuwahi kujua utani ni nini. Siku moja bana nikiwa dsm ukatokea musiba, aliyefariki muha, watani wakaja mfipa tena mwanamke na mkurya mmoja. Wacha waanze kuponda, eti ninyi waha mimi siwaelewi. Leo mnachanga hapa hata hela inayotakiwa haijatimia, kama hamjajiandaa si mngetoa matunzo na matibabu kwa marehemu? Mkurya na mfipa wakatangaza hakuna kuchimba hadi tupate hela yote iliyohitajika. Tulijichanga wala haikufika, ili shughuli ziendelee ilibidi tumfunge kamba mkurya, yule mama wa kifipa yeye tulimdhibiti.

Nikauliza, kwa nini wanafanya hivi, nikajibiwa ni watani na musiba wa juzi tuliwamwagia maji wakiwa wamelala
Ntamahoro
 
Mie sitakuja kusahau nimepanda Batco bus ya kwenda Tarime nakutana na wakurya ndani mimi ni Mnyaturu fulani hivi ukweli nilijuta hadi niliamua kushuka njiani alafu yakanirudishia na nauli yangu wenyewe na kunipa na hela ya kula
 
Sipendi mtu anitanie kuhusu maumbile. Mfano angalia xx yako, kuna siku walikuwa wanataniana kuhusu miguu, Mimi nilikuwa nacheka tu, nadhani kuna mtu alinionyeshea bila mimi kujua, huyu mama akajibu sasa huo mguu? hilo ni tende. Miaka mingi imepita lakini bado naumia japo aliyeongea ni mtani wangu, nitanie chochote sio kiungo katika mwili wangu. Jana mwingine kanitania kitu nimeumia sana, namuheshimu ila ni lazima nimwambie asinitanie tena
 
Wanyaki watani zao ni kabila gani ?
Maana hawa watu watata
 
Mie sitakuja kusahau nimepanda Batco bus ya kwenda Tarime nakutana na wakurya ndani mimi ni Mnyaturu fulani hivi ukweli nilijuta hadi niliamua kushuka njiani alafu yakanirudishia na nauli yangu wenyewe na kunipa na hela ya kula
Hao wanajua utani, walijua umekasirika wakakupoza kiaina
 
Kuna dogo anaperuzi JF kama "mgeni" kaomba nimuwekee jinsi alivyotaniwa na mkurya alipoingia mjini Mwanza mara ya kwanza,(dogo ni mhyaya) kazi aliyokuwa anafanya ni usaidizi katika ujenzi, huko alikotoka Bukoba hakuwahi kukutana na tofari zito la saruji, dogo kubeba matofari kama 10 kupandisha juu akawa amechoka vibaya na ndipo mkurya akamutania hivi: .."uliposikia dada yako anapigiwa simu huko kijijini kuwa njoo makoroboi imechangamka ukadhani imechangamka kwa wavulana! ni wasichana tu tena inachangamka usiku..."
dogo anasema alitamani kuacha kibarua ila akajipa moyo anasema mpaka leo neno hilo huwa linamuuma
 
Ukinitania kwenye msiba wa ndugu yangu nakulima buti mara mbili ya alopigwa mbasha.
 
Duuuh ila mkuu kama hujazoea ni kali ila siku hizi nimewazoea
Kazini nilikuwa na Kaka yangu ( kabila moja) yeye walipomzoea walikuwa hawamtanii, Kwanza ujue Kwa kazini mtani ndiye anayeweza kukuambia ukweli, sasa ukiona mtani anakutania pima sana ni utani gani, anaweza kuwa katumwa akupe ujumbe Kwa njia ya utani au ni utani tu. Sasa yule Kaka ikiwa utani anacheka, kuna siku Mzee mmoja kamwambia ulifikiri kuishi na mke rahisi, tangu umeoa kila siku unaongeza tundu la mkanda kitambi chote kwisha na bado [emoji2][emoji2][emoji2] Mzee hakuendelea maana alilambwa vibao viwili vya nguvu hadi chozi jamaa karudi ofisi kwake kimya baada ya kusemwa na wakubwa akamuomba msamaha na kumpa 10,000 wakasameheana.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuna jamaa mmoja nilikuwa jirani naye siku ya msiba wa mdogo wake nilisikia anaambiwa akapake miguu mafuta imekauka jamaa alivaa pensi na mtisheti mrefu kama wa lemutuz ambazo ni nguo anazoshinda nazo kila siku ni kweli miguu yake inaonekana haijawahi kupakwa mafuta siku ile aliporushiwa hilo dongo ikabidi nijitenge na kundi nikaenda kuchekea kando
 
Likizo moja baada ya msiba wa baba nilisimama barazani na wifi zangu mara kapita mama wa kihaya kaolewa na mgogo , wifi mmoja ni muha na Mimi naingia utani kwa mgogo yule bila salam akasema yaangalie mmemuua Baba yenu ili mfaidi nyumba, mmejitandaza hamjui thamani yake wanga wakubwa nyie, halafu kaendelea na safari yake hakusubiri jibu, niliumia sana wakaniambia mtani huyo.
 
Kuna njemba wakati wa msiba wa Babu iliingia kaburini inashinikiza asipumzishwe Babu Hadi ipewe gambe na mkwanja. Nilikasirika Hadi nikataka kupasuka lakini ntafanyaje wakati huo nna miaka 15 tu. Yanakera matani ya kikabila ila nasisitiza yaendelezwe maana Yanaleta mshkamano na kuambizana ukweli bila kuoneana haya.

Jamii inapumua kupitia haya matani na kuishi kwa mshikamano.

Tuliosoma social engineering courses tunaelewa dhima ya hili suala.
Ukiachana na utani wa kupitiliza utani una faida kubwa. Wengi tumefanikisha mengi kupitia watani zetu. Ukienda eneo la ugenini na ikatokea ukamkuta mtani wako huko hakika hautakuwa mpweke. Watani ufanikisha sherehe na hata misiba kwa sababu uhamasishana wenyewe kwa wenyewe na kuhamasisha wengine na kufariji wafiwa. Sitasahau jioni ya siku moja niliyoshuhudia baba yangu mzazi akipigana mieleka na mtani wake barabarani hadi wakaangushana chini mavumbini huku wote wakicheka kwa furaha. Kilichopelekea kupigana mieleka ile ni kule baba na mtani wake kutambiana kila mmoja kwamba ni mbabe na hawezi kuangushwa na mwenzie. Siku mzazi wangu alipofariki yule mtani alilia kama mtoto. Anaebeza utani yawezekana bado hajakua na kama kakua hajakulia katika haya mazingira yetu ya kiafrika. Na kama kakulia katika mazingira yetu ya kiafrika basi kakua mwili tu lakini si kiakili.
 
Umeandika point nzuri sana.
 
Back
Top Bottom