Tanzania na vifo tata vya watu bila Postmortem Wala kumhusisha Coroner

Tanzania na vifo tata vya watu bila Postmortem Wala kumhusisha Coroner

Hiki kifo kimetokea wakati mbaya sana, ndio maana kimeacha maswali mengi vichwani mwa watu.

Inawezekana kweli sababu ikawa ni hiyo tuliyoambiwa na daktari wake, au pia ikawepo nyingine zaidi ya hiyo, lakini hao wenye jukumu la kufanya huo uchunguzi watafanya hivyo?

Kawaida yao wamezoea kujikausha, hawajihangaishi miaka yote na malalamiko ya aina hii, hasa tukikumbuka vizuri sintofahamu ya aina hii ilianzia kwenye kifo cha Nyerere, ikaja kwa Magufuli, leo kwa Membe, who will be next...
 
Nchi haina pathologists tangu Professor Shaba afariki dunia, eti hawa medical assistants, GP ndio watoe uchunguzi ni craze, as far wewe sio royal families 👪, endelea kulalama huku wakati wateule wapo serengeti restaurant wanapata lunch
 
Nchi haina pathologists tangu Professor Shaba afariki dunia, eti hawa medical assistants, GP ndio watoe uchunguzi ni craze, as far wewe sio royal families 👪, endelea kulalama huku wakati wateule wapo serengeti restaurant wanapata lunch
Kwani Prof. Shaba alikufa lini?
 
Katika nchi zilizostaarabika kifo cha mtu huhitimishwa kwa postmortem (kujua kamili chanzo cha kifo) na inquest ambapo ofisi ya Coroner huhhsika. Kifo hakiishii na mambo ya tiba peke yake.

Mtu anaweza kuwa alikuwa mgonjwa mahututi hospitali, lakini kafa kwa sumu au hata kuchomwa kisu huku akiwa ICU.

Sababu za vifo zinaweza kuwa nyingi. Bila Postmortem au inquest wala ofisi ya Coroner kujihusisha kikamilifu, nadharia za michezo michafu zitaacha kuwapo vipi?

"Kama kachero mbobezi, baada ya kuhojiwa Dodoma alielekea kwenye hoteli isiyojulikana kupata chakula kizuuuri, Kwa nini isiwezekane kuwa alipata chakula tata kutokea kwenye hoteli inayojulikana?"

Vifo vya wengi vimeacha maswali mengi. Watu wanafia mikononi polisi katika mazingira yasiyokubalika. Wengi, wakubwa kwa wadogo wanakufa wengine ghafla, na sababu zinazotolewa zinakuwa haziridhishi.

Tuyafukue makaburi ya wafu wetu wote tusiokubaliana na maelezo yaliyopo. Kwani ya wafanya biashara wa Ifakara ilikuwa je?

Hadithi za kuandaana kufa kuwa kila nafsi itaonja mauti, bwana hutoa na kutwaa, nyuma yao mbele yao nk zinahitaji maboresho ya haraka. Vinginevyo binadamu watoa roho za watu tuishio nao mitaani nyusoni mwao nao ni kama watu tu.

Kama nchi tuna tatizo la kukubali vifo vya watu bila Postmortem wala inquest.

Kenya wametuzidi Sana kwenye haya.

Katiba mpya itabidi kuwa wazi kwenye hili. Kila kifo kihitimishwe kikamilifu kisheria zaidi ya si ki tiba peke yake.

Postmortem, inquests na ofisi yenye kuwajibika ya Coroner haviepukiki kwenye dunia yetu ya leo ya kutangulizana kimaskhara sikhara mbinguni bila kupenda.
Virusi vinavyogandisha damu na kuzuia mapafu kupokea hewa......elewa hilo ndio chaka
 
Tuna ndugu zetu wengi wamekufa hata Kwa kujinyonga kwa vyupi mikononi mwa polisi.

Hai ndiyo tunaotaka kuanza nao bila kuachwa jiwe juu ya jingine.

Kulikoni makasiriko yote hayo?
huyo ni mkumambavu achana nae
 
Hapa wa kulaumiwa ni makamba kwa kutomuorodhesha membe katika lile kundi la watu wema wasiokufa
 
Kwani Prof. Shaba alikufa lini?
Acha upumbavu, ukijua then itasaidia nini katika uzi huu?,nilichochangia ni kuwa since Professor Shaba afe,nchi haijawahi kuwa na pathologists ndio maana sasa hawa medical assistants,GP eti ndio wanafanya hii kazi wakati sio wataalamu wa kazi hiyo,pls soma comment ili uelewe lengo la mchangiaji
 
Acha upumbavu, ukijua then itasaidia nini katika uzi huu?,nilichochangia ni kuwa since Professor Shaba afe,nchi haijawahi kuwa na pathologists ndio maana sasa hawa medical assistants,GP eti ndio wanafanya hii kazi wakati sio wataalamu wa kazi hiyo,pls soma comment ili uelewe lengo la mchangiaji
Wewe huyo Prof. Shaba ulishiriki mazishi yake au unaandika tu habari usozijua?
 
Tumlaumu Mzee makamba kwa kumsahau membe kwenye orodha ya watu wema Tanzania ndio maana amekufa

Watu wema tanzania hawafi orodha ilitajwa dodoma

Mkuu angekua baba ako au mama ako mzazi
Ukaambiwa njoo uchukue mizoga yako
Yaan baba na mama yako wakaitwa mizoga utafurahia eeeee............
 
Wewe huyo Prof. Shaba ulishiriki mazishi yake au unaandika tu habari usozijua?
Mkuu tatizo lipo wapi kuhusiana na professor huyu?,kwani hakua pathologists?,nilipokua pale Monduli chuo cha kijeshi, kuna very interesting story kuhusu professor huyu kwa kutumia fuvu la kichwa wa cadet aliyekufa mafunzoni na hakujulikana, ila utaalamu wake aliweza kujua mwenye lile fuvu, debate hapa sio professor ni watu kuzikwa bila ya postmortem!!
 
Back
Top Bottom